mimi sijaingia tiktok, sijui hata unachosema. ila najua huko majuu watu wanatengeneza pesa kupitia mtandao huo. pili, haya mambo yote ni ya kishetani, hata hizi computer na simu ni za kishetani, kwa wajuzi wanaelewa kwamba long before computers were invented, ulimwengu wa kuzimu/ushetanini huko walishakuwa wanatumia computer kitambo. sayansi nyingi hutoka kwa mashetani, hata hao kina elon mask matajiri, wana connection ya mashetani, hata kwenye mambo ya kawaida ukiona kitu kinasababisha uraibu jua kuna mkono wa shetan nyuma yake, mfano nyimbo za diamond kwa watoto, ajenti wa kuzimu na manyimbo anaimba ni ya kishetani ila watu wanayapenda. mitandao ya porn, mitandao mbalimbali, tamthilia za kizinzi na mambo mengi kama hayo huwa kunakuwa na upako wa kishetani, hivyo hata ukikwepa hili utakutana na lile na mbaya zaidi hata kama wee hufanyi jirani yako atafanya. kwa msiojua, hata design nyingi za magari huanzia kuzimu, kuna watu huitwa magenius au watu wenye akili nyingiiii wengi huwa na vimelea vya kishetani au wanapagawa na mashetani ndio yanakuwa yanafanyakazi ndani yao.
uyaonapo hayo, changamke, Mwana wa Adam yu karibu malangoni, mwenye kanisa anakuja kuchukua walio wake, kama mchungaji agawanyishavyo kondoo na mbuzi, atawagwanya kondoo kulia na mbuzi kushoto, ndipo kitakapokuwa kilio na kusaga meno kwa wale watakaokuwa mbuzi. walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye hata malaika walio mbinguni ila Baba, basi kesheni kwakuwa hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. kama mwenye nyumba angelijua saa mwivi atakayokuja hakika angelikesha wala asingeiacha nyumba yake kuingiliwa. Okokeni mponye nafsi zenu. tubuni mkabatizwe kwa Jina lake Yesu mpate ondoleo la dhambi nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kwakuwa aaminiye na kubatizwa ndiye atakayeokoka na asiyeamini atahukumiwa. bila Yesu hapa duniani ni kazi bure.