Tanzania kila kata hatuwezi fanya harambee za kuboresha shule zetu?

Tanzania kila kata hatuwezi fanya harambee za kuboresha shule zetu?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Kwanini tusifanye harambee kuboresha shule zetu ili vizazi vyetu vipate elimu bora na kupata taifa la wenye akili.

Kuna uzi humu kanisani kijitonyama milioni 300 ya kununua nyumba ya mchungaji ilichangwa nusu saa tu.

Nikawaza watoto wanaosali hapo kanisani je wote wanapata elimu nzuri kwenye shule wanazosoma jirani na hapo kijitonyama.

Hivi kila kaya katika kata yake ikiamua kuchanga elfu 10 tu. Hatuwezi boresha shule zetu za msingi na sekondari za uma katika kata zetu ziwe na miundombinu mizuri na lugha za kufundishia ziwe english medium kama tusiime na zingine tunazolipia mamilioni.

Harambee za maendeleo mbona hazipo?
 
[emoji848] usimamizi wake utakua vipi hapo?!

Kwani kanisani usimamizi upo vipi?

Viongozi wanaweza simamia kwa mfumo wa digitali.. zinatengenezwa line kama za vicoba. Hela zote zinalipwa kwa mobile money bila makato ya kutolea na hakuna mwenye password ya kuzitoa mpaka mpesa wenyewe voda waruhusu kwa utaratibu mgumuu.. then kwenye utekelezaji anafanya mkurugenzi ama diwani wa kata ila ma auditor wanakuwa big 4 company kama pwc, kpmg, delloite ama ey kutazama value for money ya ilichokarabati . Na watalipwa huduma yao Kwa hela itakayokatwa kwenye hiyo iliyopatikana kwenye harambee
 
.hii ngumu kwani watanzania wabinafsi na wanafiki sana ...mambo ya msingi kwa maendeleo yao huwa hawayaoni...fikiria harusi zinavyochangiwa ..alafu hela yote inaliwa siku ya harusi...
 
Aiseee Padri kanunuliwa nyumba ya million 300 na waumini wanaoishi nyumba za kupanga 🤣🤣.
 
kuna hoja ya muhimu hapo... kiukweli vitu kama hivyo, shule, zahanati, barabara za mitaa, mitaro na madaraja ya mitaani tungekuwa na muunganiko thabiti chini ya uongozi usio na shaka tulikuwa Kata tunamaliza wenyewe serikali inatoa support ya wataalamu tu.
 
Kutwa kuponda walimu humu,daa ngapi wakumbuke kujenga hizo shule😳
 
Back
Top Bottom