Tanzania inatakiwa iuze unga wa mahindi nje ya nchi, ni muda muafaka Sasa kulisimamia hilo tusililie kupeleka mahindi Kenya

Tanzania inatakiwa iuze unga wa mahindi nje ya nchi, ni muda muafaka Sasa kulisimamia hilo tusililie kupeleka mahindi Kenya

Masterplaner

Senior Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
121
Reaction score
184
Kuhusu mahindi yetu kuwa Yana sumu au hayana sumu, mamlaka husika zihakiki ubora huo kwenye viwanda maalum vya kusaga mahindi yetu vitakavyo kuwa vimeidhinishwa angalau kila mkoa. Vilevile madawa yenye sumu yadhibitiwe yasiweze kumfikia mkulima ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wakulima wetu namna ya Bora ya kuyakinga mazao yetu na sumu tukianzia shambani, ukweli ni kwamba baadhi ya mahindi yetu ni kweli yanatia wasiwasi, mahindi yanasagwa lakini bado harufu ya madawa haitoki kwenye unga, ili litazamwe kwa kweli.
 
Tutafute wanaokula ugali kama sisi twende nao ng'adu kwa ng'adu.
 
Mimi ni msukuma ila sijui kuka pwani huku kumenibadili sana naweza kaa hata mwezi ugali sijagusa maana napenda sana ndizi, ubwabwa na vitu vya ngano kama chapati, tambi na maandazi na nk kwa hiyo kumbe nimeepuka sana.
 
Hivi ile Tanzania ya Viwanda ilifia wapi?
Kuna jamaa ameweka kontena pale barabarani, mbele kidogo ya mlandizi kaliandika TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA, cha ajabu miaka 3 sasa sioni chochote kikifanyika kwenye yale makontena/godauni.

Tukirudi kwenye mada, nakubaliana na mtoa mada, tuuze processed cornflower, sio raw corn/maizes.

Tuwe na viwanda vidogo vidogo vya kusaga na kukoboa mahindi na kuuza unga wake. Hii pia itafanya faida kubwa kwani kutakua na thamani imeongezeka pale.

Huu ndio ubaya wa Tanzania, hakuna kitu utafanya uwe na uhakika nacho kwa 100% sustainability yake kwa miaka 5 mfululizo. Kila kitu ni cha kubahatisha. Ukilima leo huna uhakika wa soko la mazao yako, huna ni kama kucheza kamari, upate ama ukose.

Unaweza kulima leo ukavuna vizuri, kesho serikali ikapiga marufuku kusafirisha mazao nje ya nchi, ama kesho serikali ikakupangia bei ya kuuza. Unalima leo kesho soko na nje likafa kama ilivyo leo kwa Kenya.

Ukija kwenye biashara nyingine, TRA, Osha, Halmashauri, Ushuru, fine, TFDA, TBS, Bwana afya, mtendaji kata, serikali ya mtaa, sijui ujinga gani vyote vinaangalia kukamua kibiashara chako.

Kwa Tanzania kuanzisha clean business ukatoboa ni ngumu sana, usipokwepa kodi, kufanya ujanja ujanja hutoki.

Tunaishi maisha ya kubahatisha miaka 60 ya utawala wa CCM.
 
Umenikumbusha " Kilimo kwanza" enzi ya JK.
Enzi za Nyerere kulikua na Gapex pia vyama vya ushirika ambavyo vilinunua mazao ya mkulima. Sasa hivi tunahimizwa tulime wakati wa mavuno hakuna mnunuzi wa mbaazi, nyanya uzauza ndoo sh 200/=
 
Aisee suala la viwanda Nchi hii ni kizungumkuti......nchi nyingi zinazoendelea unaona viwanda vikiboreshwa na kuwekewa mazingira mazuri huku vingine vikianzishwa.
Hapa kwetu tukihesabiana vilivyokufa na vinavyoendelea kufa. Ukiangalia na vinavyoenezishwa na kutafakari juu ya ukuaji wa viwanda unaweza ukipata ajibu mwenyewe.

Kila nikipita Kawe hususani Tanganyika packers na kuangalia yale majengo na nia a Serikali ilivyokuwa wakati wanayaanzisha. Nikisikia sauti ya watu wakikanyaga mafuta mule najisikia kizunguzungu sana.
Nambatanisha picha a Tanganyika packers kipindi cha Awamu ya kwanza.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    27.8 KB · Views: 3
  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    9.3 KB · Views: 3
Enzi za Nyerere kulikua na Gapex pia vyama vya ushirika ambavyo vilinunua mazao ya mkulima. Sasa hivi tunahimizwa tulime wakati wa mavuno hakuna mnunuzi wa mbaazi, nyanya uzauza ndoo sh 200/=
Kilimo ambacho ndiyo sababu ya uchumi wa viwanda vingi Duniani leo kinapapaswa tu.....hivi yale matrekta a kilimo kwanza yaliishia api tena?.
Tukutane pale Suma JKT kuangalia.
 
Enzi za Nyerere kulikua na Gapex pia vyama vya ushirika ambavyo vilinunua mazao ya mkulima. Sasa hivi tunahimizwa tulime wakati wa mavuno hakuna mnunuzi wa mbaazi, nyanya uzauza ndoo sh 200/=
Viazi, mihogo, ndizi , miwa, kunde, havina bei
 
Soko la mahindi tulizembea hapo katikati mpaka sasa hivi Zambia nao wamekua wazalishaji wakubwa kupitia wale wazungu waliotimuliwa Zimbabwe sasa hivi DRC wanategemea mahindi kutoka Zambia na wanapeleka Malawi kupitia Chipata huko tena hizo Nchi ni wavivu unaenda unga kabisa wangetoa Kodi kwenye mashine za kukoboa ndogo na kubwa na pia kupata vibali vya nembo ingekua rahisi na haraka hakuna sehemu unga hautakiwi ni vile tunatengenezeana mazingira magumu hayo maroli ya kubeba unga au mahindi Kodi ipo juu sijui huwa mnafikiria nini punguzeni Kodi kwenye baadhi ya vitu mtapata pesa baada ya kuuza mazao kwa wakati.
 
Back
Top Bottom