Sio hapa tunadanganyana eti uzalendo una kuja tu kwa kauli mbiu!!kuwa uzalendo ni kusifia tu kiongozi kwa lolote analofanya hata liwe la hovyo!!Ukraine ndo vivid example ya uzalendo kwa dunia ya leo
Mkuu, mbona unatusononesha wengine?1-Ni ukweli usiopingika kuwa mataifa ya Magharibi yamejiwekea mikakati mahsusi ya kutawala dunia kiuchumi.
Je Tanzania imejipangaje kukabiliana nayo bila kujali uchanga wa Taifa na uchumi mdogo wa Taifa?
ni mikakati gani tuliyonayo ya kujiimarisha dhidi yao?
Kuna mfano wa ka-inchi kamoja ambako sidhani kama kuna mTanzania wa leo anayeweza kutumia kama mfano, kwa sababu ya propaganda nyingi zinazoelekezwa dhidi ya ka-nchi hako.KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
kwanza bajeti ya Wizara ya ulinzi iongezwe mara dufu , tuwe na jeshi lenye silaha za kisasa na mafunzo ya mara kwa mara ....kuwe na umoja wa jeshi la AFRICA kama ....Kuna mfano wa ka-inchi kamoja ambako sidhani kama kuna mTanzania wa leo anayeweza kutumia kama mfano, kwa sababu ya propaganda nyingi zinazoelekezwa dhidi ya ka-nchi hako.
Lakini pamoja na udogo wake, na umaskini wa wananchi wake, na mfumo wa siasa wake, kadri siku zinavyosonga mbele, ka-nchi hako kanazidi kuwa kagumu sana kuvamiwa au kuyumbishwa na haya mapapa ya dunia leo, kwani yanajuwa, yakithubutu kukighusa ka-nchi hako, hawatoki na pua kavu.
Hako ka-nchi ni kadogo zaidi yetu, hakana raslimali kama tulizonazo sisi, isipokuwa labda katika kukosa uongozi unaojali nchi yao. Watu wake hawana elimu za kutisha sana, lakini pamoja na kuwekewa vikwazo vingi vya kiuchumi, ka-nchi hako kanadhidi kujiimarisha kwa kutengeneza makombora yanayoweza kufika nchi yoyote hapa duniani. Sasa kanatengeneza makombora ya "Hypersonic", yanayokwenda mbio zaidi ya mara tatu au zaidi ya sauti. Makombora haya yanaweza kubeba silaha za nuklia na kuyafikisha popote wanapolenga.
Sasa niambie, kama kweli Tanzania hata hatuwezi kutengeneza bunduki zetu sisi wenyewe na risasi za kuwapa wananchi kuilinda nchi hii!
Hiyo sehemu ya kwanza ya mstari ulioandika, ni utashi wetu tu kulitimiza.kwanza bajeti ya Wizara ya ulinzi iongezwe mara dufu , tuwe na jeshi lenye silaha za kisasa na mafunzo ya mara kwa mara ....kuwe na umoja wa jeshi la AFRICA kama ....
Sasa hapo ndiyo wewe unakosea kuleta mambo vyama hapa tunajadili masuala mazito ya mustakabali wa Taifa leta kiuchumi na kiusalama ,Vita ya Ukraine itufundishe kwanza uzalendo.
Hivyo vyote ulivyoandika havitakuwa na matokeo chanya kama tukivamiwa na hatuna uzalendo.
Serikali ielewe kwamba uzalendo haujengwi kwa kutuimbisha Nyimbo, na mahubiri ya majukwaani bali kwa kuwatendea wananchi wote kwa haki, usawa na uaminifu.
Tanzania ikivamiwa Leo na wanaume au vijana wakatakiwa kuingia vitani sidhani kama BAVICHA watakubali, watasema waende hao UVCCM