Tanzania insists EAC citizens MUST use passports to enter Tanzania

Tanzania insists EAC citizens MUST use passports to enter Tanzania

Haha, mikutamo mutatu ya kwanza yote Tanzania haikuona mualiko wala salamu. Mkiulizwa mnasema Oh, haya ni maswala ya nchi tatu huru, wakati nyuma yenu kuna bendera ya EAC. Mawaziri watanzania walianza kuja baada ya Museveni kuomba suluhu. Lakini hata hivyo na mpaka leo hii, yote yaliyoongelewa mnashidwa kutueleza faida iliyopatikana.

Kudakuliwa vitambulisho sio sifa kusema turuhusu mkenya yoyote aigie kwetu eti dunia nzima nyaraka zao zinadakuliwa. Miaka ya karibuni udakuzi wa hati za kusafiria umeshuka sana kutokana na usalama wa hizo hati na taarifa zake kuwekwa kwenye mitandao ya kidunia. Sasa kwanini tusitake kutumia nyaraka iliyokuwa na uhakika kuliko vitambulisho vinavyoweza kutengenezwa na wajanja wa River Road.

Hilo la mialiko kwa Tanzania silijui, ninalolijua ni kwamba Tanzania ilituzungusha kwenye mbuyu hadi maamuzi ya kuendelea kwenye tri-lateral arrangement ambayo yanaruhusiwa kwenye sheria za EAC yakaafikiwa. Tanzania ikaomba itajiunga baadaye, japo ikaishia kulia lia.

Hakuna mtu amesema kudakuliwa kwa vitambulisho ni sifa, nilichokisema ni kwamba mumejificha nyuma ya vijisababu vya kila aina na kuendelea kuweka vizingiti na vizuio, halafu mnalia kwamba mnatengwa. Watu wanaghushi hata paspoti, hivyo sio kwamba pasport ndio foolproof. Kwanza ukiangalia kwenye Global Passport Power Rank, ya Kenya ina hadhi hata zaidi ya Tanzania Global Passport Power Rank | Passport Index 2017
 
Hivyo ina maana kila developer kwenu ana passport? Sio kila mtu huwa amekaa mkao wa kutoka nchini kwao. Hata kule USA utakuta kuna madeveloper hawajawaza kutoka hiyo USA unayoishobokea.

Binafsi kwa maisha yangu yote sikua nawaza kutoka nje ya nchi yetu, ila siku moja ghafla offer ikanikuta ya kutakiwa niende Hongkong ili kuhuduhuria mafunzo ya mfumo fulani wa teknolojia walitaka kuuanzisha EAC. Tatizo sikua na paspoti, wakati wenyewe walikua wanalipia kila kitu, usafiri na malazi na mambo mengi, nilikua bado kijana kijana hivi, hivyo niliishia kuwaona wenzangu wakivuka kwa KQ hadi ikaniuma. Baadaye nilifuata pasport, hivyo sio kila mtu hukaa mkao wa kutoka kwenye nchi yao.

Na pia developers wengi wanabadilishana mawazo hapa EAC na usije ukashangaa kuna wale wanaalikana ili wasaidiane kwenye mambo fulani fulani. Kuwekea watu vizuizi ni jambo ovyo sana.
Sasa mtafute passport, EAC ni jina tu.
 
Sasa mtafute passport, EAC ni jina tu.

EAC ni jina kwa baadhi yenu mliofungiwa huko kitaa Dar, lakini kawaulize Watanzania waliojitambua na kutoka, wanaofanya biashara na kunufaika ndani ya EAC, watakushangaa kwamba hujui nini maana ya EAC.
 
Hilo la mialiko kwa Tanzania silijui, ninalolijua ni kwamba Tanzania ilituzungusha kwenye mbuyu hadi maamuzi ya kuendelea kwenye tri-lateral arrangement ambayo yanaruhusiwa kwenye sheria za EAC yakaafikiwa. Tanzania ikaomba itajiunga baadaye, japo ikaishia kulia lia.

Hakuna mtu amesema kudakuliwa kwa vitambulisho ni sifa, nilichokisema ni kwamba mumejificha nyuma ya vijisababu vya kila aina na kuendelea kuweka vizingiti na vizuio, halafu mnalia kwamba mnatengwa. Watu wanaghushi hata paspoti, hivyo sio kwamba pasport ndio foolproof. Kwanza ukiangalia kwenye Global Passport Power Rank, ya Kenya ina hadhi hata zaidi ya Tanzania Global Passport Power Rank | Passport Index 2017

Kwahiyo hakuna hata siku moja Uganda au Rwanda walikataa mnayowamezesha midomoni ila unaona ni Tanzania tu ndio inawachelewesha wakenya. Hebu tuabie Kenya ilchukiwa muda gani kukubali sarafu moja ya EAC. Muda mwingine mnajisahau kuwa EAC sio shamba la Kenya.

Sasa kama unajisifia passport yenu ina ngivu kuliko ya Tanzania (kitu cha kuchekesha kwasababu usalama wa karatasi haumaanishi ni nchi ngapi unakubaliwa kuingia). Kwanini watu wenu wanapata shida ya kuzipata na kujanazo Tanzania?
 
Why are we trying to convince these people on something everyone knows. Easy movement of people, more business, more revenue. As a kenyan if I want to visit any of the EAC countries, I am now more likely to go to either Ug or Rwanda, vice versa... It is a reality. I will visit these 2 countries and tz wont even be in my plan. All that hustle...
TZ utakuja tu upende usipende. Huku kutamu asikuambie mtu. Wakenya wapo huku wamegoma kurudi kwao. Waulize.
 
EAC ni jina kwa baadhi yenu mliofungiwa huko kitaa Dar, lakini kawaulize Watanzania waliojitambua na kutoka, wanaofanya biashara na kunufaika ndani ya EAC, watakushangaa kwamba hujui nini maana ya EAC.
EAC kitu gani wakati tuna jumuiya nyingine ya SADC. Serikali yetu imeamua kwamba muwe na passport ndio mruhusiwe kuingia kama hamtaki muwe mnatembeleana wenyewe wakenya, waganda na wanyarwanda, Tanzania ni passport kwanza.
 
Kwahiyo hakuna hata siku moja Uganda au Rwanda walikataa mnayowamezesha midomoni ila unaona ni Tanzania tu ndio inawachelewesha wakenya. Hebu tuabie Kenya ilchukiwa muda gani kukubali sarafu moja ya EAC. Muda mwingine mnajisahau kuwa EAC sio shamba la Kenya.

Sasa kama unajisifia passport yenu ina ngivu kuliko ya Tanzania (kitu cha kuchekesha kwasababu usalama wa karatasi haumaanishi ni nchi ngapi unakubaliwa kuingia). Kwanini watu wenu wanapata shida ya kuzipata na kujanazo Tanzania?

Kitu moja naona umeshindwa kujifunza ni kwamba nchi zote za EAC ni mataifa huru na hakuna hata moja nayoweza kulazimishiwa cochote, hivy Uganda na Rwanda wana haki na uwezo wa kutupia mbali chochote kisichoendana na maslahi yao kama mataifa huru, ila tofauti yao na nyie ni kwamba, wao wanakataa wasichokipenda bila kulia lia.

Paspoti zetu zina nguvu na ni mojwawapo wa mahitaji ya sisi kuingia Tanzania kulingana na sheria za kwenu, sasa sielewei swali lako hilo lina umuhimu gani au linamaanisha nini.
 
EAC kitu gani wakati tuna jumuiya nyingine ya SADC. Serikali yetu imeamua kwamba muwe na passport ndio mruhusiwe kuingia kama hamtaki muwe mnatembeleana wenyewe wakenya, waganda na wanyarwanda, Tanzania ni passport kwanza.

Kwa mtu anayejua kupiga mahesabu mapana hawezi kuongea unavyoongea, labda utakua wale wabongo wazamiaji wa kule Afrika Kusini kubeba mabox. Lakini kwa Watanzania wanaojitambua, wanatumia SADC/EAC kutanua kibiashara.
 
Nakumbuka yule jamaa anaitwa Mwanzi1 akilia lia eti Uhuru ameitenga Tanzania wakati habari kama hizi ndio zinadhihirisha Tanzania yenyewe inavyojitenga na kuwa na double standard kwa majirani. Eti wanafunzi wa Rwanda wanalipa karo moja na wale wa Tanzania ilhali wa Uganda wanalipa zaidi.

Leo hii Mnyarwanda akitaka kuasfiri kuja Kenya au Mkenya kwenda Rwanda, ilmradi anayo kitambulisho cha taifa lake hana haja ya kuhangaika na passpoti.

Hivi majuzi tumekua na tukio la ovyo sana hapo Bongo, kuna shughuli fulani ya kikazi iliyokwama ghafla na ilihitaji mtaalam fulani kutokea Kenya aje kuifanyia kazi. Tatizo jamaa alikua na matatizo na paspoti yake, ikawa hawezi kuingia Tanzania maana hata akipewa temporary passport Kenya lakini kule Tanzania hawampi business permit au CTR.

Hivi lile bomba la mafuta linalopigiwa kelele humu kila siku halikuwaunganisha Waganda na WaTz?
 
Kaka kwenye ulimwengu wa utalaam kuna mengi, nikupe tu mfano, hapa Kenya kuna software unakuta imetengenezwa na Mkenya na kuuzwa Kenya na EAC yote. Sasa upate mteja labda ni Sacoo fulani hivi Tanzania ana maboresho fulani anayotaka ifanywe na ili kumwelewa vizuri, inabidi developer mwenyewe asafiri na kwenda kukaa na mteja moja kwa moja ili kuelewa uhalisia wa hayo mahitaji na kuyafanyia kazi.

Sasa hapo unakuta developer yupo radhi kuibeba laptop yake aende kwa mteja kumslikiliza huko Tanzania, lakini tatizo linakua pale hajafuata pasipoti au ina matatizo, basi inabidi kuendelea kuelekezana kwa simu na barua pepe. Sio kwamba hakuna developers Tanzania, wapo na wana software zao, lakini mteja ambaye ni Mtanzania amechagua software iliyotengezwa na Mkenya na labda ameitumia kwa muda hadi akakumbana na uhitaji wa maboresho zaidi/customization. Sasa mnakwama nyote.

Mambo kama haya hutokea mara nyingi sana, lakini yakitokea Uganda au Rwanda, inakua mwendo wa raha maana developer atachukua laptop yake na kitambulisho chake na kuruka kwa KQ, anakwenda kuishi na mteja kama wiki moja au mbili huku shughuli ikieleweka na jioni anajiachia jiachia kwa raha zake maeneo maeneo ya burudani, shughuli ikishaeleweka anageuza na kurudi Nairobi.
After sale service of program ndo mtu atoke Kenya aje bongo. Why don't s/he use team viewer window. Mimi mara nyingi huwa nikikwama ninapotumia specialised programme such idris, arcgis from ESRI nawasiliana na staff wao kwa njia hii.
 
Kwamba Tanzania bado imechelewa kwenye kuwapa raia wake vitambulisho, sisi hatuna tatizo nalo na ndio maana mkaomba mkae pembeni mjiandae, mtafakari mfanye yote ili muwe tayari baadaye. Tatizo ni pale mnaanza kulia kwamba mumetengwa ilhali wenyewe ndiye hao baada ya kutuzungusha kwenye mbuyu baadaye mkaomba mkae pembeni kwa baadhi ya mambo.

Kuhusu ufisadi wa kuwa na vitambulisho ni tatizo linalokumba hata mataifa makubwa, hilo sio la kutupigia makelele na vijisababu vyenu visivyoisha, nakumbuka siku fulani hata waziri wenu Mwigulu Nchemba aliwahi kusema mwenyewe kawaona Wachina wana hadi vitambulisho vya kupigia kura. Sasa hadi upate cha kura lazima uwe na cha kitaifa, hebu tafakari.

Acha uongo.
Lini wapi nani raia wa china kuwa na kitambulisho cha kupiga kura.
 
Kitu moja naona umeshindwa kujifunza ni kwamba nchi zote za EAC ni mataifa huru na hakuna hata moja nayoweza kulazimishiwa cochote, hivy Uganda na Rwanda wana haki na uwezo wa kutupia mbali chochote kisichoendana na maslahi yao kama mataifa huru, ila tofauti yao na nyie ni kwamba, wao wanakataa wasichokipenda bila kulia lia.

Paspoti zetu zina nguvu na ni mojwawapo wa mahitaji ya sisi kuingia Tanzania kulingana na sheria za kwenu, sasa sielewei swali lako hilo lina umuhimu gani au linamaanisha nini.

Ili uelewe swali la pasipoti, rudi nyuma usome ulicho kiandika mwenyewe kuhusu matumizi ya vitambulisho kati ya wananchi wa Kenya na Rwanda. Unapenda kuandika mambo kiujanja ujanja, lakini unajikanyaga mwenyewe na kuumbuka. Mara unalalamika wakenya wanashindwa kuchangamkia kazi Tanzania kwasababu Tanzania wanataka pasipoti, huku unasema wakenya hawana shinda ya kupata pasipoti wanapozihitaji. Sasa tatizo liko wapi, kwanini wakenya wanalia wakiambia hawaingii Tanzania bila pasipoti?
 
Kwamba Tanzania bado imechelewa kwenye kuwapa raia wake vitambulisho, sisi hatuna tatizo nalo na ndio maana mkaomba mkae pembeni mjiandae, mtafakari mfanye yote ili muwe tayari baadaye. Tatizo ni pale mnaanza kulia kwamba mumetengwa ilhali wenyewe ndiye hao baada ya kutuzungusha kwenye mbuyu baadaye mkaomba mkae pembeni kwa baadhi ya mambo.

Kuhusu ufisadi wa kuwa na vitambulisho ni tatizo linalokumba hata mataifa makubwa, hilo sio la kutupigia makelele na vijisababu vyenu visivyoisha, nakumbuka siku fulani hata waziri wenu Mwigulu Nchemba aliwahi kusema mwenyewe kawaona Wachina wana hadi vitambulisho vya kupigia kura. Sasa hadi upate cha kura lazima uwe na cha kitaifa, hebu tafakari.

Hivi ulishawahi kuskia Tanzania ikilia kwamba imetengwa kwenye CoW?sisi huwa hatujali maamuzi yenu kwa kuwa tunajua hamuwezi kufanikisha lolote bila ya sisi,kidiplomasia sisi ndio baba wa east,central and south Africa.hapa kwenye hili bandiko wanaolia ni Waganda,wakenya na wanyarwanda,sisi watanzania tunachojua ni kwamba tunahitaji passport kusafiri kuingia nchi nyingine na tumeridhika na hilo.
 
After sale service of program ndo mtu atoke Kenya aje bongo. Why don't s/he use team viewer window. Mimi mara nyingi huwa nikikwama ninapotumia specialised programme such idris, arcgis from ESRI.

Kaka unapohusiana na wateja Waswahili jiandae kwa lolote, kuna mteja vyote hivyo havisaidii, Skype, Teamviewer, Amy wala nini. Unawatuma watu kwake lakini inaishia lazima usafiri na kukaa naye, na kumskliza mkiwa naye kwenye mazingira yake na yupo radhi kulipia hayo yote.
Labda wewe umezoea ku-support off the shelve systems, lakini kama mwenyewe unatengeneza system from scratch, pale unamskliza mteja kuanzia mwanzo hadi mnaagana, Teamviewer na hivyo vidubwash vingine havisaidii chochote.
 
Acha uongo.
Lini wapi nani raia wa china kuwa na kitambulisho cha kupiga kura.

Kaka kuwa mfuatiliaji wa matukio ya nchi yako, wacha hulka za kukurupuka.
------------------------------------------------------
Wakuu leo nikiwa kwenye Ofisi za DHL kufuatilia mzigo wangu, waliingia Wachina Kuja kuchukua Mzigo wao ambao umetumwa kutoka Huko kwao, na inaonekana hawana adress ya makazi so waliagiza kupitia ofisi ya DHL, sasa wakati anasaini ili wachukue Mzigo waliombwa vitambulisho, mimi nikajua hapo watatoa Pasport, Ila cha kushangaza walitoa Kadi za Kupigia Kura za Tanzania, kwa kweli nilichoka make wanaongea Kingereza kwa shida inaonekana wanajua tu kichina.

Ilibidi niunganishe na ile ishu niliyosoma kwamba Uraia Tanzania unatolewa kama Karanga, na sidhani kama kuna nchi ambayo ni rahisi sana kwa mgeni kupata Uraia kama Tanzania.
Kauli ya Waziri Mwigulu: Wachina "kuomba uraia"

eliakeem
 
Ili uelewe swali la pasipoti, rudi nyuma usome ulicho kiandika mwenyewe kuhusu matumizi ya vitambulisho kati ya wananchi wa Kenya na Rwanda. Unapenda kuandika mambo kiujanja ujanja, lakini unajikanyaga mwenyewe na kuumbuka. Mara unalalamika wakenya wanashindwa kuchangamkia kazi Tanzania kwasababu Tanzania wanataka pasipoti, huku unasema wakenya hawana shinda ya kupata pasipoti wanapozihitaji. Sasa tatizo liko wapi, kwanini wakenya wanalia wakiambia hawaingii Tanzania bila pasipoti?

Hebu nionyeshe wapi nimetaja kwamba Wakenya hawapati shida wakati wa kufuata paspoti, unafaa ufahamu paspoti yetu ina hadhi sana na hupati kiulaini kama karanga barabarani. Wapo wanaoghushi na kufanya yao lakini wakikamatwa huwa ngoma.
 
Back
Top Bottom