Tanzania itapigwa tena na Cape Verde

Tanzania itapigwa tena na Cape Verde

Ukweli unauma na ukweli haunaga uzalendo au laaa! kesho tutake tusitake wanaume wanatufanya vibaya wapendavyo
 
Kweli kabisa uwezo wa sisi kumfunga Cape verde haupo. Labda tutowe nao sare na ikitokea kamuujiza basi tutawafunga kamoja tena ka kibahati.
 
We kweli hujui mpira na wala hujui motivation factors. Labda niulize swali, hatujawahi kucheza na timu kubwa na wachezaji wao wakiwa wanacheza timu mbali mbali za nje na tukitoka nao draw au walau kuwashinda? "

Mpira ni strategies na pia hata bahati hutumika kwani mpira ni makosa na hivyo kufungwa na kufungwa au draw ni sehemu ya mchezo.

Ushauri wangu mimi ni kuwa tuna wachezaji wa serengeti boys, wapo wengine wapo ulaya, wale ni wazuri na waliwahi kuifunga hapa misri bao 5 na baadae bao 3. Wana uzoefu na wamecheza sana mechi za ugenini na za kimataifa, walau wachache wao waanze kupewa nafasi ili kuimarisha timu kama ambavyo timu kubwa kubwa huwa na Academy zao na huchukua watoto kuwapandisha juu na wanafanya vizuri. Mfano kwa azam kuna kipa Aishi manula, shaban chilunda, yahaya zayd, na wengineo

Hata simba na yanga wamefany hvy hvyo. Na hata timu za nje nazo hufanya hvy hvyo.

Iwapo tutataka mteremko, wapo wachezaji wengi sana na wengine wanaamua kubadilisha uraia kutokn na kutokuitwa kuchezea timu ya taifa na tayari wengine ni tegemeo sana katika timu zao huko German, Canada, England, Italy na kwingineko, nenda YouTube na uweze kusearch. Ila sijui kwa TFF sijui wanaogopa gharama au la. Huo ndo ushauri. Tofauti na hapo hata Ferguson au kocha yoyote mkubwa aje bongo hatuwezi kwenda mbele maana wachezaji hao ni wale wale miaka nenda rudi ni mbwana samatta tu.

Pia Kocha mkuu hana Muda wa kufundisha timu kutokn na Muda anaopewa. Labda tufanye kama Uganda walivyoweza kuchukua watoto wadogo wakakaa nao kwa miaka miwili then wakawaleta kucheza na timu ya taifa hapa zanzibar, tukapigwa bao mbili sijui 3 hadi kanavaro akawanyooshea mikono.

TUWE WAZALENDO KWA TIMU YETU
Maximo alishawafunga hawa Cape Buffalo Taifa mwaka 2007 kama sikosei 3-1 kumbukeni vizuri.Naunga mkono hoja yako.
 
Mtani na wewe unaisemeaje hiyo game kesho?
Mtani kesho Taifa Stars hana pakutokea, atafungwa tu. Na mda 'mashabiki' wa Taifa Stars pressure ikipanda na kushuka.. Mimi nitakua makini na timamu nikiwafatilia CR7 wa Uganda, Okwi na Juuko Murshidi wakiiongoza Uganda dhidi ya Lesotho.
 
Mtani kesho Taifa Stars hana pakutokea, atafungwa tu. Na mda 'mashabiki' wa Taifa Stars pressure ikipanda na kushuka.. Mimi nitakua makini na timamu nikiwafatilia CR7 wa Uganda, Okwi na Juuko Murshidi wakiiongoza Uganda dhidi ya Lesotho.
Hahahaaaa. Mtani kama kawaida yako na Okwi waki.

Ila fuata vile moyo wako utapata furaha Mtani ya nini kuhangaika na timu ya kutupa presha kila kukicha.
 
Hahahaaaa. Mtani kama kawaida yako na Okwi waki.

Ila fuata vile moyo wako utapata furaha Mtani ya nini kuhangaika na timu ya kutupa presha kila kukicha.
Hahaha.. Ni kweli kabisa mtani.. Mechi iliyopita Uganda waliwakung'unta Lesotho 3 kavu huku Okwi akiingia kambani mara 2.. Sasa hiyo kesho kuna hatari Lesotho akapigwa 5 huku Okwi akiondoka na mpira wake.
 
Hahaha.. Ni kweli kabisa mtani.. Mechi iliyopita Uganda waliwakung'unta Lesotho 3 kavu huku Okwi akiingia kambani mara 2.. Sasa hiyo kesho kuna hatari Lesotho akapigwa 5 huku Okwi akiondoka na mpira wake.
Duuh! Mtani nanihamasisha na mie niicheck hiyo game.

Inachezwa saa ngapi hiyo kesho?
 
MWAKA 2000 CAPE VERDE ilikuwa namba 182
Miaka kumi tu.. wapo nafasi ya 67

Bado huamini kuwa wapo juu yetu sasa ona maajabu yafuatayo hapa chini

KIKOSI cha sasa cha CAPE VERDE
na TANZANIA

1.THIERY GRACA
anacheza ligi kuu ya Ureno klabu ya Estril

AISHI MANULA
Simba

2.STOPIRA
anacheza videoton
Wanashiriki Europe league walifungwa 1:0 kwa tabu sana na Chelsea pale Darajani

2.KESSY
Nkana Red Devils Zambia

3.FERNANDO
anacheza PAOK salonike wanashiriki Europe league

3.Gadiel michael
Yanga

4.ALMEIDA
anacheza uniao madeira Ureno

4.MWANTIKA
Azam
5:NUNo ROCHA
Anacheza Tosno ya ligi one Urusi

5:AGREY
AZAM FC

6:JANILO
Anacheza HERACLES ligi kuu ya Uholanzi

6.Abdi BANDA
BARoka fc LIGI KUU YA SAPL

7:CARLos
Anacheza Aves ligi kuu Ureno

7:Himid Mao
Petrojet ligi kuu ya Egypt

8:Tavales
Mchezaji tegemeo wa DIJON ya ligi kuu ya UFARANSA

8:MUDATHIRI
AZAM

9:ZE LUIS
Anacheza SPARTAK MOSCOW ya ligi kuu ya URUSI na wanacheza EUROPE LEAGUE

9: ULIMWENGU
LIGI KUU YA SUDAN

10: GARY RoDRIGUEZ
Straika tegemez wa GALATASARAY ya Uturuki wanashiriki UEFA

10:SAMATA
GENK .. EUROPE LEAGUE

11:KUCA
Anacheza Boavista ligi kuu Ureno

11:MSUVA
Difaar Hasan Al Jaadid ligi kuu ya Morocco

hawa ni wachezaji 11 wa pande zote mbili...sasa Hivi kweli bado unamlaumu Amunike kwa kipigo cha juzi...???

Eti kamuacha mkude,kichuya,nyoni,yndani,

Hebu tuweni na AIBU ukweli ni kuwa hatuna wachezaji wa kutupa matokeo chanya yenye muendelezo MPIRA NI SAYANSI sio blah blah wenzetu wanawekeza sisi tunasubiri miujiza

Tusubiri kwanza mpaka tutakapo amua kuwa serious...hii ni kwa yule binti ambae alisema Cape Verde ni wa kawaida *SAAAANA*
Napata tabu sana na kizazi hiki..Waganda wamewafunga Cape Verde kwao kwani wanawachezaji wangapi Ulaya....Zambia ilipowafunga Ivory Coast fainali ya AFCON na kuchukuwa ubingwa walikuwa wana wachezaji wangapi Ulaya????Tumeshawahi kuwafunga Morocco goli tatu kwa mchina...
 
Hili napingana nalo, kwenye soka hakuna kitu kama hicho, angalia Madrid ya akina Figo, Raul, Ronaldo, Beckham hawakuchukua uefa aisee,
Wao wawe committed na game tuu
 
Back
Top Bottom