Tanzania kuendelea na Mkataba wa Adani wa Dola Milioni 95 kuendesha Gati za Bandari ya Dar Licha ya Tuhuma za Rushwa

Tanzania kuendelea na Mkataba wa Adani wa Dola Milioni 95 kuendesha Gati za Bandari ya Dar Licha ya Tuhuma za Rushwa

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
1732776198851.png

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuheshimu mikataba yake na kampuni tanzu ya Adani Group licha ya mashtaka mapya dhidi ya Gautam Adani, mwenyekiti bilionea wa kundi hilo, anayekabiliwa na tuhuma za utoaji hongo na udanganyifu, afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Bandari amethibitisha.

Wiki iliyopita, Adani na mpwa wake walikabiliwa na mashtaka ya udanganyifu na hati za kukamatwa zilitolewa dhidi yao, wakituhumiwa kupanga njama ya dola milioni 265 kuwahonga maafisa wa India ili kupata mikataba ya usambazaji wa umeme. Hata hivyo, Adani Group imekana tuhuma hizo.

Mwezi Mei, Tanzania ilisaini mkataba wa miaka 30 na Adani Ports, kampuni tanzu ya Adani Group, kuendesha Gati ya Makontena 2 katika Bandari ya Dar es Salaam. Mkataba huo pia ulijumuisha ununuzi wa asilimia 95 ya hisa za Kampuni ya Huduma za Gati za Makontena za Kimataifa ya Tanzania (TICTS) kwa dola milioni 95.

"Hatujakuwa na matatizo na mtu yeyote. Shughuli zetu zote zinafanywa kwa mujibu wa sheria na makubaliano yetu," alisema Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, alipoongea na Reuters Jumanne. Alisisitiza kuwa Tanzania haikabiliwi na madai yoyote ya udanganyifu kuhusu mikataba yake. "Kama kuna watu wengine wanachukua hatua, basi wanachukua kwa sababu zao."

Wakati huohuo, nchini Kenya jirani, Rais William Ruto hivi karibuni alifuta mkataba wa Adani wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme. Pia alikataa mapendekezo ya kuongeza barabara ya pili ya ndege na kuboresha kituo cha abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, mpango ambao ungehusisha mkataba wa upangaji wa miaka 30.

PIA SOMA
- Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani
 
Ukiiangalia hii comment ni kama ina nia njema, ila kiuhalisia ni ya kishenzi sana na ya kurudisha maendeleo ya taifa nyuma. Na bila shaka wewe uliyeandika comment hii upo kwenye system
Kupanga ni kuchagua. Huitaji kuwa kwenye system kung'amua yanayoendelea duniani, nchi yetu ikiwemo ndani....

Kenya wameenda na "guilty until proven innocent "...contrary to our stand.. hii ya wakenya nayo ina ubaya wake.

Mfano ukijikuta upo mikononi mwa wananchi wenye hasira kali, bila wao kujua umemfumania demu wako yupo ghetto kwake kakugeuzia kibao akakuitia nduru za mwizi mpaka ukweli unafahamika ushalamba mavumbi kitambo sana... RIP Mandojo.
 
Kupanga ni kuchagua. Huitaji kuwa kwenye system kung'amua yanayoendelea duniani, nchi yetu ikiwemo ndani.... Kenya wameenda na "guilty until proven innocent "...contrary to our stand.. hii ya wakenya nayo ina ubaya wake. Mfano ukijikuta upo mikononi mwa wananchi wenye hasira kali, bila wao kujua umemfumania demu wako yupo ghetto kwake kakugeuzia kibao akakuitia nduru za mwizi...mpaka ukweli unafahamika ushalamba mavumbi kitambo sana... RIP Mandojo.
Ngoja tuone
 
tuko vizuriiii mazeee....kanjibai kalamba dumeee
 
Yaaani

Kwamba

Tanzania inapanga kuheshimu mikataba yake na kitengo cha Adani Group licha ya shtaka la Marekani dhidi ya mwenyekiti wake bilionea Gautam Adani kwa tuhuma za hongo na udanganyifu, afisa mwandamizi wa mamlaka ya bandari alisema.

Adani alishtakiwa kwa udanganyifu wiki iliyopita, na hati za kukamatwa zilitolewa dhidi yake na mpwa wake kwa madai ya kuhusika katika mpango wa dola milioni 265 wa kuhonga maafisa wa India ili kupata mikataba ya usambazaji wa umeme. Adani Group imekanusha tuhuma hizo.

Tanzania plans to honour its contracts with an Adani Group unit despite a US indictment of its billionaire chairman Gautam Adani on accusations of bribery and fraud, a senior official at the ports authority said.

Adani was indicted for fraud last week and arrest warrants were issued for him and his nephew for their alleged roles in a $265 million scheme to bribe Indian officials to secure power-supply deals. Adani Group has denied the accusations.

READ: thecitizen.co.tz/tanzania/busi

PIA SOMA
- Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani
 

Attachments

  • 20241127_203114.jpg
    20241127_203114.jpg
    102.6 KB · Views: 6
Tajiri wa Kihindi aitwaye Gautam Adani anatia shaka kila aendako tokana na kukosa uaminifu kibiashara kimataifa na namna alivypta utajir wake kwa kumtumia waziri mkuu wa India Narendra Modi.

Kenya wamemtimua baada ya Marekani kuwatonya. Je ni kweli Tanzania tumeendelea kumkumbatia na kupuuza maonyo ya wenzetu?

Nadhani ni kwa sababu rais wetu mbeba maone kipenzi na chaguo la Mungu ana huruma. Je ni kweli au kuna ka rushwa?
 

Tanzania kuheshimu na kuyazingatia makubaliano na Adani kwa kituo cha kontena bandarini, afisa anasema​

5:01 | 27 Nov 2024
0 Maoni Chapisha Shiriki
Adanil.r

FILE - Nembo ya Kikundi cha Adani inaonekana kwenye uso wa mbele wa Jumba lake la Biashara nje kidogo ya Ahmedabad, India, Novemba 22, 2024. [Picha ya faili: Reuters/Amit Dave]

Tanzania inapanga kuheshimu kandarasi zake na kitengo cha Adani Group licha ya Marekani kumfungulia mashitaka mwenyekiti wake bilionea Gautam Adani kwa tuhuma za hongo na ulaghai, afisa mkuu katika mamlaka ya bandari alisema.


Adani alishtakiwa kwa ulaghai wiki iliyopita na vibali vya kukamatwa vilitolewa kwa ajili yake na mpwa wake kwa madai ya majukumu yao katika mpango wa dola milioni 265 kuwahonga maafisa wa India ili kupata mikataba ya usambazaji wa umeme. Adani Group imekanusha tuhuma hizo.

Mwezi Mei, Tanzania iliingia katika makubaliano ya mkataba wa miaka 30 na Adani Ports, kitengo cha Adani Group, kuendesha kituo cha kontena katika bandari yake ya Dar es Salaam, kinachojulikana kama Container Terminal 2.


Kampuni ya Adani Ports pia ilifikia makubaliano ya ununuzi wa hisa kwa asilimia 95 ya hisa katika kampuni ya kimataifa ya Tanzania International Container Terminal Services TICTS kwa dola milioni 95.

“Hatuna matatizo na mtu yeyote. Kila kitu tunachofanya ni kwa mujibu wa sheria na makubaliano yetu,” Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Plasduce Mbossa aliiambia Reuters siku ya Jumanne alipoulizwa kuhusu hali ya kandarasi hizo.


“Kwa mikataba tuliyonayo, hatuna madai hayo (ya makosa). Ikiwa kuna watu wengine wanachukua hatua, basi wanafanya kulingana na sababu zao.


Wiki iliyopita katika nchi jirani ya Kenya, Rais William Ruto alifutilia mbali mkataba uliotiwa saini na kitengo cha Adani kujenga njia za kusambaza umeme.


Pia alighairi pendekezo la kuongeza njia ya pili ya ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA na kuboresha kituo cha abiria badala ya kukodisha kwa miaka 30.
Chanzo: Reuters
 
IMG-20241128-WA0057.jpg

=
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Bandari nchini Tanzania Bw. Plasduce Mbossa ameliambia The Citizens kuwa TANZANIA inaendelea na mkataba wake wa uendeshaji wa bandari na Kampuni ya Adani Group kupitia Gati No2.

Mtakumbuka Tanzania na Adani Groups wamesaini mkataba wa zaidi ya $95milioni karibu sawa na zaidi ya TZS 247bn wa kuendesha Gate namba 2 utakaodumu kwa miaka 30.

Wakati haya yanaendelea kwa upande wake Bw. Davidi Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPP yeye ameendelea kuwa kimya juu ya ama ataendelea na mpango wake wa awali wa kumpata mbia katika Ujenzi wa msongo wa Umeme pamoja na Uendeshaji wa Viwanja vya ndege kwa sharti la PPP kwa kupitia watia nia waliopo au laa.

Wakati huu ambapo Adani Green Energy Ltd pamoja na kampuni ya Uingereza ya Gridworks Development Partners LLP zimeonesha nia hiyo ambazo ndizo kampuni pekee za kigeni zilizoonesha nia ya kuwekeza katika miradi hiyo na kwa kuzingatia tuhuma za sasa za rushwa na Ulaghai dhidi ya billionaire Adani Gautam.

 
Back
Top Bottom