Tanzania - India Relations: Hakuna msaada wowote tunaweza kuwapa rafiki zetu wa India? Hata kama ni salamu za pole pekee zinatosha sana

Tanzania - India Relations: Hakuna msaada wowote tunaweza kuwapa rafiki zetu wa India? Hata kama ni salamu za pole pekee zinatosha sana

Kwa wakati huu kusingepaswa kuwe Kuna nchi inapitia pito gumu la corona Kama ilivyokua mwanzoni mwa kuanza kwa ugonjwa wenyewe.

Kwa sababu elimu inatokiwa kupewa watu wameshapewa Sana, tagadhari zinazotakiwa kuchukuliwa kuukwepa ugonjwa huu zinajulikana wazi na zaidi ya yote chanjo zipo na zinasadikika kufanya kazi.

Sasa sijajua huko India Ni wapi wamekosea, yote ya yote Mungu awape wepesi .
Je, hujui kwamba huyo kirusi wa mwanzo sio sawa na virusi wa sasa???
 
Je, hujui kwamba huyo kirusi wa mwanzo sio sawa na virusi wa sasa???
Mkuu, halafu hii ndio inayonichanganya sana mpaka ninahisi labda kuna watu wanafanya huu mchezo wa kubadilisha virusi.
 
Afu hivi kwanini lugha ya kihindi haizunguzwi na wazawa kama zilivokuwa lugha nyengine? Kwanini watanzania wanaokijua kihindi ni wachache ukilinganisha na kichina, kiarabu, kingereza, kiitaliano, kihispania nk shida nini sisi wazawa hatutaki kujifunza au wao hawataki kutufundisha
India wana malugha mengi hata sijui lugha yao ya taifa ni ipi wale watu, ni nchi ya nne dunia kuwa na karibia lugha zaidi ya 400 ndani ya taifa moja
 
India wana malugha mengi hata sijui lugha yao ya taifa ni ipi wale watu, ni nchi ya nne dunia kuwa na karibia lugha zaidi ya 400 ndani ya taifa moja
Daaah, lugha 400 ndani ya nchi moja mzee baba?
 
Je, hujui kwamba huyo kirusi wa mwanzo sio sawa na virusi wa sasa???
Ndo kusema chanjo kwa sasa sio msaada kabisa? Maana kuna new variants wa virus kila uchao.
 
Mkuu, halafu hii ndio inayonichanganya sana mpaka ninahisi labda kuna watu wanafanya huu mchezo wa kubadilisha virusi.
Kwa kawaida kirusi huwa na tabia ya kujibadilisha umbile la kijenetiki "antigenic drift" na "antigenic shift"
 
Embu acha kuchekesha

Msaada ? Wakati tunaamini corona haipo/ mchezo wa mabeberu/ hila msaada wowote wa maana hatuwezi kutoa hata ushauri ni bora tubaki tu kimyaa
Mambo mengine ni kuacha yapite kama walivyosema wahenga kuiga kunywa kwa tembo.... Sio kuona usa na ulaya wakifanya yao na sisi tufanye
 
Ila kusema kweli kirusi cha India na Africa viko tofauti,, sijajua mazingira yanatubeba au chanjo tulizopewa wakati tupo wadogo,,, kama hali hiyo ingeikumba Tanzania au baadhi ya nchi za Africa wangebaki wachache hasa wale wanaoishi vijijini!!!!!
 
Daaah, lugha 400 ndani ya nchi moja mzee baba?
Lugha kubwa ni Hindu, ukiacha hiyo wana lugha 22 rasmi "official" ambazo zinazungumzwa kulingana na majimbo yao yale...

Lakini kwa ujumla sasa wana aina tofauti zaidi ya 400, kuna wakati nilikuwa nafuatilia historia ya waafrika walio nje ya Afrika, nikaja kukutana na documentaries za Waafrika waliotoka kwetu East Africa, waliokimbilia sehemu kubwa ya kaskazini magharibi mwa India ambapo hao wahindi ni weusi tiii na kuna baadhi ya traces za Kiswahili katika lugha zao...

India has the world's fourth highest number of languages (447), after Nigeria (524), Indonesia (710) and Papua New Guinea (840)
 
Ndo kusema chanjo kwa sasa sio msaada kabisa? Maana kuna new variants wa virus kila uchao.

Bado ni msaada kwa sababu haujui ni wakati gani utakutana na kirusi gani
 
Embu acha kuchekesha

Msaada ? Wakati tunaamini corona haipo/ mchezo wa mabeberu/ hila msaada wowote wa maana hatuwezi kutoa hata ushauri ni bora tubaki tu kimyaa
Hata kutuma salamu ya pole tu hatuwezi?
 
Mambo mengine ni kuacha yapite kama walivyosema wahenga kuiga kunywa kwa tembo.... Sio kuona usa na ulaya wakifanya yao na sisi tufanye
Mbona msiba wa mume wa malkia Elizabeth hatukuacha tu upite na dunia nzima ilimlilia? Rais alituma salamu kwa niaba ya watanzania wote.
 
kwani india walishawahi kutupatia msaada gani aisee, yaani mhindi akupe msaada. hata ubalozi wao hapa kwetu mimi huwa sioni umuhimu wao, hao hawana faida kama walivyo mataifa mengine ya africa tu.
 
Mbona msiba wa mume wa malkia Elizabeth hatukuacha tu upite na dunia nzima ilimlilia? Rais alituma salamu kwa niaba ya watanzania wote.
Ule msiba upo tofauti na haya yanayojiri india, kwa ule msiba mtu mmoja pole tu ilikuwa yatosha kuonyesha mshikamano.
Lakini kwa haya yanayoendelea india ukituma pole utakuwa kituko katika medani za kidiplomasia. Ili uende sambamba yabidi utume vifaa vya kusaidia juhudi maana bado mapambano yanaendelea na watu wanaendelea kufa. Angalia jinsi misri ilivyojitutumua kipindi marekani kabanwa koo na korona kwa kutuma ppe angali yeye ni taifa dogo sana compare na Marekani kadhalika na urusi, china watu wa nchi hizi walilalamika but ilikuwa big win in diplomatic relation kwa hizi nchi

Ila fresh kama kutuma pole itabidi uwekwe utaratibu kutuma pole kila wiki coz kutakuwa kuna marehemu wengine wamezalishwa na covid
 
Back
Top Bottom