Tanzania imezuia madereva wa Kenya kuingia nchini humo

Ninarudia tena kwamba, ninyi wakenya uwezo wenu wa kuekewa ni mdogo sana, uwezo wenu wa kufanya analysis ni mdogo mno. Hivi wewe unadhani umuhimu wa nchi ni katika volume of trade pekee?.

Ngoja nikuulize swali, kati ya Pskistan inayonunua chai kwa wingi toka Kenya, na Tanzania inayowauzia chakula kwa bei ndogo na mnakipata kwa wakati muafaka, ni nchi ipi ni muhimu?, japo "volume of trade in terms of cash" inaonekana ni kubwa kati ya Pakistan na Kenya, lakini Tanzania ni muhimu kwa sababu ya umuhimu wa chakula kwa Kenya ambacho ni bei nafuu na kinapatikana kwa wakati.

Kati ya UK inayonunua maua toka Kenya na ninyi mnanunua silaha na "spare parts", na Tanzania ambayo inawauzia Mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyenu, ni nchi gani ni muhimu zaidi?, japo " raw materials" bei zake zipo chini hivyo kuonyesha kwamba volume of trade kati ya Tanzania na Kenya ni ndogo ukilinganisha na UK, lakini bila raw materials toka Tanzania, viwanda vya Kenya vitakufa kwa sababu sio rahisi Kenya kuagiza "raw materials" kama pamba, mbao, ngozi, karatasi, toka nchi za mbali.

Mwisho ni kwamba, Kenya imewekeza zaidi Tanzania kuliko nchi yoyote ile hapa duniani, makampuni ya Kenya ni takriban 600, japo uwekezaji huu hauonikani katika volume of trade, lakini ni muhimu kwa uchumi wa Kenya kuliko hizo trade kati ya Uganda na Kenya.

Vivyo hivyo kuhusu biashara na nchi za kusini mwa Africa. Historically Kenya haikuwa na mahusiano mazuri na nchi za Kusini mwa Africa kutokana na kutoshiriki kwake katika ukombozi mwa Africa, na kuegemea "western block during cold war", baada ya "cold war" kumaliza, sasa hivi Kenya inapanua masuko katika nchi za COMESA, 75% za wanachama wa COMESA ni nchi za kusini mwa Africa, ambazo nyingi ni landlocked countries, bila Tanzania Kenya haiwezi kuzifikia.

Viongozi wenu wanajua umuhimu wa Tanzania, ndio sababu walipoambiwa wachague kati ya UK au TZ, waliamua kuichagua TZ na kuachana na UK.
 
Kenya na Tz tunategemeana sana hususan upande wakenya kwasababu mnanunua matunda, mchele,mahindi na vingine kibao kutoka Tz kwa bei nafuu ambayo hamuwezi sehem nyingine yoyote hapa duniani na sisi tunawategemea kwenye makampuni yenu yanayofanya investment hapa Tz lakin nyinyi ndio mna gain sana kwenye huu ujirani kuliko sisi ndio maana serikali yenu haiwez kufanya chochote juu yetu all in all tunategemeqnaa sana ila nyinyi wenzetu mnataka kuleta ubabe ,na very soon mtaanza kununua sukari kutoka bongo kwa wing na gesi
 
Inabidi tuwawekee ngumu!
Wamekuja kupiga magoti baada ya Magari yao kufungiwa, hawa jamaa bila Tanzania hawana maisha.
Tony254,
Hamuwezi kukaa ngumu. Kenya ni kama yule msichana mpenzi wako wa kwanza uliyekuwa ukimpenda hata kushinda mke wako wa sasa. Yaani hata akikukosea unamsamehe hata kabla yeye kuomba msamaha. Tegea kesho utasikia kwamba border imefunguliwa. Mnatupenda na hilo linaonekana wazi.
 
Sasa mbona mnakuja kupiga magoti wakati ninyi ndio mliazuia mahindi yetu bila kutujulisha?, hivi mnajisikiaje kila mara mnapoanzisha chokochoko ambazo mwisho wake mnakuja kupiga magoti?.

Hii ndio ikionyeshe kwamba Tanzania ni muhimu kwa Kenya kuliko nchi yoyote, UK ilipiwaweka katika redlist, hamkutuma ujumbe wowote, lakini tulipozuia Magari yenu, mnatuma ujumbe haraka haraka.

Ninarudia tena, Tanzania ni nchi muhimu kwa Kenya kuliko nchi yoyote ile.
 
Sasa unajisifu? Mbona usingoje usifiwe?
 
Ugly truth Ugly truth
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…