Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

Tetesi zlizopo ni kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha na kampuni za nje lakini fedha hizi zimefanywa siri bila kuingizwa katika kasri za serikali, na hivyo kuwa nje ya wigo wa ukaguzi wa serikali kutia na CAG. Hili ndilo simulizi lililopo.

Nitawawapa dondoo za mazungumzo yaliyofanyika.

"Asikudanganye mtu, suala la Tanzania kununua ndege kwa fedha za kodi na pia kujenga Stiegler na SGR, daraja la Salenda na hizo flyover na mabarabara na miradi mikubwa inayofanyika, sio kwamba ni fedha za kodi. Tanzania haina ubavu huo wa fedha za kodi kufanya miradi mikubwa kama hiyo. Mnadanganywa. Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha ambayo zimefanywa siri, na uongozi wa nchi kutumia fedha hizo kama mtaji wa kisiasa".

Lakini je, fedha hizo zinatoka wapi, na kwa nini Tanzania ilipwe? Simulizi linaendelea.

"Fedha hizo ni fedha za Helium ya Tanzania. Katika nchi ambazo zimebarikiwa rasilimali asili Tanzania labda inaongoza. Kuanzia miaka ya 2010 dunia ilionekana kwamba inaishiwa gesi ya Helium ambayo imekuwa ikitengenezwa viwandani na kuuzwa kwa bei kubwa"

"Kuna nchi sita tu duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, na viwanda 14 duniani. Karibu nusu ya hii gesi inatoka USA. na theruthi moja inatoka Qatar. Sasa viwanda vyote hivi 14 vilivyopo duniani, vinazalisha Helium kutokana na natural gas. Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo Helium imepetikana ardhini kwa wingi sana na ndio maana sasa iko katika nafasi ya kuongoza soko la Helium duniani".

"Hii gesi inapopatikana ardhini inakuwa na concentration ya wastani wa 2% na hivyo kufanya bei yake kuwa juu sana kwa kuchimba, na ndio maana inazalishwa viwandani. Sasa jambo moja la ajabu lilitokea. Mwaka 2015 wataalamu waligundua hii gesi Tanzania ikiwa inapatikana kwa kiwango cha juu sana, kati ya 5-15%. Hii ilifanya Tanzania kuwa nchi pekee ambayo ina Helium ardhini ambayo inaweza kuchimbwa na kuzalishwa kwa gharama ya chini kuliko inavyozalishwa na viwanda hivi 14 katika nchi 6 duniani. Na matokeo ni kwamba Tanzania ikajikuta katika nafasi ya kuongeongoza soko la Helium duniani, kama ambavyo Saudi Arabia inaongoza soko la mafuta duniani."

"Kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa Helium. Kufuatia upungufu wa hii gesi, Marekani hata walianza kuweka hifadhi kubwa ya gesi hii kwa ajili ya matumizi ya baadae. Upungufu wa hii gesi umefanya bei yake uongezeka kwa zaidi ya asilimia 135% kwa mwaka mmoja tu!"

"Hii gesi ya Helium ni muhimu sana na itaipaisha Tanzania kiuchumi kuliko hata kama ingekuwa na mafuta. Matumizi ya hii gesi ni pamoja na kwenye mambo kama welding na hata utaalamu wa space (kwa kiingereza uses of Helium gas: are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, space travel, etc)"

"Lakini sasa kukawa na tatizo. Ikiwa Tanzania ingeruhusiwa kuchimba hii Helium na kuuza, basi ingeuza kwa bei poa kiasi kwamba ingeua kabisa uzalishaji wa hivi viwanda 14, USA akiwa mzalishaji mkubwa. Basi inaonekana kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzania icheleweshe uzalishaji wa Helium hadi wakati unaokubalika. Lakini kwa kufanya hivyo, lazima kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzaia ilipwe fedha nyingi kama "compensation" ya kuzuia uzalishaji wa Helium ili kunusuru kampuni zinazouza Helium kwa sasa. Hiyo ndiyo fedha inayofanya miradi yenu ambayo wanasiasa wenu wanawaambia eti ni kodi za wananchi ili kuji-promote kisiasa. Habari ya ugunduzi wa Heluim Tanzania na umuhimu wa hii gesi katika soko la dunia, ilipaswa kuwa kubwa kuliko kama Tanzania ingegundua mafuta. Sasa jiulize, kwa nini wanasiasa wenu wamekaa kimya kuhusu huu ugunduzi mkubwa uliofanyika Tanzania? Tanzania ni nchi pekee duniani unapata Helium ardhini na utatawala soko la dunia kama ilivyo kwa Tanzanite, na mnakaa kimya, kwa nini?"

Reference: In Photos: Massive Underground Helium Reserve Found in Tanzania

Taarifa ya Bloomberg Businessweek juu ya Helium ya Tanzania
2019-08-28

Helium is produced on Earth by the natural radioactive decay of uranium and thorium, which are present in all rocks. But that process takes a long time—as in billions of years—so you’d need some seriously old stones. And because such old rocks don’t have a lot of gas-trapping formations, you’d need some geologic activity to break them apart and form fractures through which the helium could escape. Then you’d need heat to push the helium up through the fractures, and sedimentary formation at the surface to store it in traps between the layers of sediment, as in a reservoir.

Ballentine and colleague Diveena Danabalan identified Tanzania as one place with this kind of interplay at work. Ancient rocks formed in the African tectonic plate about 2 billion years ago, making them sufficiently old for radioactive decay to produce a lot of helium. Thirty million years ago, the plate began to pull apart, forming the Great Rift Valley, which reaches 1,700 miles from southern Tanzania up to Eritrea and the Red Sea. That process created fractures that allow magma to escape; the magma would provide the heat necessary to force the helium upward. Meanwhile, at the surface, sediments were deposited, providing the reservoirs where helium could be found. “That combination of factors makes possible helium accumulation at the surface,” says Emmanuel Kazimoto, a geology lecturer at the University of Dar es Salaam.

Among the key uses for helium today are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, and space travel. The Large Hadron Collider, the particle accelerator outside Geneva wrestling with the biggest questions of physics, needs 120 metric tons of helium a week to keep running. Helium can make things superconductive, meaning they can transmit electricity basically forever without generating any heat, and other helium properties make the element essential for semiconductor manufacturing. Every MRI machine in the world bathes its magnetic coils in liquid helium to prevent overheating.

Like the price of lithium, the price of helium is one of the more opaque among commodities, but reports said it jumped 135% from the previous year. With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania.
Kwa kuwa ni Tetesi, ngoja tusikilizie tu hizi Tetesi kama ulivyosema na kuandika

Tetesi, basi sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipenda Sana taarifahii, nitafurahi zaidi Kama malipo yatakuwa yawazi nakupangiwa bajeti na bunge

Mara umeisha ukubali huo uzushi billa kufanya utafiti zaidi na kujiridhisha?
Je kama hela hiyo wange iweka kwenye account za nje bila kutengeneza hizo miundo mbinu!
Hueleweki Mkuu. Kuweka hela nje kivipi?
 
Dah!! Eti aingii kwenye kasri sijui hazina

Lakini zinajenga bwawa la maji, salender, SGR, kununua Ndege, je kuna ubaya gani hapo?

Tunachoshana kwa siasa za maji taka, nilifikiri wamehifadhi kwenye akaunti zao binafsi kumbe zinajenga miundo mbinu na vitu vingine vya kimaendeleo.
 
Ukubali au ukatae wewe ni kilaza kama walivyo vilaza wengine hapo mtaani kwenu

Sasa kama hizo pesa wameshindwa kuzilipia madeni au kuongezea mishahara kw a kumuhofia CAG Kichere halafu wakazitumie kujengea reli na kununulia ndege
Unajionyesha upumbavu wako. Ikiwa fedha hii inalipiwa nje kwenye account ambayo Tanzania imetengeneza say Uswiss, na serikali inaitumia kulipa kampuni ya nje inayojenga SGR, au Boeing kununua ndege, au kampuni ya nje kujenga Stiegler nk, nani atajua kwa kuwa hizo transaction zinafanyika huko nje? Kwani unafikiri kampuni za nje zinazokuja kufanya kazi hapa zinalipwa shilingi toka Benki kuu, au watauliza hizi hele tulizolipwa mbona chanzo chake sio Tanzania? Je Boeing watauliza mbona mmelipia ndege kutoka account ya Uswiss?

Sasa njoo upande wa pili. Ili utumie hiyo hela kulipa mshahara, huelewi kwamba itabidi uiingize kwenye account za serikali? Sasa utaonyesha imetoka wapi au ni mapato ya nini? CAG lazima ajue kila hela ya serikali iliingia kutoka wapi na kwenda wapi ili atengeneze balance. Utaeleza hii hela ilitokana na nini? Hebu basi fuatilia hela tuliyolipa Boeing ilitoka wapi na account ipi ya serikali, kwa nini haikupitishwa Bungeni nk, haafu njoo uongee hapa. Fuatilia hela ya kulipia SGR inalipwa toka account gani, je inajadiliwa bungeni nk

Na labda uanze kujiuliza kwa nini pale Wizara ya Fedha kuna mtu wa karibu na mkulu, au kwa nini mtu kama Prof Ndulu ilibidi aondoke na South Africa wakamdaka akawasaidie kama mshauri wa Ramaphosa.

Unajifanya unajua kumbe kilaza wahed.
 
Dah!! Eti aingii kwenye kasri sijui hazina

Lakini zinajenga bwawa la maji, salender, SGR, kununua Ndege, je kuna ubaya gani hapo?

Tunachoshana kwa siasa za maji taka, nilifikiri wamehifadhi kwenye akaunti zao binafsi kumbe zinajenga miundo mbinu na vitu vingine vya kimaendeleo.
Kwa hiyo wakilipwa Bilioni 2, wakatumia bilioni 1 kujenga miundo mbinu na ile moja ikapotezewa ni sawa tu? Na kama ni kweli, kwa nini tusiwe wazi na kusema jamani tunalipwa hizi fedha na sababu ni hizi? Anyway, ni tetesi.
 
Inawezekana ni kweli.
Wikipedia wameelezea mradi wa sgr na chanzo cha pesa yake.
Link ya wikipedia
 
Attachments

  • IMG_20200122_152847.jpg
    IMG_20200122_152847.jpg
    35.7 KB · Views: 2
  • IMG_20200122_152933.jpg
    IMG_20200122_152933.jpg
    36.5 KB · Views: 3
Tujitoe tu ufahamu, tuanze kuchimba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndilo jambo kuu. Lakini Marekani wataturuhusu kuuza ikiwa tukiuza tunaua biashara yao?

Nasikia Tanzania inataka kuwekewa vizuizi. Usikute ndio mambo hayahaya. Tumewajia juu wakasema watatutengeneza.

Angalia hapa report ya Bloomeberg kuhusu hii Helium;

"Helium One expects to be producing helium from Tanzania by the end of 2020, a few months before the world's main supplier, the U.S. government, ceases to supply the gas from the Federal Helium Reserve in Texas"

Hiyo statement hapo juu ina mambo makubwa sana ambayo yanafanya hii tetesi iwe na uzito!
 
Inawezekana ni kweli.
Wikipedia wameelezea mradi wa sgr na chanzo cha pesa yake.

Kinachonifanya niwe na wsiwasi ni kwamba, kwa nini hii miradi mikubwa Tanzania matumizi yake ya fedha hayajadiliwi na kupitishwa na Bunge, na inatekelezwa kama miradi binafsi ya mtu mmoja ambaye anajua wapi atapata fedha kwa ajili ya hiyo miradi?

Ulisikia Bunge limejadili na kupitisha bajeti ya kununua Dreamliner? Lakini unaambiwa ni kodi zetu. Hebu tuonyenywe fedha za kununulia Dreamliners zilitoka wapi. Je kwenye report ya CAG zimo? Mie sijui.
 
Ndio munavoongepeana hapo kwenye viwanja vya Lumumba,mbona deni la taifa linakua kwa speed ya umeme,miaka minne mtu amekopa 50/% ya waliokaa miaka 40........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wakilipwa Bilioni 2, wakatumia bilioni 1 kujenga miundo mbinu na ile moja ikapotezewa ni sawa tu? Na kama ni kweli, kwa nini tusiwe wazi na kusema jamani tunalipwa hizi fedha na sababu ni hizi? Anyway, ni tetesi.
Unajua kiasi wanacholipwa mkuu?
 
Ngoja kwanza.
Kwa hyo unataka kusema tumedanganywa.
Na ule wimbo wa juhudi za awamu ya tano.
Kumbe ni gesi ya helium?.
Si angesema tu ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachonifanya niwe na wsiwasi ni kwamba, kwa nini hii miradi mikubwa Tanzania matumizi yake ya fedha hayajadiliwi na kupitishwa na Bunge, na inatekelezwa kama miradi binafsi ya mtu mmoja ambaye anajua wapi atapata fedha kwa ajili ya hiyo miradi?

Ulisikia Bunge limejadili na kupitisha bajeti ya kununua Dreamliner? Lakini unaambiwa ni kodi zetu. Hebu tuonyenywe fedha za kununulia Dreamliners zilitoka wapi. Je kwenye report ya CAG zimo? Mie sijui.
Mikopo ya siri haihojiwi.
Wikipedia wameandika kabisa sgr ni mkopo wa standard chartered na export credit bank ya uturuki.
Labda wikipedia wahojiwe wametoa wapi hiyo taarifa.
 
Unajionyesha upumbavu wako. Ikiwa fedha hii inalipiwa nje kwenye account ambayo Tanzania imetengeneza say Uswiss, na serikali inaitumia kulipa kampuni ya nje inayojenga SGR, au Boeing kununua ndege, au kampuni ya nje kujenga Stiegler nk, nani atajua kwa kuwa hizo transaction zinafanyika huko nje? Kwani unafikiri kampuni za nje zinazokuja kufanya kazi hapa zinalipwa shilingi toka Benki kuu, au watauliza hizi hele tulizolipwa mbona chanzo chake sio Tanzania? Je Boeing watauliza mbona mmelipia ndege kutoka account ya Uswiss?

Sasa njoo upande wa pili. Ili utumie hiyo hela kulipa mshahara, huelewi kwamba itabidi uiingize kwenye account za serikali? Sasa utaonyesha imetoka wapi au ni mapato ya nini? CAG lazima ajue kila hela ya serikali iliingia kutoka wapi na kwenda wapi ili atengeneze balance. Utaeleza hii hela ilitokana na nini? Hebu basi fuatilia hela tuliyolipa Boeing ilitoka wapi na account ipi ya serikali, kwa nini haikupitishwa Bungeni nk, haafu njoo uongee hapa. Fuatilia hela ya kulipia SGR inalipwa toka account gani, je inajadiliwa bungeni nk

Na labda uanze kujiuliza kwa nini pale Wizara ya Fedha kuna mtu wa karibu na mkulu, au kwa nini mtu kama Prof Ndulu ilibidi aondoke na South Africa wakamdaka akawasaidie kama mshauri wa Ramaphosa.

Unajifanya unajua kumbe kilaza wahed.
Nahisi na wewe unatoka katika kabila la wachunga ngombe na wapanda punda
 
Unajua kiasi wanacholipwa mkuu?
Hapana Mkuu. Ila nawashangaa hawa wanaosema kama tulanlipwa na fedha zinatumika kujenga miundo mbinu basi sio tatizo. Suala ni kwamba, kama kweli tunalipwa, hizo fedha zinatumika zote kwa miundo mbinu? Na kwa nini zifanywe siri na kuishia huko huko nje?

Hata hivyo, labda haya ni mambo ya kawaida. Katika mambo ya uzalishaji mafuta, kuna kitu kinaitwa "signature bonus" ambayo huwa haiandikwi kwenye mkataba ni kiasi gani kinalipwa. Sasa serikali nyingi za Afrika huwa zinaamua zitakavyoitumia bila kuiingiza kwenye mifumo ya fedha za serikali. Mara nyingine inafunguliwa akounti ya nje. Na hiki ndicho chanzo cha maraisi wa nchi zenye mafuta, kama Abacha wa Nigeria, kujitajirisha sana.

Inawezekana Tanzania imefanya kitu kama hiki, kama ni kweli tunalipwa.
 
Mikopo ya siri haihojiwi.
Wikipedia wameandika kabisa sgr ni mkopo wa standard chartered na export credit bank ya uturuki.
Labda wikipedia wahojiwe wametoa wapi hiyo taarifa.
Dreamliners, Airbus na bombardiers sio mikopo mkuu - cash!
 
Back
Top Bottom