Tanzania iwekeze pesa nyingi kwenye waokoaji kuliko magari ya viongozi

Tanzania iwekeze pesa nyingi kwenye waokoaji kuliko magari ya viongozi

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,880
Afrika ili tuonekane tuna akili inabidi ifike wakati tuweke pesa kwenye "emergency responders" zaidi kuliko kuwekeza mabilioni kununua magari ya kukaa viongozi moja moja badala yake tuwekeze kwenye kuokoa raia kwenye majanga.

Ajali ya precision imetuonyesha kuwa kama nchi tuko nyuma sana kwenye "first responders"(polisi, paramedics, firefighters, emergency medical technicians), yani hawa watu tunao ila ajali inatokea inabidi wapande daladala kwenda eneo la tukio bila vifaa kwa nauli zao kuokoa maisha ya wahanga.

Nchi za wenzetu hawa watu ndo walitakiwa wajae pale aneo la ajali sekunde mbili baada ya ajali na magari yao na ving'ora na vifaa mbalimbali vya uokoaji kabla hata wavuvi hawajavuka wameshazungushia barricade tape wanaendelea na uokoaji.

Sielewi tuna raia million 61 tunatumia billioni 600 tunanunua magari ambayo linakaa jitu moja moja alafu inatokea janga tuna parade wavuvi kwenye mabunge wakati tuna first responders wanatakiwa wawe eneo la majanga kwa nauli zao za daladala alafu tunashangaa kwanini kwenye tv za nje tunaonekana kama manyani kwenye mitumbwi.
 
Afrika ili tuonekane tuna akili inabidi ifike wakati tuweke pesa kwenye "emergency responders" zaidi kuliko kuwekeza mabilioni kununua magari ya kukaa viongozi moja moja badala yake tuwekeze kwenye kuokoa raia kwenye majanga.
Umeongea suala la msingi sana. Waafrika sisi kwa kiasi kikubwa ni wapuuzi sana linapokuja suala la vipaumbele. Hayuna vipaumbele. Tumewekeza kulinda wanasiasa na maslahi yao kuliko maisha ya raia na maslahi mapana ya nchi zetu kwa ujumla.

Ukiangalia gharama ambazo serikali inawekeza kwenye magari ya washawasha, helikopta na defender (kupambana na wanaokosoa serikali), gharama hizo zilitosha kabisa kuwekeza kwenye uokozi wa raia dhidi ya majanga kama mafuriko, moto na ajali kubwakubwa. Mbaya zaidi hakuna kiongozi hata mmoja aliejiuzulu kutokana kutowajibika wakati wa ajali.
 
Tatizo wataalam wamegeuka wanasiasa Kazi za kitaalam zinakuwa za kisiasa

Nitoe mfano mmoja Wizara ya Ardhi. Mtaalam Kamishina anajuakabisa Eneo linabadilishwa matumizi kutoka Mashamba kuwa Mji Eneo Lina hati miliki kiserikali.

Mtaalam huyo huyo baada yakuwa Mbuge Anafumbia macho wakazi halali wanapo dhulumiwa Ardhi yao
Aibuuuu ndiyo Tz
 
Umeongea suala la msingi sana. Waafrika sisi kwa kiasi kikubwa ni wapuuzi sana linapokuja suala la vipaumbele. Hayuna vipaumbele. Tumewekeza kulinda wanasiasa na maslahi yao kuliko maisha ya raia na maslahi mapana ya nchi zetu kwa ujumla. Ukiangalia gharama ambazo serikali inawekeza kwenye magari ya washawasha, helikopta na defender (kupambana na wanaokosoa serikali), gharama hizo zilitosha kabisa kuwekeza kwenye uokozi wa raia dhidi ya majanga kama mafuriko, moto na ajali kubwakubwa. Mbaya zaidi hakuna kiongozi hata mmoja aliejiuzulu kutokana kutowajibika wakati wa ajali.

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
Nimeona lawama nyingi sana kwa hawa waokoaji ila tatizo ni la wanasiasa. Ifike wakati watu wawajibike, vipaumbele vyao ni vitambi vyao.
 
Jamii yetu yenyewe, nayo ni tatizo. Hata uzembe wa wazi kabisa wa Serikali, bado utapata majitu yanatetea huo uzembe. Mtu akihoji utendaji wa Serikali, hasa Waziri Mkuu, utasikia kuwa eti wanaohoji wana chuki naye au wanautaka Uwaziri Mkuu! Hoja za kijinga kabisa.

Yaani kila mmoja autake Uwaziri Mkuu au Uwaziri wa Mambo ya Ndani, wanaacha kujibu hoja, wanakimbilia kulinda vyeo.

Ndiyo maana Rais Obama alisema kuwa Afrika haiendelei kwa sababu viongozi badala ya kufikiria namna ya kuyaletea mataifa yao maendeleo, wao wakati wote wanafikiria vyeo.
 
Back
Top Bottom