SoC04 Tanzania inahitaji Ilani ya Taifa na si ya vyama vya siasa

SoC04 Tanzania inahitaji Ilani ya Taifa na si ya vyama vya siasa

Tanzania Tuitakayo competition threads

KijanaHai

Member
Joined
Aug 7, 2022
Posts
7
Reaction score
6
Utangulizi

Tanzania inalindwa na katiba kama sheria kuu na kilanja mkuu wa sheria zingine zote zilizopo na zitakazotungwa nchini. Maendeleo ya Tanzania yanaratibiwa na kulindwa na mihimili mitatu Serikali, Bunge na Mahakama lakini yanapangwa, kutungwa kuongozwa na kutekelezwa kwa kufuatwa mifumo tungishi ambatano minne Sera, Sheria, mpango mkakati na bajeti yote hiyo ikisimamiwa na serikali kama muhimili mkuu wa utekelezji na ufuatiliaji serikai, ambayo imechaguliwa kuingia madarakani kwa kushinda kihalali wakati wa uchaguzi mkuu unaofanyika kila baadaa ya miaka mitano kumchagua rais, mbunge na diwani, serikali ambayo inatokana na chama cha siasa baada ya kunadi mambo yalioandikwa katika nyaraka iitwayo ILANI wakati wa kampeni mgombea akilezea wananchi namna gani icho chama cha siasa endapo kitapewa ridhaa ni namna gani kitaongoza serikali na matatizo yapi ya wananchi na nchi kimayapa kipaumbele kutatua kipindi cha uongozi, ili tuweze kupima utendaji na utekelezani wa ahadi za vyama tunahitaji ILANI itokanayo na wananchi vyama vije vishindane kunadi mikakati na mipango waliyoandaa,Yenye Kupimika, Kutekelezeka, Uhalisia na yenye Mda Maalumu inayojibu mambo yatokanayo na ilani ya Taifa.

1200px-Flag_of_Tanzania.svg.png

Picha:Wikipedia

Kwanini Tunahitaji ILANI ya Taifa?

ILANI ni nyaraka inayoandaliwa kuonyesha matatizo na mipango ya taasisi za kisiasa zinavyoyaona matatizo na changamoto za wananchi na vipi wanatamani kutatua kwa mujibu na mtazamo wao. Ivyo chama husika kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi watumishi wote mpaka wa umma hujikita katika kutekeleza Ilani ya chama bado tunakosa kipimo sahihi cha namna gani chama kimebeba uwajibikaji.

Changamoto na Shida za watanzania na Taifa haziwezi kutatuliwa na mitazamo na hisia za makundi ya upande mmoja bali sauti zilizoskilizwa na kukusanywa nchi nzima na wananchi wote wamekuwa sehemu ya kufikiria matatizo yao na nchi kwa kujadili njia zipi wanahitaji kutumika kutatuliwa kabla ya kufanya uchambuzi wa kitaalamu, hii inaenda sambamba na uandishi wa miradi ya kutatua matatizo ya kijamii sehemu kubwa ya tatizo ni lazima jamii husika iwe imeshirikishwa lisiwe tatizo dhaania ambapo taasisi au mtu amelibuni kichwani kwake, na huu ni mfumo ambao unatumiwa na serikali na wadau wengine wa maendeleo pindi wanaophitaji fedha, mkopo au rasilimali fedha kutoka vyanzo tofauti tofauti, kwanini tusifanye ivyo pia kwenye kuandaa Ilani ya Taifa ambayo wananchi wameshiriki moja kwa moja bila ubaguzi wa kisiasa kidini na mitazamo.

IMG_20240526_160019.jpg

Twitter😡RaiNewspaper

Kuna maswala mtambuka kama Afya, Ajira, Elimu, Kilimo na Ufugaji, Tehama( Sayansi na Teknolojia na Ubunifu), Uongozi na Utawala bora, Ulinzi na Usalama, Uchumi, Rasilimali, na mswalaa ya Sanaa,burudani na Michezo n.k ni lazima ushiriki wa wananchi nchi nzima uwepo kwani wao ndo wenye kuathirika na kunufaika na matokeo katika maeneo yote na wanajua wanaathirika kwa namna gani na kuna namna wao wanatamani njia fulani zitumike kutatua, maswala haya hawawezi kuwa Ajenda ya chama kuamua yapi kwao ni matatizo na yapi ni kipaumbele kutatua wakati hao wanaoenda kutatuliwa hawajashirikishwa.

Matatizo na Changamoto ni Ajenda ya wananchi ivyo kuwa na Ilani ya Taifa ndo suluhu ya kukomesha ahadi hewa za wagombea na vyama kwakuwa itakuwa imebeba Ajenda ya wananchi na sauti za wananchi vyama vya saiasa vije kunadi mikakati na mipango yenye kupimika kwa kiingereza linatumika neno ( SMART),ivyo wakati wa kampeni vyama vije vijibu maswali yafuatayo ( Nini, Wapi,Lini, Kwanini, Jinsi Gani) kwa kiingereza zinatafsiri ( What,Where,When,Why and How) majibu katika maswali hayo yatokane na Ajenda za wananchi na vipeumbele vitakavyotokana na ILANI ya Taifa ambavyo vitagawanyika kimkoa, wilaya ,kata, kijiji na mitaa.

Ilani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi lakini imefika wakati tuandae ilani ya taifa inayobeba sauti shirikishi za watu wote pasipo kubagua makundi yao na vyama vya siasa kuja kunadi mpango na mikakati ya kutataua changamoto na vipaumbele wananchi wavitakavyo itasaidia kuongeza uwajibikaji na ufuatiliaji kwani kwa mwenendo wa sasa ILANI za vyama inabagua makundi mengine ambayo yanaamini katika vipaumbele vya kimitizamo iliyowekwa kwa vyama na makundi yao endapo wao pia wangeshinda uchaguzi.

Inapatikana vipi Ilani?

Mpango huu unaweza kutekelezwa na mihili miwili Serikali, Bunge au Wadau wenye kutamani kuona Tanzania inakuwa na maendeleo endelevu pasipo utememezi na vizazi vijavyo kuwa na utamaduni shirikishi na wenye kujenga umoja wa kutetea na kulinda maslahi ya wananchi na taifa pasipo kufungamana/kufungwa na itakadi za kidini,siasa, kabila na mitazamo kinzani. Ilani ya Taifa inaweza kupitia mchakato ufuatato kwa serikali kukubali na kupitisha sheria ya kukusanya maoni nchi nzima na kupigiwa kura ili kupata ilani yenye malengo ya mda mfupi na mrefu.

Vikao vifanyike Kuanzia ngazi ya mtaa, kata, kijiji,wilaya na mkoa baada ya hapo makundi na vikundi mbalimbali vitashirikishwa kulingana na maeneo twaja yatakayojadiliwa na kupewa umuhimu wake wakati wa ukusanyaji maoni mwisho kuwa na mjadala wa taifa utakao shirikisha wataalamu na wadau wenye kuweza kuchambua na kujadili maswala muhimu mtambuka.

Katika vikao ivyo wananchi watajidili vitu vitatu matatizo, vyanzo na utatuzi wanaopendekeza kutataua changamoto katika meaneo mtambuka Afya, Ajira, Elimu, Kilimo na Ufugaji, Tehama( Sayansi na Teknolojia na Ubunifu), Uongozi na Utawala bora, Ulinzi na Usalama,miundo mbinu, Uchumi, Rasilimali, na mswalaa ya Sanaa,burudani na Mchezo n.k.

Tume iliyoundwa kukusanya maoni itaratibu zoezi la kutunza kumbukumbu na baada ya kukusanywa maoni nchi nzima wadau na wataalamu watakaa kuchambua na kutenganisha maoni ya kimikoa na maoni muingiliano na kulingana na ukubwa wa kila changamoto yatatengwa na kuwekewa kipaumbele.

Baada ya mchakato wa maoni na uandaaji wa nyaraka ya awali wananchi watapiga kura vipaumbele vilivyo wekwa kwa kutumia mfumo wa simu ambapo menu ya ilani ya taifa itatengezwa na vipaumbele pendekezwa kupigiwa kura ili wananchi kuchagua mustakabali wao na matokeoa yatatangazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na ilani ya taifa kuandaliwa rasmi kuchapishwa na kusambazwa katika ngazi ya serikali ya mitaa na mitandaoni ili kila mwananchi kuweza kuisoma na kufanya tathmini na ufuatilaji kama vinatekelezwa na chama kilichopewa ridhaa.


Faida za kuwa na ILANI ya Taifa

Ilani itakuwa ni nyenzo muhimu ya kuongeza uwajibikaji na kupunguza ahadi hewa na zisizotekelezeka kwa wananchi pindi vyama vinavyopewa ridhaa kuongoza nchi vinaposhindwa na wanaporudi itakuwa rahisi kuuliza kwanini jambo flani la kweye ilani hawajatekeleza kwani ukiuliza saizi vyama watajibu halikuwa kwenye ilani yao.
 
Upvote 1
tunahitaji ILANI itokanayo na wananchi vyama vije vishindane kunadi mikakati na mipango waliyoandaa,Yenye Kupimika, Kutekelezeka, Uhalisia na yenye Mda Maalumu inayojibu mambo yatokanayo na ilani ya Taifa
Hili ni wazo zuri sana, tutapata kitu cja kutuunganisha wote kama Taifa, halafu tunabakia kushindana tu kwamba ni nani atatufanikisha mipango ambayo tayari tunayo. Nimeipenda hii.

Ivyo chama husika kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi watumishi wote mpaka wa umma hujikita katika kutekeleza Ilani ya chama bado tunakosa kipimo sahihi cha namna gani chama kimebeba uwajibikaji
Kweli kabisa mwanangu

Faida za kuwa na ILANI ya
Mojawapo nyingine ni kutabirika kwa sera za nchi. Kama ilani ya Taifa imesema tuongeze masoko ya wakulima ndani na nje ya nchi basi mtu atawekeza akiwa na uhakika kwamba aje nani, aje nani Ilaninyetu ni masoko hadi nje ya nchi anajiamini.

Asee ahsante sana kwa wazo hili, watu wa katiba mpya, liunganisheni na hili la Ilani ya Taifa
 
Hili ni wazo zuri sana, tutapata kitu cja kutuunganisha wote kama Taifa, halafu tunabakia kushindana tu kwamba ni nani atatufanikisha mipango ambayo tayari tunayo. Nimeipenda hii.
Ni kweli kabisa hakuna Ajenda unayofanya watanzania kwa pamoja wakahoji serikali inayopewa ridhaa kwasababu kila chama kinakuja na Ilani Yake na mambo Yake wao ni waajiriwa WA wananchi ivyo wao wanapaswa kupewa majukumu ya kufanya na wao watuamie ni njia zipi watatumia kutekeleza majukumu ili kupata matokeo tagemewa ya kazi waliyopewa
 
Hili ni wazo zuri sana, tutapata kitu cja kutuunganisha wote kama Taifa, halafu tunabakia kushindana tu kwamba ni nani atatufanikisha mipango ambayo tayari tunayo. Nimeipenda hii...
Kweli kabisa ni muhimu kuwa na Sera zinazojibu Ajenda za ILANI ya Taifa ivyo kila Sera ya Taifa inavyokuwa inaboreshwa na ndivyo ambayo sera za nchi zitaboreshwa na itasidia wananchi kujiwekea katika maeneo tajwa wakitambua kuwa hatutakuwa na mabadiliko ya ghafla katika maeneo wanayofanyia KAZI au biashara.
 
Back
Top Bottom