Hivi ile Tanzania ya Viwanda ilifia wapi?
Kuna jamaa ameweka kontena pale barabarani, mbele kidogo ya mlandizi kaliandika TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA, cha ajabu miaka 3 sasa sioni chochote kikifanyika kwenye yale makontena/godauni.
Tukirudi kwenye mada, nakubaliana na mtoa mada, tuuze processed cornflower, sio raw corn/maizes.
Tuwe na viwanda vidogo vidogo vya kusaga na kukoboa mahindi na kuuza unga wake. Hii pia itafanya faida kubwa kwani kutakua na thamani imeongezeka pale.
Huu ndio ubaya wa Tanzania, hakuna kitu utafanya uwe na uhakika nacho kwa 100% sustainability yake kwa miaka 5 mfululizo. Kila kitu ni cha kubahatisha. Ukilima leo huna uhakika wa soko la mazao yako, huna ni kama kucheza kamari, upate ama ukose.
Unaweza kulima leo ukavuna vizuri, kesho serikali ikapiga marufuku kusafirisha mazao nje ya nchi, ama kesho serikali ikakupangia bei ya kuuza. Unalima leo kesho soko na nje likafa kama ilivyo leo kwa Kenya.
Ukija kwenye biashara nyingine, TRA, Osha, Halmashauri, Ushuru, fine, TFDA, TBS, Bwana afya, mtendaji kata, serikali ya mtaa, sijui ujinga gani vyote vinaangalia kukamua kibiashara chako.
Kwa Tanzania kuanzisha clean business ukatoboa ni ngumu sana, usipokwepa kodi, kufanya ujanja ujanja hutoki.
Tunaishi maisha ya kubahatisha miaka 60 ya utawala wa CCM.