Tanzania kufanya msako dawa nne zilizozuiliwa na WHO

Tanzania kufanya msako dawa nne zilizozuiliwa na WHO

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Serikali ya Tanzania imesema, inafanya ukaguzi maalumu ili kubaini iwapo aina nne ya dawa zilizopigwa marufuku na Shirika la Afya Duniani (WHO), zimeingia katika mzunguko nchini humo.

Jana Jumatano, Oktoba 5, 2022, WHO ilizitangaza dawa hizo kutoka India kuwa ni hatari na zimesababisha vifo kwa watoto 66 nchini Gambia wakizitaka ziondolewe sokoni.

Kwa mujibu wa WHO, dawa hizo ni aina ya Promethazine Oral Solution, Kofexmalin Baby Cough Syrup, Major Baby Cough Syrup na Magrip N Cold Syrup kutoka nchini India ni hatari na zimesababisha vifo kwa watoto 66 nchini Gambia.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Oktoba 6, 2022 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale wakati akitoa ufafanuzi alipoulizwa iwapo dawa hizo zinapatikana nchini.

“Kuna dharura imetolewa na WHO baada ya dawa hizi kubainika huko Gambia na zinatengenezwa na kiwanda cha Maiden Pharmaceutical ltd cha India. Kwa upande wetu hapa nchini wenye mamlaka ya kusajili dawa vifaa tiba TMDA wamenihakikishia kwamba dawa hizi hazipo nchini.

“Aidha Serikali kupitia Wizara ya Afya tutafanya ukaguzi maalumu ili kubaini kama kuna sampuli mojawapo imeingia kwenye mzunguko,” amesema.

Meneja wa kitengo cha mawasiliano TMDA, Gaudensia Simwanza amesema, "dawa hizi hazijawahi kusajiliwa nchini na hazipo. Tunaandaa taarifa kwa umma."

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom