Tanzania itavunja rekodi kuwa nchi ya kwanza Afrika, Mgombea urais wao anaishi Ulaya anakujaga kugombea urais Afrika

Tanzania itavunja rekodi kuwa nchi ya kwanza Afrika, Mgombea urais wao anaishi Ulaya anakujaga kugombea urais Afrika

Kama ingelikua hajashambuliwa kwenye Ardhi yake na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ningeunga mkono hoja ya bandiko

#yuko wapi Mayalla
Kwa hiyo mwakyembe nae akaombe hifadhi ubelgiji?
 
usisahau pia Tanzania ni nchi ya kwanza kuwa na mgombea uraisi aliyemiminiwa risasi nyingi kama walikuwa wanaua tembo ila akatoka hai na serikali ikagoma kata-kata kugharamia matibabu hili-hali alikua ni Mbunge.
 
Hivi jamani kama hamna la kusema ni lazima muandike hapa? Mwandishi wa uzi huu hajui historia za nchi zozote za afrika zaidi ya Tanzania halafu anataka kusema jambo la kuihusisha bara zima la Afrika. Hivi ni kwa nini hakufanya research ndogo tu ya kutafuta katika internet waliowahi kugombea urais barani afrika wakati wakiishi nchi ya nchi zao ikiwamo nchi za ulaya?

Inawezekana huyu mwenzetu nae amekuwa na mentality ile ya wamarekani wanaofikiri neno the world linaashiria USA na huyu anadhani neno afrika linaashiria zanzibar na tanganyika. 🙂
 
Kama ingelikua hajashambuliwa kwenye Ardhi yake na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ningeunga mkono hoja ya bandiko

#yuko wapi Mayalla
Huyo kibaraka chizi Lissu alikuja hapa kwenye kampeni mwaka jana, akazurura mpaka manzese kwa mfuga mbwa, tandale kwa tumbo, kwa Ali maua, vingunguti, kiembembuzi, Mwanza Makoroboi, mabatini, Musoma bweri, butiama mpaka kwa mwalimu, mbona hakupigwa risasi?? huyo ni kibaraka wa mabeberu anapikwa kuja kugawa nchi kwa mabeberu na ndio maana wanakaa naye wanamlisha wanamvisha na kumkogesha kama mwari ili waje wamtumie. There is no free lunch in europe we bro
 
Huyo kibaraka chizi Lissu alikuja hapa kwenye kampeni mwaka jana, akazurura mpaka manzese kwa mfuga mbwa, tandale kwa tumbo, kwa Ali maua, vingunguti, kiembembuzi, Mwanza Makoroboi, mabatini, Musoma bweri, butiama mpaka kwa mwalimu, mbona hakupigwa risasi?? huyo ni kibaraka wa mabeberu anapikwa kuja kugawa nchi kwa mabeberu na ndio maana wanakaa naye wanamlisha wanamvisha na kumkogesha kama mwari ili waje wamtumie. There is no free lunch in europe we bro
Wahisani wa Umoja wa Ulaya walikinga kifua mbona mambo walikuwa hadharani kila mbabe ana mbabe wake bwashee
 
Je alienda ulaya kwa kupenda??

Pia je vipi kuhusu mijizi iliyoiba pesa za walipa kodi na imezificha ulaya halafu inawasanifu huko nyumbani?

Zoezi la viongozi kuorodhesha mali zao ziliishia wapi?

Leo hii uzalendo ni kumsifia mtu au kikundi cha watu!
 
Mwakyembe na Mangula huo mchezo wa ndani bibiye
Kwa hiyo umekubali ni kweli kwamba kilichompata Tundu ulikua mchezo wa nje eee😅😅😅😅😅
Ndio maana hata namba2 alisema hakuna askari anaweza fanya walichofanya kwa Tundu, ni wahuni tuu ndio wanaweza fanya hivyo

Haya nimekuelewa
 
Kwa hiyo umekubali ni kweli kwamba kilichompata Tundu ulikua mchezo wa nje eee😅😅😅😅😅
Ndio maana hata namba2 alisema hakuna askari anaweza fanya walichofanya kwa Tundu, ni wahuni tuu ndio wanaweza fanya hivyo

Haya nimekuelewa
CCM ina Mauaji ya ndani yaani wao kwa wao sasa Lissu alikuwa auwawe lakini si mwanaCCM ndio point yangu
 
Nimegundua PROPAGANDA jina lake lingine ni KIKI
 
Wakati nchi nyingi za bara la afrika zimekuwa zikitia aibu na marais ambao wakichaguliwa aidha wanakaa nunusu kwa nusu Ulaya na nyumbani au kuamia kabisa Ulaya, Marekani au hata Falme za kiarabu na kuwa na miji huku na kuona hayo ni maisha ya kiongozi. Hii imekuwa aibu na fedhea sana kwa bara hili la Afrika ambalo wazungu walilialibu na kufanikiwa kuharibika.

Wakati haya yakienelea kutuongezea aibu kubwa pia linatokea lingine la mwaka katika nchi ya Watanganyika na Wazanzibari kwani tayari 2020 kupitia chama cha ukombozi, ambacho pia kiliwai kuwa chama kikuu cha upinzani TZ tulipata mgombea Urais mzalendo aliye beba ukombozi wa watanzania akitokea Ulaya. Taarifa za ndani kabisa za chama hicho ambazo zimevuja zinasema kuwa chama hicho bado kinamuandaa mleta ukombozi huyo na mzalendo kutoka Ulaya kuja kugombea tena 2025.

Kwa maana hiyo Tanzania itakuwa inafunga ukurasa wa historia ya aibu katika bara la Afrika kwani viongozi wengi wa kizalendo walikuwa wanaanda mashambulizi ya kupata uhuru kutokea nchi za Afrika kwa Afrika kama Samora Machel, Mugabe, Museven na wengine wengi, lakini huyu yeye kaenda mbali anaanzia kwa mabeberu kuja Afrika kama Savimbi.

Hiki chama cha ukombozi pia kiliwai kuwa chama kukuu cha upinzani hapa nchini licha ya kututia aibu katika mambo mengi ambayo yamekuwa gumzo Afrika na duniani kuwa na siasa za kushangaza kama kuwa na chama Saccos na kinakusanya sadaka kama kanisa au msikitini, kuwa na siasa za kiki na maandamano kila kuchao. kilishangaza zaidi ulimwengu baada ya kuwa siasa za kutafuta kiki hata katika misiba na majanga ya asili. Lakini pia wamewashangaza wengi kwa uwezo usio wa kawaida wa kuwa wasahaulifu hata kama wameongea jana tu leo wanasahau kuwa walisema nini jana.

Kuna baadhi ya mambo ya kustaajabisha kuna wakati walikuwa wanatangaza maandamano nchi nzima lakini ilikuwa inatokea Rais anawaita Ikulu wanapewa bahasha na kahawa ya Ikulu wanasimamisha ukombozi wote waliotaka kuufanya. Ni aibu ambazo tulipata wote kama nchi kwani hawakuwa na woga wala haja ya kujadili kama kuna ishu ya pesa mbele wako tayari kutoa na kuweka giabox nyingine angani hata kama ni hata watabadili gia ngani, hili lilitokea wakati wanamchukuwa mgombea kutoka chama tawala ambaye kwa miaka 8 walimtusi kuwa fisadi na mwizi aliyeshindikana Afrika mara...

Wadadavuaji wa mambo ya siasa wanasema kuwa kutokana na kuwa Tanzania inamgombea kutokea Ulaya hilo litarahisisha Tanzania kuingizwa katika umoja wa Ulaya kirahisi zaidi. Kwani hadi sasa tunaogea tayari upendo mkuu wa wazungu tumeuona kwani walileta Utumwa, mapinduzi ya viwanda, ukoloni, ubepari, imperializimu, democrasia na dini na tamaduni zake ambavyo vyote vimekuwa msaada mkubwa wa maendeleo ya bara letu sasa tukipata Rais kutokea Ulaya kilakitu kitakuwa sawa.

Wakati wa uchaguzi maisha yake hayako hatarini, lakini baada ya uchaguzi maisha yake yanakuwa hatarini. Sisi tupo na vichinjio vyetu; tunamsubiri 2025!
 
Wakati mwingine ninasikia aibu kutambuliwa pamoja na mleta mada kama watanzania!!

Yaani hata mtu ameishi wapi nayo ni taabu. Mbona viongozi wako wamesoma nje, au mnataka viongozi wawe waliosoma Tanzania tu?? Tutafikia kama mtu kasoma shule ya serikali au binafsi. Kisha yeyote aliyewahi kuishi nje si mzalendo nk.

Ubaguzi unaendelea kukua! Ninadhani akigombea usimpigie kura na itakuwa imetosha. Au vipi??
 
Back
Top Bottom