Tanzania inazidi kudidimia katika soko la Viwanda vya Uzalishaji, China, Ulaya & Marekani wakigombea umwinyi wa Afrika

Tanzania inazidi kudidimia katika soko la Viwanda vya Uzalishaji, China, Ulaya & Marekani wakigombea umwinyi wa Afrika

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Zamani tulishuhudia Afrika ikiwa kwenye Makwapa ya mataifa ya Ulaya na Amerika Leo China imeongeza kwapa lake .

Tanzania na Afrika imejisalimisha Rasmi na imekubali nguvu zake za uchumi ikabidhi kwa Wachina,

YeboYebo na makobazi yanayouzwa kama njugu barabarani hayatengenezwi Dar es Salaam yanatoka China na kama wapo Dar kuanzia Teknolojia ni mali ya mchina.

Tanzania inayojisifu kuwa na vyuo vikuu,maprofesa na madaktari wa kutosha Haina uwezo wa kutengeneza makobazi ya kuendea chooni.Hii ni ajabu

Wachina wanaizunguka Afrika na mpango wao wa BRICS huku wamarekani wapo Kusini wakianzia Angola na mpango wao wa Lobito.

Kifupi twafaaaaaaa.
Kwenye nadharia za maendeleo wapo wasomi Wanasema ili Afrika isonge mbele inatakiwa kukata kabisa Kamba ya mashirikiano na mataifa haya,

bahati mbaya wengi Afrika wamewekwa mfukoni na hawana uwezo hata wa kupumua

Afrika imegeuka kuwa soko la bidhaa kutoka China huku ikiwa imebarikiwa utajiri wa kutupwa.

Bandari ya Dar es Salaam imesheheni makontena ya bidhaa hususani nguo kutoka China huku mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa na ardhi na hali ya hewa inayoruhusu uzalishaji wa Pamba na viwanda vya nguo vyote vimekufa.

Wachina sasa hawaleti nguo pekee,sasa wanakuja wenyewe kuuza nguo na kuwachezesha Watanzania Kamari.

Wachina wapo Kuanzia Kariakoo mpaka Kigoma wanachezesha Kamari na kuuza bidhaa kama nguo na vifaa vya kielekloniki.

Wamejaa Kanda ya Ziwa wanachimba madini mpaka sehemu ambazo walistahili wachimbaji wadogo wadogo.

Wachina wanauza nguo kama machinga wa Makoroboi,Karume na Kariakoo.

Wewe mtanzania huwezi kufanya haya Beijing.

Watanzania wanachezesha Kamari, Wachina wanafurika kuja masokoni na kuanza kuuza nguo, wanakujua suala la mavazi ni moja ya mahitaji ya msingi ya binadamu. Wamatuzamisha Mazima

Itaeendelea jioni

 
Watu wanajibebea tu malighafi wanapeleka kwao
Sema ndy hivyo sisi tumewekeza kwenye kukata mauno kwa sana

Ova
 
Kwa sisi ambao tumebobea kwenye masuala ya Historia ya Afrika kabla, wakati, na baada ya ukoloni; hata hatushangai kuona haya yanayoendelea kutokea kwenye Bara lote la Afrika, na Tanzania ikiwemo!!

Huu ni Ukoloni Mamboleo uliochangamka kweli kweli!! Yaani viongozi wetu na wenyewe sijui wako usingizini! I wish Mama angenitafuta ili niwe mshauri wake maalum kwenye haya masuala ya kupambana dhidi ya hila za Mabeberu!!
 
Back
Top Bottom