Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Hawaelewei jinsi gani mavazi ya binadamu yanavyoingia katika jamii na kusamba.
Sijui ni elimu yetu imeporomoka kiasi cha kuzalisha watu wenye akili hizi au ni ushamba ulioganda watu kama ruba.
Ni kama unafunga uhuru wa maoni. Na maoni yangu ni halina maana na haliwezi fanikiwa abadani maana vazi halitafutwi. Ni auto tu, ninyi mnadhan Nigeria walitaguta vazi lao, au Rwanda?
 
Hawaelewei jinsi gani mavazi ya binadamu yanavyoingia katika jamii na kusamba.
Sijui ni elimu yetu imeporomoka kiasi cha kuzalisha watu wenye akili hizi au ni ushamba ulioganda watu kama ruba.
Punguza ushamba kijana
 
Mambo ya vazi la taifa ni ushamba wa kiwango cha juu.
Hamuelewei ni jinsi gani mavazi yanakuwa maarufu na kupendwa na watu hadi yanavaliwa na kila mtu bila hata kuamuliwa na vikao?
Sasa ndio umeandika nini?
 
Mambo ya vazi la taifa ni ushamba wa kiwango cha juu.
Hamuelewei ni jinsi gani mavazi yanakuwa maarufu na kupendwa na watu hadi yanavaliwa na kila mtu bila hata kuamuliwa na vikao?
Mkuu, kama vazi la taifa ni ushamba kwa maoni yako sawa ila kwa maoni yangu mimi na wengine huo sio ushamba hata kidogo.
 
Mambo vp jamiiforums.

Ninashauri sana nchi yetu ya Tanzania isiwe na vazi moja tu la taifa. Tuwe na mavazi rasmi matano (5) kutoka katika makabila yetu yatakayorasimishwa na kupewa hadhi ya utaifa. Yaaani kama inawezekana mpangilio uwe hivi au hata kama kura ya maoni inaweza kupigwa itakuwa sawa tu.

Picha hapo chini ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne mzee Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamependeza vizuri kabisa katika mavazi ya kabila ya Waha (baba) pamoja na Maasai (Mama)
=====
View attachment 1718602

(1) Kaskazini - Vazi la kimaasai (Mkoa Arusha)

(2) Kusini - Vazi la Kimakonde (Mkoa Mtwara)

(3) Mashariki - Vazi la Kisambaa (Mkoa Tanga)

(4) Magharibi - Vazi la Waha (Mkoa Kigoma)

(5) Kanda ya kati - Vazi la wagogo (Mkoa Dodoma)

Nchini Afrika ya kusini wamefanya hili kwa upande wa lugha rasmi za taifa, ila sisi tunaweza kufanya hivi hivi kwa upande wa vazi rasmi la taifa.

Kwa uhalisia tu ni kwamba, huko nchini Afrika ya Kusini kuna makabila mengi sana yaliyopo katika majimbo tofauti tofauti na matokeo yake lugha zinatawala katika majimbo yao husika ambayo inafanya kuwa lugha mahususi haswa kwa eneo/mkoa husika.

Takribani lugha thelathini na tano (35) zenye asili ya Afrika Kusini huzungumzwa katika nchi hiyo, kumi kati ya hizo ni lugha rasmi za taifa la Afrika Kusini: Ndebele, Pedi, Sotho, Swati, Tsonga, Tswana, Venda, Xhosa, Zulu na Afrikaans.

Lugha rasmi ya kumi na moja ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha ya msingi inayotumiwa katika mazungumzo ya kibunge na kiserikali, ingawa lugha zote rasmi zina uzito sawa katika hadhi ya kisheria na katika ya nchi hiyo.

Kama katika lugha 35 kutoka nchi nzima waliweza kuchagua lugha 11 tu kutambulika kama "official languages" na Tanzania yenye makabila takribani 120 pia inaweza kuchagua mavazi kutoka makabila 5 tu kuwa ndio mavazi rasmi ya taifa ili tumalizane na hili suala kwa maana tangia lianze kujadiliwa ni zaidi ya miaka 15 sasa na bado sijaona solution ya maana mpaka sasa.

Zamani ilikuwa ni Dar es Salaam kwa kabila la wazaramo ila sasa ni Dodoma kwa wagogo ndipo kumepewa hadhi ya makao makuu ya nchi na serikali. Kama mkoa wa Dodoma umeweza kupewa hadhi hiyo na kuacha mikoa mingine, kwanini makabila matano niliyoyaorodhesha hapo juu yasiwakilishe mavazi rasmi ya taifa?

Soma pia>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Vazi linapaswa li emerge kutokana na tamaduni za watu husika siyo watu kubebeshwa mavazi wasiyoyajua. Ulipaswa kufanya utafiti wako vizuri kabla ya kuja na mada kama hizi. Najaribu kuwaza uwaambie wazee wa kichaga (na walivyo jeuri) wakavae mashuka ya kimasai yanayowafanya watembee makalio yakiwa wazi, hili haliwezekani.
 
Back
Top Bottom