Tanzania inahitaji Rais kama Hayati Magufuli

Wewe lazima darasa la saba “la zamani”
 


Akili km hizi eti ndio kamati kuu zinatuchagulia Raisi...

Halafu tunajiuliza mchawi wetu wa maendeleo ya kweli ni nani....
 
"Nchi yetu imechezewa sana, sijui hao wanaotuchezea sijui wanatuona sisi ni binadamu au majitu.
"Maisha ya watanzania ya leo ni maisha ya aina gani"
"Watu wanaona nazungumza tu, lakini nataka kuwaeleza kuwa tunazo information zote, tuna mawasiliano yao yote, walipostuka na kubadilisha ilikuwa ' Too Late.'"
 
Hicho usemacho it's relative...dhambi kwako kwangu ni ubinadamu...sijui umenipata?!
Hata Mseveni hatambui makosa yake,hata Lucifer tangu mwanzo wa ulimwengu bado hajatambua makosa yake,hata nduli Amini hakutambua makosa yake,kama umeegemea kwenye makosa huwezi tambua makosa yako.
 

Hatuhitaji viongozi makatili, tunataka katiba mpya itakayopunguza madaraka ya rais, na yeyote ikiwemo rais ashitakiwe akiwa madarakani au ametoka. Hii tabia ya kuwapa watu nguvu kuliko sheria ndio imetufukisha hapa.
 

Vitu kibao vilipanda bei wakati wa Magufuli ikiwemo mafuta ya kula, sukari nk. Na kama ni mgao wa maji hata yeye kiangazi kilipokuwepo mgao wa maji ulikuwa kama kawaida. Au umesahau wakati anasema watu wabadilishane debe la mahindi na ng'ombe watatu? Huu mgao wa umeme ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi za 2020, kila mara umeme ulikuwa unakatika. Hadi leo tatizo limezidi kuwa kubwa. Au kwakuwa nyie mmesahau mnadhani kila mtu kasahau?
 
Tatizo la TZ ni wananchi na wala sio viongozi, Wananchi wanatakiwa waseme wanachotaka katika maendeleo yao sio kutafuta mtu wa kuwaongoza kutafuta maendeleo. Wananchi ndio waseme wanataka nini na wanataka waongozwa vipi. Nguvu ibaki kwa wanachi na sii kwa viongozi madikteta. Bottom line ni katiba ya wananchi, sasa hivi imetekwa na CCM na Rais wao hawataki wananchi watafute Katiba yao. Katiba iliyopo imetengeneza madikteta na kuwa juu ya wananchi na katiba hii haitakaa itengenezwa na serikali hii wala yeyote ijayo chini ya CCM. Tumenzisha vyama vingi kimagumashi, na tumevidhibiti kupitia matamko yanayopingana na katiba na hakuna cha kufanya kwani katiba iliyopo imewaweka juu ya sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…