Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Tusije kuweka matumaini makubwa kwenye chanjo halafu tukabakia tunaombea ifanye kazi tofauti na inavyofanya kazi kwenye nchi nyingine. Hapa Marekani jana CDC imetutangazia kuwa hata sisi tuliopata chanjo tayari tuanze kurudi kuvaa mabarakoa tukiingia sehemu mbalimbali. Kuna hofu hapa kuwa namba za wanaoambukizwa zinazidi kupanda na mahospitali wagonjwa wanaanza kujaa (wengi ni wale waliogoma kuchanja!).
Lakini hofu nyingine ni kuwa hii aina ya kirusi cha COVID19 cha Delta kinazingua sana na kirusi cha Lambda nacho kiko njiani na hawajui ni kwa kiasi gani vitaendelea kugeuka geuka - kuna hofu kama kitafikia kirusi cha Omega itakuwaje!
Njia salama zaidi ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 70 ya watu kwenye jamiii inapata chanjo hivyo itapunguza na kutengeneza kinga ya kijamii (community immunity/herd immunity). Kimsingi watu wengi wakichanjwa wanawalinda wasiochanjwa! Lakini kama namba hii haijafikiwa au haitafikiwa basi hali inayoendelea Marekani na baadhi ya nchi itawakuta Tanzania na wale waliochanjwa nao watajikuta matatani tena.
Tusifikirie na tusije kuwaaminisha Watanzania kuwa chanjo inawazuia kupata virusi; haiwazuii! Na kutegemeana na chanjo zenyewe mnaweza kujikuta mko square one. Chanjo hii ya Jenssen ya Johnson & Johnson inawazingua hapa Marekani na kuna taarifa watu waliochanjwa hiyo tayari wanaanza kutafuta chanjo nyingine za kuongezea.
Kimsingi ni kuwa huu ugonjwa bado haujapatiwa majibu ya uhakika na kudhania chanjo peke yake itaudhibiti labda ni kujipa matumaini makubwa mno. Chanjo hii si kinga kama tulivyozoea chanjo nyingine. HII SI CHANJO ya kukuzuia kupata virusi. Hizi chanjo zinadhibiti virusi visilete madhara kwa mtu zaidi - hivyo mtu anaweza bado akapata kirusi cha corona lakini asiumwe kabisa au akaumwa kidogo.
Lakini pia tunajua hata watu waliochanjwa kabisa wanaumwa bado na wengine wanaumwa vikali (serious illness) hasa kama kuna mambo mengine ya kiafya.
Lakini ninachoogopa zaidi - ni kuwa labda hofu ambayo tunaitengeneza kwenye jamii itaumiza zaidi kuliko watu wanavyofikiria. Ni lazima tufikirie tofauti siyo tu vile tunaambiwa. Hawa wakubwa wenyewe hawajapata suluhisho tusitegemee kofia yao kututosha. Tuchanganye na za kwetu. Miye mwenyewe pamoja na kuwa nimechanjwa toka mwezi Machi navaa barakoa nikitoka home...
Ukishachanjwa, changanja na za kwako...usiende kujiachia tu... hadi hiki kirusikitupite.
Lakini sijui chanjo milioni moja kwa watu karibu milioni 30 ambao wanahitaji bado ni kiasi kidogo sana kuweza kuwa na matokeo yoyote ya maana.
Maoni yangu.