Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Maoni murua ila umeharibu unapotoa shutma pasi ya kutoa ushahidi usio na shaka kuwa Mama 'anategemea zaidi' ushauri kutoka kwa JK!!!, kwanini hutaki apewe ushauri kutoka kwake, ambaye ndiye immediate past president kabla ya Magu?
Kama una bifu na JK hilo ni lako na ufe nalo mwenyewe usiwakanganye wengine kwa kupandikiza fikra potofu.
 
dawa gani tena mambo yanaonekana utelebwe kabisa.

Mama ni binadamu. Kila binadamu ana mapungufu yake kama alivyokuwa mwendazake.

Linganisha wawili hao. Ole, bashiri, chaku, katelefoni bila ya kulisahau genge lile pendwa la kikabia wanayo habari ya dawa unayoiulizia.

Mama? Hakuna cha mtelebwe wala mterembwe. Mambo mdundo.

Wenye nchi tunasubiri ripoti ya CAG BOT na TPA kwa kuanzia.

Watakoma raia wa Sengerema
 
naona tunazidi kuongezeka kwa kasi tuliposema hakuna rais hpo ...mimi siku ya kwanza tu baada ya jiwe kufariki niliamini hatuna rais sema sheria zetu tu ndizo zilizotupelekea kufika hpa tulipo
Kwanza mama ni mvivu sidhani kama ana muda wa kusoma na kufuatilia, sioni tukipiga hatua za maana kutoka hapa tulipo, mimi niligundua kuna udhaifu mahali siku nyingi .
 
Uzi gani sasa akaze? Anahangaika tu na maisha

Waliokaziwa uzi wakisikia swali lako watajua unawacheza shere.

List yao hii hapa: "Ole, bashiri, chaku, nk na kundi lote la vibaraka wao." Kina Malyamungu wenyewe kwenye utawala wa Nduli Amini.

Mama kaweka wazi hataki kodi za dhuluma, anataka maridhiano, anataka ukaguzi wa wazi Jan - March 2021 BOT na TPA, anataka haki, na mengi kama hayo.

Hiyo ndiyo dawa yenyewe yakhe. Dawa hiyo ni chungu mno kwa vibaraka wote wakiwamo wasiojulikana na timu nzima ya lile genge letu pendwa la kikabila.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Mbona sasa ndo anazidi kuharibu, ujambazi umeshamiri kila kona, nchi haieleweki, Mama mwenyewe haeleweki yupo yupo tu kama maiti
 

Ndo nashindwa eti kazi iendelee mxieew, to be honest nchi imeoza hata magufuli hana miez sita kaburini, tuseme yote ila magu alijua kuiweka Tanzania kwenye mstari, nchi ilikua na adabu, wachawi, majambazi wote walikua wanamuogopa, alikua tishia hadi kwa wazungu unadhan huyo ni mtu wa kawaida
 
Mbona sasa ndo anazidi kuharibu, ujambazi umeshamiri kila kona, nchi haieleweki, Mama mwenyewe haeleweki yupo yupo tu kama maiti
CCM ipo madarakani, kumsema mama ni sawa na kuisema CCM kwamba ni dhaifu.
 
Kwa hili ngoja nichangie leo;

Rais Samia anaonekana anasikiliza sana Ushauri wa Kikwete kwakua Kikwete ndiye Rais Mstaafu pakee aliyebakia na mshauri mwenye uzoefu wa nafasi hiyo.

Mzee Mwinyi Kwa umri wake sidhani kama yupo katika hali ya kuweza kumshauri lolote Rais Samia.

Ila Sasa pamoja na hayo inampasa kuchukua ushauri na kuchanganya na maamuzi yake mwenyewe ili huku mtaani iwe vigumu sisi raia kujua hayo maamuzi yake source yake ni wapi.

Ila kwa sasa ni rahisi kutrace the source kwani mambo yanaonekana na Kila mtu.

Ajitahidi sana kurekebisha hilo.

All the best kwake na team yake.
 
Kwanza mama ni mvivu sidhani kama ana muda wa kusoma na kufuatilia, sioni tukipiga hatua za maana kutoka hapa tulipo, mimi niligundua kuna udhaifu mahali siku nyingi .
La kuwa Mvivu nakubaliana nawe 100%.
 
Ok, vizuri ila hao raia wa sengerema imekuwaje?
 
Ni hatari kwa nchi kumruhusu Kikwete kujaza hilo ombwe la uongozi kwani historia yake huko nyuma haikutukuka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…