Halafu suala la ujenzi wa miundombinu linategemeana na mahitaji, na vilevile future ambayo imekuwa envisoned. Na wala siyo suala la kushindana, kwa maana kama unasema Nairobi ina Flyover (interchanges) 50 na Dar inazo 2, hiyo ni kutokana na mahitaji.
Huwezi kushindana kwenye miundombinu maana inaendelea kujengwa, Kwa mfano ukiangalia miundombinu ya Washington DC miaka ya 70 na 80 ilikuwa more superior ukilinganisha na Beijing. Lakini leo miundombinu ya Beijing kuanzia Airport mpaka Public Transit ni more superior kuliko ile ya Washngton DC.
Sawasawa na sisi, Nairobi imeanza kujenga interchanges muda mrefu, Mfano Waiyaki way ina madaraja mengi kuondoa uwezekano wa magari kukutana, unaweza kuendesha kuanzia Limuru mpaka Westlands pasipo kusimama, na hii barabara ni ya muda mrefu. At the same time Dar haikuwepo. In short kwa wakati huo haikuwa priority.
Kwenye public transportation, Dar ina better public transit kuliko Nairobi (hata ukiiondoa BRT), Mfumo wetu wa Daladala ni bora kuliko zile Matatu za Nairobi, na hiyo ndo maana pia wakazi wengi wa Nairobi wana magari binafsi au wanatembea kwa miguu maana usafiri wa umma si mzuri sana.
Kwenye planning, miundombinu yote ya Dar kwa sasa inajengwa kwa ku-consider Public Transport (hasa BRT), hata hizi interchange chache zinazojengwa (TAZARA wameacha njia pale katikati kwa ajili ya mabasi), Ubungo Interchange itakuwa na lanes za BRT, Barabara ya Bagamoyo (Moroco-Mwenge) na sasa hivi BRT Mbagala.
Nairobi sidhani kama mnafikiria suala ya mass transit katika miundombinu yenu. Otherwise msingepaka rangi Thika Highway.
Future ya cities sio flyovers bali ni public transit.