Tanzania itavunja rekodi kuwa nchi ya kwanza Afrika, Mgombea urais wao anaishi Ulaya anakujaga kugombea urais Afrika

Kama ingelikua hajashambuliwa kwenye Ardhi yake na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ningeunga mkono hoja ya bandiko

#yuko wapi Mayalla
Kwa hiyo mwakyembe nae akaombe hifadhi ubelgiji?
 
usisahau pia Tanzania ni nchi ya kwanza kuwa na mgombea uraisi aliyemiminiwa risasi nyingi kama walikuwa wanaua tembo ila akatoka hai na serikali ikagoma kata-kata kugharamia matibabu hili-hali alikua ni Mbunge.
 
Hivi jamani kama hamna la kusema ni lazima muandike hapa? Mwandishi wa uzi huu hajui historia za nchi zozote za afrika zaidi ya Tanzania halafu anataka kusema jambo la kuihusisha bara zima la Afrika. Hivi ni kwa nini hakufanya research ndogo tu ya kutafuta katika internet waliowahi kugombea urais barani afrika wakati wakiishi nchi ya nchi zao ikiwamo nchi za ulaya?

Inawezekana huyu mwenzetu nae amekuwa na mentality ile ya wamarekani wanaofikiri neno the world linaashiria USA na huyu anadhani neno afrika linaashiria zanzibar na tanganyika. πŸ™‚
 
Kama ingelikua hajashambuliwa kwenye Ardhi yake na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ningeunga mkono hoja ya bandiko

#yuko wapi Mayalla
Huyo kibaraka chizi Lissu alikuja hapa kwenye kampeni mwaka jana, akazurura mpaka manzese kwa mfuga mbwa, tandale kwa tumbo, kwa Ali maua, vingunguti, kiembembuzi, Mwanza Makoroboi, mabatini, Musoma bweri, butiama mpaka kwa mwalimu, mbona hakupigwa risasi?? huyo ni kibaraka wa mabeberu anapikwa kuja kugawa nchi kwa mabeberu na ndio maana wanakaa naye wanamlisha wanamvisha na kumkogesha kama mwari ili waje wamtumie. There is no free lunch in europe we bro
 
Wahisani wa Umoja wa Ulaya walikinga kifua mbona mambo walikuwa hadharani kila mbabe ana mbabe wake bwashee
 
Je alienda ulaya kwa kupenda??

Pia je vipi kuhusu mijizi iliyoiba pesa za walipa kodi na imezificha ulaya halafu inawasanifu huko nyumbani?

Zoezi la viongozi kuorodhesha mali zao ziliishia wapi?

Leo hii uzalendo ni kumsifia mtu au kikundi cha watu!
 
Mwakyembe na Mangula huo mchezo wa ndani bibiye
Kwa hiyo umekubali ni kweli kwamba kilichompata Tundu ulikua mchezo wa nje eeeπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Ndio maana hata namba2 alisema hakuna askari anaweza fanya walichofanya kwa Tundu, ni wahuni tuu ndio wanaweza fanya hivyo

Haya nimekuelewa
 
CCM ina Mauaji ya ndani yaani wao kwa wao sasa Lissu alikuwa auwawe lakini si mwanaCCM ndio point yangu
 
Nimegundua PROPAGANDA jina lake lingine ni KIKI
 

Wakati wa uchaguzi maisha yake hayako hatarini, lakini baada ya uchaguzi maisha yake yanakuwa hatarini. Sisi tupo na vichinjio vyetu; tunamsubiri 2025!
 
Wakati mwingine ninasikia aibu kutambuliwa pamoja na mleta mada kama watanzania!!

Yaani hata mtu ameishi wapi nayo ni taabu. Mbona viongozi wako wamesoma nje, au mnataka viongozi wawe waliosoma Tanzania tu?? Tutafikia kama mtu kasoma shule ya serikali au binafsi. Kisha yeyote aliyewahi kuishi nje si mzalendo nk.

Ubaguzi unaendelea kukua! Ninadhani akigombea usimpigie kura na itakuwa imetosha. Au vipi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…