SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Ulitaka atumbuliwe mara ya pili. Mambo mazuri hayataki haraka,si unaona sasa kiulaiiiini.Huyu waziri amwpaya sana, kwanini hakuyafanya haya kabla ya 17 March.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulitaka atumbuliwe mara ya pili. Mambo mazuri hayataki haraka,si unaona sasa kiulaiiiini.Huyu waziri amwpaya sana, kwanini hakuyafanya haya kabla ya 17 March.
Yule sponsor wa Sukuma Gang alisema 5G inatumika kueneza Corona.Gwajima atapinga sana 5G sijui kama ana kumbukumbu ya alichowahi kusema kuhusu 5G
Teknolojia hii tu tuliyonayo bado haina tija, nilidhani wangefanya kwanza kuboresha miundo mbinu kama vile mkonga wa taifa ambao unateknolijia ya kisasa kwa maana huo wa zamani na teknolojia yake sidhani utatusaidia sana, jijini Dar Es Salaam tu mawasiliano ni ya shida .
Na Prisca Ulomi, WMTH
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake.
Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa.
“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini.
Wakizingua kwenye katiba hatuwakopeshi kwasasa kwa hili wanastahili hizi sifaUmevuka mipaka ya kusifia, hebu rudi nyuma kidogo mpaka tupate Katiba Mpya.
This has cost implication, talking of fast downloads, 4k, FHD means speed ya kula mb itakuwa kubwa, ni vizuri mkawaandaa watu wasije letu vilio vya mbona nikiweka 10gb inaisha siku mbili?nadhani itakua majaribio tu ...lkn kiukweli hatujafikia level ya kuhitaji matumiz ya 5G....
5G is the fifth generation of wireless technology. But users will know it as one of the fastest, most robust technologies the world has ever seen.
That means quicker downloads, much lower lag and a significant impact on how we live, work and play. The connectivity benefits of 5G are expected to make businesses more efficient and give consumers access to more information faster than ever before.
1. Connected cars,
2. smart communities,
3. industrial IoT,
4. immersive education—they all will rely on 5G networks.
Na Prisca Ulomi, WMTH
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake.
Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa.
“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya
Naagiza Huyu jamaa apewe kazi pale B.O.T kitengo cha online, Kuna mzee pale hataki kufungulia PAY PAL ifanye kazi Tanzania.