SI KWELI Tanzania imezuiliwa kuingia Marekani

SI KWELI Tanzania imezuiliwa kuingia Marekani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Screenshot 2024-12-05 140828.png
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zitazuiwa kuingia nchini Marekani baada ya rais Trump kuingia madarakani rasmi mwaka 2025 zilisambaa zaidi siku ya Desemba 4, 2024. Tazama hapa, na hapa.

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa wengi waliotoa taarifa hiyo ama kuulizia uhalisia wake waliipata kutoka kwenye taarifa ama muongozo uliopo kwenye tovuti ya chuo kikuu cha Cornell nchini Marekani. Taarifa hiyo imeelezea kuwa huenda uongozi mpya wa Trump ukaleta sheria mpya ya uhamiaji ambayo inaweza kuzizuia baadhi ya nchi kuingia nchini humo ikiwemo zile ambazo zilizuiliwa katika utawala wa kwanza wa Trump.

Ufuatiliaji umebaini kuwa Tarehe 31 January, 2020 Marekani ilitoa tangazo kuhusu kuboresha mchakato wa uingiaji nchini mwao, ambapo walizua baadhi ya mataifa kupata viza ya kuingia nchini humo. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo lakini zuio lililotolewa kwa Tanzania halikuwa kwa viza zote na badala ilizuiwa kushiriki kwenye via za bahati nasibu.

Sababu zilizotolewa ni kuwa Tanzania ilishindwa kutoa baadhi ya taarifa kwa yanaoyoendelea nchini ikiwemo hali ya usalama wa umma, huku nyingine zikitolewa kwa kasi ndogo sana.

Muongozo wa chuo cha Cornell kwenda kwa wanafunzi wake, wahadhiri na wafanyakazi kuelekea muhula mpya

Chuo kikuu cha Cornell ni chuo binafsi cha tafiti kilichopo nchini Marekani katika jimbo la New York, pia kina ushirika na chuo kikuu cha New York. Cornell walitoa muongozo wenye jina (Guidance: Possible Immigration Changes in 2025) tarehe 26-11-2024 wa kuwatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wao kutokea mataifa ya nje wakiwataka warudi kwa wakati ili kuepusha kukutana na kadhia ya kuingia katika Taifa hilo kutokana na uongozi mpya wa Donald Trump kuanzia 2025.

Muongozo huo unaeleza kuwa huenda kukawa na sheria mpya ya uhamiaji itakayoanza kutumika mara baada ya uongozi wa rais mpya wa Marekani kuingia madarakani mwaka 2025. Ambapo wamegusia kuwa huenda sheria hiyo ikaathiri baadhi ya nchi ambazo zilipigwa marufuku kuingia nchini Marekani katika uongozi wa awamu ya kwanza wa Trump (2017-2021) nchi hizo ni Kyrgyzstan, Nigeria, Myanmar, Sudan, Tanzania, Iran, Libya, North Korea, Syria, Venezuela, Yemen, na Somalia. Na mataifa mapya yanayotarajiwa kuongezwa kwenye orodha hiyo ni China na India. Kwenye aya ya kwanza ya muongozo huo waliandika kuwa;

"Marufuku ya kusafiri inatarajiwa kuanza kutekelezwa muda mfupi baada ya kuapishwa. Marufuku hiyo huenda ikajumuisha raia wa nchi zilizolengwa katika utawala wa kwanza wa Trump: Kyrgyzstan, Nigeria, Myanmar, Sudan, Tanzania, Iran, Libya, Korea Kaskazini, Syria, Venezuela, Yemen, na Somalia. Nchi mpya zinazoweza kuongezwa kwenye orodha hii, hasa ni China na India".

Madai ya Tanzania kuzuiliwa kuingia Marekani

Madai ya Tanzania kuzuiliwa kuingia nchini Marekani katika awamu ya kwanza ya Rais Trump na kubaini kuwa, Tanzania mwaka 2020 ilipigwa marufuku kushiriki bahati nasibu ya Visa ya Marekani (Diversity Visa) ambapo raia wengine waiokuwa wanahitaji kwenda kwa ajili ya utalii na biashara waliruhusiwa na halikuwa zuio kwa raia wote.

BBC waliandika kuwa viza hiyo ya bahati nasibu hutoa viza kwa takribani watu 50,000 kutoka kwenye nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani. Ambapo mara baada ya maombi hayo idara ya taifa hutumia kompyuta kuchagua watu bila mpangilio miongoni mwa wale waliotuma maombi hayo kwa idadi iiyokusudiwa.

Chuo cha Cornell katika muongozo huo hakikuthibitisha moja kwa moja kuhusu uwepo wa mabadiliko ya uhamiaji na badala yake wameeleza kuwa;

‘’Mazingira ya uhamiaji huenda yakabadilika chini ya utawala mpya wa rais. Mwongozo huu unalenga kuwajulisha na kuwasaidia wanafunzi wa kimataifa, wahadhiri, na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Cornell. Unategemea taarifa zinazopatikana kwa sasa na unaweza kubadilika kadiri ukweli na sera zinavyobadilika.’’

Athari ya muongozo huo kwa baadhi ya wanafunzi

Tovuti ya global times inaeleza kuwa baadhi wa wanafunzi na wahitimu kutokea nchini China walioahirisha safari zao kuelekea nje ya marekani ili kuepuka kukutana na kadhia hiyo. Na hata kwa wanafunzi ambao vyuo vyao havijatoa matangazo ama taarifa hiyo kuhusu tahadhari lakini wameamua wao wenyewe kuahirisha safari zao ili kutokumbana na changamoto wakati wa kurudi.

=

Taarifa hiyo ilikuwa ni tahadhari ya kutoka kwa chuo hiko kwenda kwa wanafunzi wake na watumishi, na siyo uthibitisho kamili wa kuwa nchi hizo zimezuiliwa na hata hivyo chuo hiko kimegusia kuwa huenda nchi hizo zitazuiliwa, wametoa maoni yao kuwa huenda nchi zilizopata changamoto katika awamu ya kwanza ya u rais wa Trump huenda zitaathirika.
Back
Top Bottom