Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Watawala wa Tanzania walidhani kwa kuua roho ya ujasiri, uthubutu na ubunifu kwa vijana wa Kitanzania kupitia mifumo mibovu ya kielimu, kisiasa na ya kijamii kwamba athari zake zingebaki tu katika mambo ya siasa ili kulinda maslahi ya hao watawala. Badala yake, athari za mambo haya tunaziona zikiwa zimesambaa katika nyanja zote za kijamii hadi za kiuchumi, sanaa na michezo.
Vijana wa Kitanzania wamepoteza na kukosa kabisa uthubutu. Vijana wamepoteza kujiamini. Wamepoteza roho ya kujaribu, kufanya, kuvuruga (ndiyo, kuvuruga pia ni sifa nzuri unapotafuta maendeleo).
Moja ya sifa kuu ya kijana ni kuwa na jeuri ya kufanya mambo, kujaribu, kuwa "disruptor" au mvurugaji. Tunawasifia kina Bill Gates, Zuckerberg na magwiji wengine wa teknolojia zinazobadili dunia kila uchwao ila ukiangalia nyuma yao ni mifumo rafiki inayozalisha vijana wenye roho za uthubutu na "kuvuruga".
Leo viongozi wa serikali ya Tanzania wanatamani kijana aitwaye iShowSpeed aje Tanzania na wapo tayari kumlipa mamilioni ya pesa kutangaza utalii ila ukiangalia kwa undani anachokifanya kijana huyo siyo cha ajabu sana zaidi tu ya kuwa na roho ya uthubutu ambayo vijana wa Kitanzania wamepotezewa. Hawana majibu kwa nini vijana kama hao hawaibuki ndani ya Tanzania.
Ukipita katika hosteli nyingi za vyuo ndani ya Tanzania (hata pale UDSM) utakuta vijana wameanika nguo zao chini katika majani. Hapo hapo hosteli hizo zimezungukwa na miti. Hata fikra na utashi wa kuongeza sehemu za kuanikia nguo zao unakosekana. Hawa ndiyo tunategemea waende kufanya mapinduzi makubwa ya kijamii.
Ukizunguka mijini na vijijini utaona mambo mengi katika jamii yetu yanaendeshwa kwa fikra za kizamani. Tumeamini ndivyo inavyotakiwa kuwa na hakuna njia bora zaidi ya kuyafanya hayo. Matokeo yake ni jamii kudumaa. Tunabaki kuwalaumu vijana kwa ulegevu, uvivu na kutochangamkia fursa huku tunasahau tumewajenga hivyo na haya ni matunda yake.