Tanzania izuie matumizi ya Mtandao wa Tiktok

Tanzania izuie matumizi ya Mtandao wa Tiktok

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Hello wanajf,

Mtandao wa Tiktok ni mtandao unaokuja kwa Kasi Sana.

Mtandao huu unatengeneza addiction Fulani ambayo inamfanya mtu asichoke kabisa kuutumia.

Nilichokiona mpaka sasa ni kwamba asilimia kubwa ya vijana, watoto na wazee wanashinda huko.

Athari za baadae
👉 kupunguza uwezo wa watu kufikiria na kuchanganua matatizo kwasababu ya uraibu

👉Kuongezeka kwa uzembe utakaoathiri uchumi wa mmoja mmoja hatimaye taifa zima.

👉Vijana na ubunifu ndio itakuwa basi.

👉Kuongezeka mmomonyoko wa maadili kwani ticktock video za utupu ndio huuza Sana so wadada wengi wameona ndio fursa kwao Jambo litakaloathiri vijana.

👉Umasikini Kuongezeka kwani pesa inayotumika kwa ajili ya bando ni kubwa, imagine bando la buku Tiktok ni dakika 45 tu basi ikiwa mtu atashinda huko pesa nyingi Sana zinapotea ambazo zingefanya Mambo mengine.

Hivyo Kama ilivyo kwa nchi zingine Kama vile China , India, Turkey, North Korea na zinginezo ambazo zimezuia matumizi ya mtandao wa Tiktok.

Nashauri Tanzania nayo iangalie namna ya kuwaokoa vijana kwa uraibu wa huu mtandao.

Karibu kwa maoni
 
Kuna vitu watu huwa wanajiendekeza tu, haswa uraibu wa mitandao kama hiyo jamii ya tiktok, instagram, snapchat n.k

Ukiona una uraibu wa hiyo mitandao, ujue huna majukumu yanayokuweka 'busy'
 
Ni Watanzania wangapi wenye smartphone, na kati ya hao ni wangapi wenye ku afford full access ya internet, na kati ya hao ni wangapi wenye tiktok, na ni wangapi kati yao wanajielewa? TUANZIE HAPO KWANZA.
 
Hilo nalo litegemee maamuzi ya Gvt kweli.
Utashi Wa mtu binafsi. Maisha ni vile unachagua kuwa mjinga au laa.

Kinachotuponza wengi wetu ni urimbukeni na umasikini. Kutaka kujionesha Kwa Mambo yasiyo na manufaa

Ukitazama Kwa % kubwa huko Tick-tock wengi ni vijana wa kike kuonesha matako, kucheza kuimba. Na ujinga ujinga mwingi.

Hayo yote nimatokeo ya mabadiliko ya teknolojia tutegemee baada ya Miaka 10 mabadiliko makubwa zaidi.

Swali je jamii na Taifa Kwa ujmla limejiandaa Kwa hayo mabadiliko?

Je haya mabadiliko yatatuacha salama au ndio tunaangamia Kwa kukosa maarifa.

Ni vigumu sana kuzuia mabadiliko ya Aina yoyote ile yawe ya kimwili, akili, hisia, teknolojia, mazingira na kimaadili katika nyakati kama hizi. Hilo ukubali au ukatae lipo na litaendelea kuwepo.
 
Ni waTanzania wangapi wenye smartphone, na kati ya hao ni wangapi wenye ku afford full access ya internet, na kati ya hao ni wangapi wenye tiktok, na ni wangapi kati yao wanajielewa? TUANZIE HAPO KWANZA.
Maana yake the way you present an issue seems like unatuletea ushuhuda kutoka kwenye sample ya mademu zako na washkaji wa kitaa Sinza na ilala sijui na kimara & the like halafu ukaja na general conclusion hapa JF kwa GT. We need to question this first. Tujue hiyo recommendation yako imepitia methodology zipi?!
 
Umeeleza ukweli mtupu.
Umeunga hoja ambayo kiuhalisia Haina ukweli,,,. Iko hivi watanzania tupo zaidi ya million 65

1. Milioni ngapi Wana Smart phone au hawana smart phone

2 . Million ngapi hawajui tictok ingawa Wana Smart phone

3. Wangapi wanaijua TikTok lakin hawana bando

4. Wangapi wanaijua TikTok na Wana bando lakin hawapati mda wa kuingia TikTok

5. Wangapi waijua TikTok na Wana bando ila ni dakika ngapi Wana spend Kwa kuingia TikTok

6. Mwisho .........chukua namba Moja Hadi 6 jumlisha upate jumla alafu utoe total ya watanzania wanaobaki ni kiasi gan?

Isharrah
 
Back
Top Bottom