Tanzania itahitaji miaka zaidi ya elfu moja au zaidi kupata mageuzi ya kweli

Turudi kwa Mungu sasa kumuuliza tulipo ni sawa au si sawa?
Hali hii kwa jicho la kiimani..pitia taarifa hii ya kihistoria kisha pima uhalisia na kilichofanyika wakati huo, lbd itasaidia kuona kosa lilifanyika wapi kiimani na lirekebishwe vipi..

"Wengi wetu tumebahatika aidha kushiriki au hata kuchangia mbio za Mwenge wa uhuru wa Tanganyia (Tanzania), lakini ni wangapi kati yetu tunajuwa asili haswa ya huo Mwenge!?
Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima. Wapo wanaodhani kwamba aliyeleta mabadiliko katika nchi kwa kuanzishwa kwa mwenge huo ni Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere lakini kiukweli haswa Mwalimu Nyerere si mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru.
Mnajimu maarufu ambaye sasa ni marehemu, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema na ikaandikwa kwamba mvumbuzi wa wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.
Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Sheikh Yahya Hussein (1925).
Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima (alifunga), jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.
Sheikh Yahya Hussein alinukuliwa akisema hata hivyo, katika mashimo yale Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya shimo kwa ajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wenzake nje wakimngoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es Salaam.
Utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema, zindiko la Bagamoyo linafanya kazi.
Kilichoshangaza, alisema ni mtu huyo kuingia shimoni na kukaa siku kumi na siku ya kumi na moja alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa, na alikuwa akiongea lugha hisiyojulikana.
"Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho," alisema Sheikh Yahya.
Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere:
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau."
Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)," alisema Sheikh Yahya.
Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo "UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI" akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.
Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:
"Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38," na ndivyo ilivyokuwa.
Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38 =115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.
Je, tambiko hili ndio matokeo ya udumavu kifikra na kimaamuzi kwa watanzania? TAFAKARI.
 
Sio unabii au utabiri bali ni hitimisho ambalo nimekuja nalo baada ya kupitia mambo mbali mbali katika hii nchi.

Habari za wakati huu wasomaji wa JF ndani na nje ya mipaka ya taifa hili.

Hii nchi ina watu na vitu vya kushangaza sana.Nianze ni hii;hali ya sintofahamu inayohusu mvua kubwa zinazotarajiwa.Mamlaka ya hali ya hewa zimetoa tahadhari juu ya mvua kubwa.Kinachonishangaza ni kwamba baada ya hii tahadhari watu ndio wamepata muamko wa kufanya usafi.

Nimeona baadhi ya mamlaka za miji zikikumbuka kwamba kuna mitaro ilishaziba toka enzi na enzi inazibuliwa sasa.Swali langu ni kwamba kama isingekuwa hiyo tahadhari hii mitaro ingebaki michafu sio? na vipi tunajipanga na hizo mvua kubwa,what if,kukatokea ukame na mvua zikaenda kwingine tutabadili mipango yetu tena?(ndio maana nikahitimisha kwamba safari yetu ya mageuzi itatuchukua muda mrefu)

Jambo jingine la ajabu tena ni hili hapa.Kiongozi wa upinzani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ndugu Tundulissu mpaka sasa yapata mwaka na miezi ya kutosha anashikiliwa(makosa yake sitaki kusema ni ya kweli au ya uongo,fuatilia mwenendo wa kesi utajua) lakini sija ona mwamko wa watu katika hili jambo kutoa msukumo kwa mamlaka husika kutenda haki kwa kiongozi huyu.Swali langu ni kwamba CHADEMA haina wafuasi loyal au haina ushawishi katika hili taifa kufikia kiongozi mkubwa hivi anafanyiwa dhuluma ambayo inaonekana wazi?(ndio maana hitimisho langu likasukumwa na hoja kama hizi)

Mwisho kabisa,Suala la msanii Dudu baya(jina lake halisi sijalitafuta).Nimeshangazwa sana na kitendo cha BASATA kumfungia pamoja na kumtoza faini.Sitaki kuamini kwamba kauli mbiu yake ya kupinga ushoga ina shida sana kama kweli tunaka kujenga jamii imara na kusimamia maadili.Naweza nisikubaliane nae juu ya kushambulia baadhi ya watu lakini kauli mbiu yake ilikuwa na nia ya kukumbusha watu kusimama katika misingi imara hasa kwa malezi ya mtoto wa kiume.

Ni hayo tu kwa leo lakini ikiwa tunahitaji kujenga taifa imara inabidi tuamke.Muda tulio lala umetosha.
CCM sio chama cha siasa tena, ni genge la kihalifu kama magenge mengine ya kihalifu (mafia,sinaloa,yakuza).

Chama cha siasa kinatakiwa kufanya siasa kama ambavyo CHADEMA wanavyofanya, lakini CCM kwa kuwa si chama cha siasa, ukihoji chochote kinyume na matakwa yao, unapotezwa mchana kweupe.

Polepole na Nchimbi ni mfano hai wa jinsi CCM ilivyogeuka kuwa genge la kihalifu kwa mgongo wa chama cha siasa.

Ni mwanaCCM yupi amejitokeza kuulizia kuhusu uwepo wa hawa waliokuwa viongozi waandamizi wa chama na serikali!!??

Kwenye mchakato wa "uchafuzi"wa kumpata mgombea wa genge la CCM, nfdugu Malisa alihoji kuhusu mchakato kuvurugwa, kilichompata sote tu mashahidi wa kilichomtokea.

Katiba mpya ndio mwarobaini wa kumaliza huu upuuzi unaofanywa na genge la kihalifu la CCM.
 
Sasa katiba mpya itapatikani vipi ikiwa tayari umeona CCM tena sio chama cha siasa bali kundi la wahalifu kiongozi?

Ndio maana nikasema kuamka ni muhimu.CCM hawezi kukupa katiba huku anajua ikifanyika hivyo anapoteza mamlaka na nguvu zote alizokuwa nazo sasa.Sahau hili la CCM kukupa katiba mpya
 
Mtanzania wa kawaida akiandika uzi mtandaoni wa kumsifia Lissu au akishatoa ile michango ya Tonetone anaamini amemaliza jukumu.

Funzo kwa viongozi wa upinzania, usije uka take risk kwa imani kuna watanzania watakupambania. Take risk kwa sababu upo tayari kwa matokeo yoyote yatakayokujia.
Yes, tukishajitokeza kujaza mikutano ya siasa tumemaliza, tunarudi nyumbani kwa mizuka kulala tukijiona tumewamaliza CCM.

Kesho asubuhi tunaamkia vijiweni na mitandaoni kushangilia "nyomi" ya jana mkutanoni!.

Bado sana kufikia mabadiliko tunayohitaji, bado tupo gizani kifikra. Kuendelea kutafuta njia nyepesi ili kutatua tatizo gumu ni kujiliwaza kijinga.
 
CCM sio chama cha siasa tena, ni genge la kihalifu kama magenge mengine ya kihalifu (mafia,sinaloa,yakuza).

Chama cha siasa kinatakiwa kufanya siasa kama ambavyo CHADEMA wanavyofanya, lakini CCM kwa kuwa si chama cha siasa, ukihoji chochote kinyume na matakwa yao, unapotezwa mchana kweupe.

Polepole na Nchimbi ni mfano hai wa jinsi CCM ilivyogeuka kuwa genge la kihalifu kwa mgongo wa chama cha siasa.

Ni mwanaCCM yupi amejitokeza kuulizia kuhusu uwepo wa hawa waliokuwa viongozi waandamizi wa chama na serikali!!??

Kwenye mchakato wa "uchafuzi"wa kumpata mgombea wa genge la CCM, nfdugu Malisa alihoji kuhusu mchakato kuvurugwa, kilichompata sote tu mashahidi wa kilichomtokea.

Katiba mpya ndio mwarobaini wa kumaliza huu upuuzi unaofanywa na genge la kihalifu la CCM.
Lkn inakuwaje kupitia imani zetu tusiamue kuwatenga wote wanaoambatana na ccm..? Mfano makonda, hivi inawezekanaje anapewa nafasi kusimama mbele kanisani..mtu ambae si mfuasi wa ccm tu, ndie miongoni wa wanaotekeleza uharamia..je, imani zetu zinatusaidia kushape aina ya maisha yenye kutufanya kuchukia mambo mabaya..?
 
Hali hii kwa jicho la kiimani..pitia taarifa hii ya kihistoria kisha pima uhalisia na kilichofanyika wakati huo, lbd itasaidia kuona kosa lilifanyika wapi kiimani na lirekebishwe vipi..

"Wengi wetu tumebahatika aidha kushiriki au hata kuchangia mbio za Mwenge wa uhuru wa Tanganyia (Tanzania), lakini ni wangapi kati yetu tunajuwa asili haswa ya huo Mwenge!?
Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima. Wapo wanaodhani kwamba aliyeleta mabadiliko katika nchi kwa kuanzishwa kwa mwenge huo ni Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere lakini kiukweli haswa Mwalimu Nyerere si mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru.
Mnajimu maarufu ambaye sasa ni marehemu, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema na ikaandikwa kwamba mvumbuzi wa wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.
Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Sheikh Yahya Hussein (1925).
Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima (alifunga), jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.
Sheikh Yahya Hussein alinukuliwa akisema hata hivyo, katika mashimo yale Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya shimo kwa ajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wenzake nje wakimngoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es Salaam.
Utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema, zindiko la Bagamoyo linafanya kazi.
Kilichoshangaza, alisema ni mtu huyo kuingia shimoni na kukaa siku kumi na siku ya kumi na moja alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa, na alikuwa akiongea lugha hisiyojulikana.
"Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho," alisema Sheikh Yahya.
Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere:
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau."
Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)," alisema Sheikh Yahya.
Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo "UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI" akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.
Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:
"Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38," na ndivyo ilivyokuwa.
Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38 =115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.
Je, tambiko hili ndio matokeo ya udumavu kifikra na kimaamuzi kwa watanzania? TAFAKARI.
Asante sana kwa historia hii, kufahamu haya inatusaidia kurudi kwenye msingi wangu wa maombi. Kupangua hili ni kumwomba Mungu aingilie kati jambo hili zito.
 
Hapa ndio penye chimbuko la hali jinsi watanzania wengi walivyo..wmefunikwa blanket kwenye fikra zao na macho yao..unaweza kuona kwa wazi nani alianzisha hili tambiko, wala si Nyerere..na wanaolishikilia hadi sasa wanajulikana kupitia ccm..kwa hiyo wao na ccm ni kitu kimoja huwezi watenganisha..na malengo yao kwa ujumla ni kustawisha ufalme wa giza/shetani ktk nchi hii nzuri Mungu aliumba..! Pima kwa mfano, kanisa kubwa lenye misingi ya imani ya ukristo, mmoja wa waumini wake anafanyiwa uharamia wa kutisha hadharani, nchimbi anazuiwa hata kwenda kushiriki ibada na waumini wenzake..lkn ajabu waumini wakatoliki wako kimya, wachache km Prof. Tibaijuka wamekemea mambo km haya..wengine wote wanaona kinachofanyika ni sawa..kwa hali km hii, mkatoliki anafanya nini kubaki ccm, alivyofukuzwa nchimbi na anayotendewa..wakatoliki wote wangeachana na ccm kabisa..lkn uzito huu wa kutambua wanachofanyiwa na kuukataa unasababishwa na nini..? Hili tambiko wengi limedumaza kiwango cha utambuzi wao na kufanya uamuzi..wengi wako gizani, ni wakatoliki kwa majina tu lkn mioyoni mwao imani ya ukristo haipo!
 
Hoja zako zina nguvu, nashindwa kukukatalia, hasa nikipime kiroho unachoongea.
 
Back
Top Bottom