#COVID19 Tanzania Itafute Mbinu Bora ya Kupambana na COVID19

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Tusije kuweka matumaini makubwa kwenye chanjo halafu tukabakia tunaombea ifanye kazi tofauti na inavyofanya kazi kwenye nchi nyingine. Hapa Marekani jana CDC imetutangazia kuwa hata sisi tuliopata chanjo tayari tuanze kurudi kuvaa mabarakoa tukiingia sehemu mbalimbali. Kuna hofu hapa kuwa namba za wanaoambukizwa zinazidi kupanda na mahospitali wagonjwa wanaanza kujaa (wengi ni wale waliogoma kuchanja!).

Lakini hofu nyingine ni kuwa hii aina ya kirusi cha COVID19 cha Delta kinazingua sana na kirusi cha Lambda nacho kiko njiani na hawajui ni kwa kiasi gani vitaendelea kugeuka geuka - kuna hofu kama kitafikia kirusi cha Omega itakuwaje!

Njia salama zaidi ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 70 ya watu kwenye jamiii inapata chanjo hivyo itapunguza na kutengeneza kinga ya kijamii (community immunity/herd immunity). Kimsingi watu wengi wakichanjwa wanawalinda wasiochanjwa! Lakini kama namba hii haijafikiwa au haitafikiwa basi hali inayoendelea Marekani na baadhi ya nchi itawakuta Tanzania na wale waliochanjwa nao watajikuta matatani tena.

Tusifikirie na tusije kuwaaminisha Watanzania kuwa chanjo inawazuia kupata virusi; haiwazuii! Na kutegemeana na chanjo zenyewe mnaweza kujikuta mko square one. Chanjo hii ya Jenssen ya Johnson & Johnson inawazingua hapa Marekani na kuna taarifa watu waliochanjwa hiyo tayari wanaanza kutafuta chanjo nyingine za kuongezea.

Kimsingi ni kuwa huu ugonjwa bado haujapatiwa majibu ya uhakika na kudhania chanjo peke yake itaudhibiti labda ni kujipa matumaini makubwa mno. Chanjo hii si kinga kama tulivyozoea chanjo nyingine. HII SI CHANJO ya kukuzuia kupata virusi. Hizi chanjo zinadhibiti virusi visilete madhara kwa mtu zaidi - hivyo mtu anaweza bado akapata kirusi cha corona lakini asiumwe kabisa au akaumwa kidogo.

Lakini pia tunajua hata watu waliochanjwa kabisa wanaumwa bado na wengine wanaumwa vikali (serious illness) hasa kama kuna mambo mengine ya kiafya.
Lakini ninachoogopa zaidi - ni kuwa labda hofu ambayo tunaitengeneza kwenye jamii itaumiza zaidi kuliko watu wanavyofikiria. Ni lazima tufikirie tofauti siyo tu vile tunaambiwa. Hawa wakubwa wenyewe hawajapata suluhisho tusitegemee kofia yao kututosha. Tuchanganye na za kwetu. Miye mwenyewe pamoja na kuwa nimechanjwa toka mwezi Machi navaa barakoa nikitoka home...

Ukishachanjwa, changanja na za kwako...usiende kujiachia tu... hadi hiki kirusikitupite.

Lakini sijui chanjo milioni moja kwa watu karibu milioni 30 ambao wanahitaji bado ni kiasi kidogo sana kuweza kuwa na matokeo yoyote ya maana.

Maoni yangu.
 
Kwahiyo tuende na wazo la Mbowe chanjo iwe ni lazima ili walau tuweze ku-achieve hiyo herd community?

Vinginevyo hili bandiko lako linazidi kuongeza utata kwani ni wazi hakuna cha kushika(no suluhisho)
Chanjo iwe lazima huku kuna dozi million moja na watu wako million 59+ hiyo chanjo ya kuchanja wote itatoka wapi?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lipo wapi wakati maisha magumu kasema chanjo ni hiari ya mtu.
 
Kamati yetu yenyewe imeshindwa kutoa If nchi hii ipo kwenye "Natural Herd Immunity". Wao wamemeza kuhusu chanjo. Sweden wamefanya both chanjo+natural herd immunity and the last time I checked they had zero covid deaths for 10days running
 
Kwahiyo tuende na wazo la Mbowe chanjo iwe ni lazima ili walau tuweze ku-achieve hiyo herd community?

Vinginevyo hili bandiko lako linazidi kuongeza utata kwani ni wazi hakuna cha kushika(no suluhisho)

Ukichanja wewe na mbowe wako inatosha.

Huyu mbowe pamoja na ukoo wake walitangazia umma kuwa wamechanjwa lakini mbona kila siku wanatangaza kutembelewa na huyu Corona.

It's very challenging to get definitive vaccine for a virus which mutates in several form within a short period of time.

That virus seems to have no proof reading mechanism in its genome
 
Ukichanja wewe na mbowe wako inatosha.
Huyu mbowe pamoja na ukoo wake walitangazia umma kuwa wamechanjwa lakini mbona kila siku wanatangaza kutembelewa na huyu Corona...
Ukisikia Jina la Mbowe unapagawa na kuvurugukiwa mpaka unashindwa kuelewa maana ya swali kulingana na mada iliyotolewa!!
 
Nimeona Marekani wanasema hata watu walio chanja fulk doze waanze kuvaa barakoa na ku keep distance.

Sasa maana ya hii chanjo hata sijaona
 
Ukisikia Jina la Mbowe unapagawa na kuvurugukiwa mpaka unashindwa kuelewa maana ya swali kulingana na mada iliyotolewa!!
Samahani Mama kwa kumtaja mmeo kwenye mchango wangu wa thread ya Mzee Mwanakijiji.

Una wivu uliovyo kubuhu we nyumbu wa ufipa aisee
 
Kwahiyo tuende na wazo la Mbowe chanjo iwe ni lazima ili walau tuweze ku-achieve hiyo herd community?

Hili bandiko lako linazidi kuthibitisha kuwa mpaka saaa hakuna suluhisho na dunia haijui ifanye nini hasa katika kukabiliana na huu ugonjwa.
Magufuli alisema haya muda mrefu tu
 
Nina wasiwasi wanaochanja ndio wanaosambaza sasa. Hili tatizo limetengenezwa na hao hao wanatupa suluhisho.

Huko dunia ya kwanza wamechanja lakini hali ndio inazidi kuwa mbaya! Kama chanjo ni kinga kwanini kuvaa barakoa?

JPM alisimama na suluhisho ambalo sasa dunia ndio inafata. Tunaweza kuumiza kichwa tuje na solutions zetu. Ndio hatutengenezi hata tooth pick lakini tuanzie mahali. Dunia inapigwa tusiingie kichwa kichwa na kuwafuata wazungu kikondoo.
 
1. Ukipata chanjo unaweza kupata corona? = Ndiyo[emoji3581]

2. Ukipata chanjo unaweza pia kufa kwa corona? = Ndiyo [emoji3581]

SWALI:
Kwanini upate chanjo?
 
Ukichanja wewe na mbowe wako inatosha.
Huyu mbowe pamoja na ukoo wake walitangazia umma kuwa wamechanjwa lakini mbona kila siku wanatangaza kutembelewa na huyu Corona...
Lete hilo bandiko lake aliposema ukoo wa Mbowe umechanja
 
Kwahiyo tuende na wazo la Mbowe chanjo iwe ni lazima ili walau tuweze ku-achieve hiyo herd community?

Hili bandiko lako linazidi kuthibitisha kuwa mpaka saaa hakuna suluhisho na dunia haijui ifanye nini hasa katika kukabiliana na huu ugonjwa.
Ni vigumu kuifanya lazima wakati huna uwezo wa kutengeneza hata dozi moja. Unaona mtego?
 
It's just the matter of Time before this thing - vaccination becomes mandatory
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…