Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

najaribu kumfikiria M nakosa majibu anatuchezesha mfumo gani,kisera,utendaji,uteuzi. cjajua ni KIONGOZI WA AINA GANI?nabaki kusema Mambo yote yanaitaji maandalizi.RIP JPM
 
Angalau watu hawatekwi,watu wanapanda madaraja kazini na hajijengei uwanja wa ndege usio na tija kijijini kwake.....na angalau anawaondoa mapema na si kuwabakisha kwa jeuri kama Bashite ili tu kuwakomoa wanaompinga
Hayo mambo yashapita ndugu yangu mwendazake alishajiendea zake. Tujadili mambo ya nyakati hizi. Tanzania yupo Raisi mwingine lakini bado viatu alivyovaa ni vikubwa havimtoshi .
 
Samia akijisimamia tutapata Rais bora sana lakini ni hatari hii staili ya maelekezo kwa remote straight from Msoga. Mbaya zaidi ndio rumours zinazosambaa hadi kwa wananchi wa kawaida na hata "waandamizi" wanajipendekeza Msoga zaidi maana ni kama version ya 2010- 2014 imerejea.
 
..hapo inatakiwa WABUNGE wawe na nia na uwezo wa kumdhibiti.

..bahati mbaya yeye ni mwenyekiti wa chama, na amiri jeshi mkuu.

.
Uwezo wa kumdhibiti wanao kikatiba, labda nia ndio hawana ukichanganya na huo uenyekiti wake.

Kwa muono wangu, urais ni wadhifa ulio juu sana ya uwezo wake.
 
Msoga mtambebesha lawama asizostahili. Tatizo ni uwezo mdogo wa rais mwenyewe.

Kuongoza taifa ni tofauti sana na kuongoza NGO. Kuna mtu kaniambia huyu mama alikuwa karani masjala huko nyuma.
 
Uwezo wa kumdhibiti wanao kikatiba, labda nia ndio hawana ukichanganya na huo uenyekiti wake.

Kwa muono wangu, urais ni wadhifa ulio juu sana ya uwezo wake.

..inawezekana kinadharia.

..lakini ukija kufanya kwa vitendo haiwezekani.

..mbunge wa ccm akileta fyoko-fyoko anaweza kufukuzwa toka kwenye chama na mwenyekiti.

..vilevile kwasababu mwenyekiti ni amiri jeshi mkuu anaweza kutumia vyombo vyake kumdhibiti mbunge / mwanachama mkorofi.

..nadhani unakumbuka tukio la Bashe na Musukuma kukamatwa wakati wa kikao cha CCM.

..ni vigumu sana kujinasua kutoka kwenye " utando " wa ccm, serikali, na vyombo vya dola. Kuna faida kwa CCM kwasababu inawahakikishia ushindi " tutake tusitake." Lakini hasara zake ni kwamba ni mfumo unaofuga uzembe, ufisadi, ukatili, etc etc.
 
Uyo mlete mada ni kahaba fulani asiejielewa
 
Msoga mtambebesha lawama asizostahili. Tatizo ni uwezo mdogo wa rais mwenyewe.

Kuongoza taifa ni tofauti sana na kuongoza NGO. Kuna mtu kaniambia huyu mama alikuwa karani masjala huko nyuma.
Mwambie basha wako basi aje tumpe nchi
 
Kwa muono wangu, urais ni wadhifa ulio juu sana ya uwezo wake.

..nadhani it is up to her kufanya vizuri au kufanya vibaya.

..anachotakiwa ni kutafuta wasaidizi very competent kwenye key ministries wamsaidie kuongoza nchi.

..aupukane na kishawishi cha kutaka kufanya mambo mengi makubwa kwa wakati mmoja.

..zaidi, asijaribu kujifanya anajua kila kitu.
 
Kama mwendazake ndiye alikuwa na sifa ambazo mama hana. Ni kheri mno mama azikose kabisa.

Mama akaze uzi hapo hapo tayari dawa inapenya.
dawa gani tena mambo yanaonekana utelebwe kabisa.
 
Mkuu GENTAMYCINE kinachoendelea kwa sasa, kiutawala, nchini kinafikirisha. Kuna wakati nilitakata kuweka bandiko kuhusu UTASHI WA KISIASA na MAAMUZI MAGUMU. Kwa nini sikufanya hivyo, bado najiuliza. Ila lililo kichwani mwangu bado naendelea kupokea na kuchambua yanayojiri katika utawala wa sasa, kama hilo la TEUZI nk.

Sifa/uwezo wa Mwanasiasa kuamua na kufanya mambo ambayo yataleta matokeo yatakayotakiwa, yamo katika misingi ifuatayo:
1. kuweka ‘utashi wa kisiasa’ ndani ya sehemu nyingine za mfumo fulani wa kisiasa.
2. Mwanasiasa lazima awe na angalau maono fulani – uwezo wa kufanya hivyo akitambua na kubainisha jinsi mambo yanavyoweza kuwa tofauti kutokana na maamuzi yake binafsi.
3. Sifa hizo ziwe ni za mwanasiasa binafsi si kwa pamoja - maamuzi magumu binafsi yenye maslahi mapana kitaifa.
 
Siku 100 zina uhusiano gani na umakini wa mtu? Mbona tunapenda kujiliwaza hata katika mambo yaliyo wazi? Tulishasema toka awali kuwa huyu hana uwezo! Anapenda kusoma kwenye Press kuwa Raisi wa JMT amefanya uteuzi wa fulani fulani kuwa fulani na kisha kukimbilia kwenye mitandao kuona comments. Ni Raisi mtaka misifa.
 
Mkuu naunga mkono hoja. Kwenye para ya 7 mimi nadhani mama amteue/kupata ushauri kutoka kwa Mzee Warioba kuhusu rasmu yetu (wanainchi) ya KATIBA ili mambo yaendelee.
 
Ndugu,
Rais wa sasa, angekuwa alibahatika kujua kabla hata kwa mwezi kuwa uhai wa Jiwe u karibu kukatika, angeweza kujipanga na kuja na orodha kamili za teuzi kwa ngazi zote kama alivyotamani.
Kwa hakika mpaka sasa anafanya vizuri na mabadiliko/marekebisho ayafanyayo BAADA ya muda mfupi ni kielelezo cha uangalifu mkubwa aliyonao, ili madosari ya uongozi aliyoyaona kwa mtangulizi wake, yaachwe hukohuko. Ni kweli kuwa, kuna baadhi ya mambo/vitu vizuri vinaweza hata kuja kuyumba, lakini hizo ndio gharama za mabadiliko ambazo yaweza kuwa sio rahisi sana kuziepuka.
Kutoka kwenye aina ya uongozi wa Mwendazake, ambako Mungu wa haki mwenye huruma ametuepusha na ili kukwepa kuendeleza kufanya makosa yaleyale dhidi ya binadamu wengine, hata kama itachukua siku zaidi ya hizo mia, nitaendelea kuunga mkono nia yake NJEMA ya kulitibu taifa letu, lililokuwa limekwishaacha mwenendo mwema wa kutoa UHURU NA HAKI kwa watz.
Ninaomba kwa Mungu azidi kuwaongoza wazalendo wa kweli, tusichoke kumuunga mkono kwenye HILI. Na pia tusije Tukakubali KUTAMANISHWA kwa lugha yoyote ile kurudi kwenye ule udhalimu.
AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…