Tanzania kuanza kutumia 5G. Sheria ya kulinda Taarifa binafsi za Wananchi yaja

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
IMG_20210518_043738_408.jpg

Na Prisca Ulomi, WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake.

Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa.

“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini.
 
Tulipitishwa kipindi kigumu sana kama taifa. Lakini kwa NEEMA tu tumekombolewa!

Ni kama vile tunafufuka toka kuzimu na kuunda LEGACY mpya ambayo ni GENUINE isiyohitaji mapambio wala kulindwa kwa mtutu wa bunduki.

Mungu ni mwema wakati wote. TAZAMA YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA!
 
Sasa na sisi tunaanza kuenda na wakazi wa Dunia sio kama kipindi kile sheria zote anatunga yule Sadist
 
Mbona hiyo ipo kwenye katiba, uhuru wa FARAGHA na kutoingiliwa mawasiliano binafsi ya mtu.
 
Simu zetu nyingi naona ni 4G hiyo 5G si watapata watu wachache
 
SERIKALI MBIONI KUTUNGA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI

Na Prisca Ulomi, WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake

Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa

“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Tulipitishwa kipindi kigumu sana kama taifa. Lakini kwa NEEMA tu tumekombolewa!

Ni kama vile tunafufuka toka kuzimu na kuunda LEGACY mpya ambayo ni GENUINE isiyohitaji mapambio wala kulindwa kwa mtutu wa bunduki.

Mungu ni mwema wakati wote. TAZAMA YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA!
Umevuka mipaka ya kusifia, hebu rudi nyuma kidogo mpaka tupate Katiba Mpya.
 
^nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G^

Linii!??? Mr TCRA!??? Mbona kila barua unayoiandika ina tarehe!

^Iko mbioni^
^Tuko kwenye mchakato^
^Serikali iko kwenye hatua za mwisho^
^Inamalizia awamu ya mwisho^
^tuko kwenye upembuzi yakinifu, uchanganuzi & usanifu^
^Haitachukua muda mrefu^
^Hivi karibuni^
^Muda si mrefu^

#Wanatuchelewesha sana!!!
 
nadhani itakua majaribio tu ...lkn kiukweli hatujafikia level ya kuhitaji matumiz ya 5G....

5G is the fifth generation of wireless technology. But users will know it as one of the fastest, most robust technologies the world has ever seen.

That means quicker downloads, much lower lag and a significant impact on how we live, work and play. The connectivity benefits of 5G are expected to make businesses more efficient and give consumers access to more information faster than ever before.
1. Connected cars,
2. smart communities,
3. industrial IoT,
4. immersive education—they all will rely on 5G networks.
 
Na Prisca Ulomi, WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake.

Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa.

“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini.
Gwajima atapinga sana 5G sijui kama ana kumbukumbu ya alichowahi kusema kuhusu 5G
 
Tulipitishwa kipindi kigumu sana kama taifa. Lakini kwa NEEMA tu tumekombolewa!

Ni kama vile tunafufuka toka kuzimu na kuunda LEGACY mpya ambayo ni GENUINE isiyohitaji mapambio wala kulindwa kwa mtutu wa bunduki.

Mungu ni mwema wakati wote. TAZAMA YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA!
Ni hatua lakini bado. Ifike mahali kila mhimili ufanye kazi yake stahiki. Katiba mpya ni muhimu. Iligeuka mtu ni nchi na nchi ni mtu. Mapambio yakazidi walau ss tunapata ufahamu
 
Hili lilikua ni ombi langu kila siku hatimaye serikali yetu tukufu imeanza mchakato wa 5g

Asante rais wangu mama samia

Kilikua kilio changu cha muda mrefu

jamiiforums-___CO__7mED1dy___-.jpeg
BeautyPlus_20210518105228207_save.jpeg
 
Tulipitishwa kipindi kigumu sana kama taifa. Lakini kwa NEEMA tu tumekombolewa!

Ni kama vile tunafufuka toka kuzimu na kuunda LEGACY mpya ambayo ni GENUINE isiyohitaji mapambio wala kulindwa kwa mtutu wa bunduki.

Mungu ni mwema wakati wote. TAZAMA YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA!
Hii Corona ilikuwa blessings in disguise
 
Back
Top Bottom