Vita vya Kagera lazima Amin angeshindwa maana Waganda wenyewe walikua wamemchoka hawamtaki, hivyo wakaruhusu nchi yao ikojolewe na jirani, ukizingatia pia maelfu ya waasi na wafuasi wapiganaji wa Museveni, Tito Okello na wale wa Ojok waliungana na jeshi la Tanzania, na pia kunao wapiganaji kutokea Msumbiji wote pia walihusika dhidi ya nduli Amin.
Halafu wengi wa wanajeshi wa Amin walikua majizi, hawakua na uzalendo, hawangepigana hadi mwisho, walitaka fursa za kuiba tu, bora hata wale wa Hitler ambao walizingua kishenzi, hawa wa Amin walikimbia uwanja wa mapambano baada ya kupora.