Tanzania kuilipa Indiana Resources Ltd Bilioni 237 baada ya kuvunja mkataba mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

Tanzania kuilipa Indiana Resources Ltd Bilioni 237 baada ya kuvunja mkataba mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take: Kama Nchi ingesubiria na kutangaza kwamba haitaongeza mda wa leseni by 2020 basi mradi hodhi ungerejea Serikalini bila kulipa fidia yeyote.

Akili ni nywele kama huna wenya nazo wataendelea kutunyoa Kwa msumeno.Pia soma Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

---
Tanzania Yakubali Kulipa Bilioni 237 ya Fidia Kwa Kuvunja Mkataba Mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

Tanzania na kampuni ya uchimbaji madini kutoka Australia, Indiana Resource Limited zimefikia makubaliano ya fidia ambapo Tanzania itailipa kampuni hiyo dola za kimarekani milioni 90 kutokana na kuvunja makubaliano katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill uliopo mkoani Lindi. Tanzania imeshatanguliza malipo ya awamu ya kwanza ya dola milioni 35 sawa na bilioni 92.

Pia soma: Indiana waitaka Tanzania ilipe Tsh. Bilioni 277 kabla ya Agost 17, 2023

Haya yameelezwa leo Julai 29,2024 katika taarifa iliyotolewa na kampuni ya Indiana Resouces ambayo inaeleza kuwa kampuni hiyo imekubali kupokea ofa ya Tanzania ya dola milioni 90 sawa na bilioni 237, kiwango ambacho ni kidogo kuliko kile cha awali ambacho Tanzania kiliamriwa kulipa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID).

Mnamo Julai 14, 2023, Tanzania ilitakiwa kuilipa kampuni ya Indiana Resources Ltd, dola milioni 109 ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 250 baada ya kituo hicho kujiridhisha uwepo wa ukiukwaji wa mkataba wa uwekezaji katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa imeamua kukubali kiwango hicho kupunguza mzigo wa gharama utakaotokana na kuendelea na ubishano katika vyombo mbalimbali vya kisheria. Katika makubaliano hayo Tanzania itatakiwa kumalizia kiwango kilichobaki kwa awamu mbili, ambapo mpaka Oktoba 24 itatakiwa kulipa dola milioni 25 na ifikapo Machi 30,2025, itatakiwa kulipa dola milioni 30.

Changamoto kati ya Indiana Resources na Tanzania ilitokana na mabadiliko ya sheria za madini Tanzania mwaka 2017 na 2018. Mnamo Januari 10, 2018, Serikali ya Tanzania, kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 01 la mwaka 2018, ilitangaza Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018, ambazo zilifuta leseni hodhi zilizokwisha tolewa kisheria.

Pia soma: Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

Aidha, Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018 zilienda mbele zaidi, chini ya kanuni ya 21(2) kwa kueleza kuwa haki zote za madini zilizokuwa zikihodhiwa na wamiliki wa leseni hodhi kwenye maeneo yote yaliyokuwa chini ya leseni hodhi, zitakuwa haki za Serikali ya Tanzania.

Hii iliathiri kampuni ya Indiana Resources iliyokuwa na leseni hodhi katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill ,mradi uliokadiriwa na kampuni hiyo kuwa unaweza kupata madini yenye thamani ya dola milioni 217. Leseni hiyo iliyofutwa ilikuwa inategemewa kuisha muda wake mnamo Aprili 2020.

Leseni hodhi ni zile leseni ambazo zinaruhusu kampuni husika kushikilia maeneo kwa kipindi cha leseni bila kufanya chochote ikiwa wana vikwazo vya kiufundi, au hali ya uchumi kutoruhusu.

Msukumo mkubwa wa Tanzania kufuta leseni hodhi ni kile kilichoonekana kuwa ni mfumo wa kinyonyaji ambapo kampuni huweza kushikilia maeneo bila kuyaendeleza huku wakijinufaisha kwa kuweka kama mali katika vitabu vyao ilhali Tanzania ikiwa hainufaiki chochote.

Hata hivyo, kutokufuata taratibu na sheria ilizoziweka kumeweza kuigharimu Tanzania na kujikuta ikifuguliwa mashauri mbalimbali duniani juu ya maamuzi yake katika miaka hiyo.

Nakala imeambatishwa hapa nchini
 
Attachments

Kuna mtu alikuwa bogus sana lakini kuna mazezeta eti ndiyo wanamsifia!
Kuna Kiongozi Kijana wa Burkina Faso, ukisogea mpaka Mali, Niger wao Kwa Sasa wanavunja mikataba ya kinyonyaji ya mabeberu.

Kuanza Upya sio Ujinga... Madini hayaozi, Kulipa Billion hizo, lkn Madini yakabaki salama, na yakachimbwa Kwa Mkataba wenye Masilahi na Nchi, kipi Bora??.

Kama huna GPA ya kuanzia walau 3.5 Chuo Kikuu, huwezi kunielewa.
 
Kama hayo madini yalivunwa kwa miaka mingi kulikuwa kuna ugumu gani kusubiri miaka miwili iliyobaki kumaliza mkataba kuliko kulipa hayo mabilioni bure tu,halafu unaleta story za viongozi wa Burkina Faso na Mali kwani wao ni malaika?
Kwa taarifa yako viongozi wa Kiafrika wote ni majizi tu wanachokifanya ni kuvuruga yale ya wenzao waliopita na kutengeneza michongo yao.
 
Mkuu hizi GPA harafu unalala na Jiko la gesi hakuna maana zinakua za kutafutia mademu bar ila ulichoongea kama upo sahihi..
 
Kuna Kiongozi Kijana wa Burkina Faso, ukisogea mpaka Mali, Niger wao Kwa Sasa wanavunja mikataba ya kinyonyaji ya mabeberu.

Kuanza Upya sio Ujinga... Madini hayaozi, Kulipa Billion hizo, lkn Madini yakabaki salama, na yakachimbwa Kwa Mkataba wenye Masilahi na Nchi, kipi Bora??.

Kama huna GPA ya kuanzia walau 3.5 Chuo Kikuu, huwezi kunielewa.
Wanakurupuka au? 😂😂
 
Kama hayo madini yalivunwa kwa miaka mingi kulikuwa kuna ugumu gani kusubiri miaka miwili iliyobaki kumaliza mkataba kuliko kulipa hayo mabilioni bure tu,halafu unaleta story za viongozi wa Burkina Faso na Mali kwani wao ni malaika?
Kwa taarifa yako viongozi wa Kiafrika wote ni majizi tu wanachokifanya ni kuvuruga yale ya wenzao waliopita na kutengeneza michongo yao.
Hakuna miaka Mingi iliyovunwa,ilikuwa stage ya awali ya Utafiti na tayari Mkandarasi alikuwa ameweka pesa,ulitegemea awachekee?
 
Back
Top Bottom