Tanzania kuilipa Indiana Resources Ltd Bilioni 237 baada ya kuvunja mkataba mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

Kuna mtu alikuwa bogus sana lakini kuna mazezeta eti ndiyo wanamsifia!
Wewe ndio mjinga tena haswa ji bora nusu hasara kuliko hasara kamili..
Sekta ya madini baada ya kufanyiwa marekebisho ya sheria mbalimbali sasa inaingizia nchi trillion sio cuini ya 3 kwa mwaka...bora kulipa hizo fidia maana sasa tunafaidika sana kuliko tulivyokuwa tunanyonywa huko nyuma..
 
Kuna Kiongozi Kijana wa Burkina Faso, ukisogea mpaka Mali, Niger wao Kwa Sasa wanavunja mikataba ya kinyonyaji ya mabeberu.

Kuanza Upya sio Ujinga... Madini hayaozi, Kulipa Billion hizo, lkn Madini yakabaki salama, na yakachimbwa Kwa Mkataba wenye Masilahi na Nchi, kipi Bora??.

Kama huna GPA ya kuanzia walau 3.5 Chuo Kikuu, huwezi kunielewa.
Aliyesaini hii mikataba ni nani?
 
My Take: Kama Nchi ingesubiria na kutangaza kwamba haitaongeza mda wa leseni by 2020 basi mradi hodhi ungerejea Serikalini bila kulipa fidia yeyote.

Akili ni nywele kama huna wenya nazo wataendelea kutunyoa Kwa msumeno👇👇

---
Tanzania Yakubali Kulipa Bilioni 237 ya Fidia Kwa Kuvunja Mkataba Mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

Tanzania na kampuni ya uchimbaji madini kutoka Australia, Indiana Resource Limited zimefikia makubaliano ya fidia ambapo Tanzania itailipa kampuni hiyo dola za kimarekani milioni 90 kutokana na kuvunja makubaliano katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill uliopo mkoani Lindi. Tanzania imeshatanguliza malipo ya awamu ya kwanza ya dola milioni 35 sawa na bilioni 92.

Pia soma: Indiana waitaka Tanzania ilipe Tsh. Bilioni 277 kabla ya Agost 17, 2023

Haya yameelezwa leo Julai 29,2024 katika taarifa iliyotolewa na kampuni ya Indiana Resouces ambayo inaeleza kuwa kampuni hiyo imekubali kupokea ofa ya Tanzania ya dola milioni 90 sawa na bilioni 237, kiwango ambacho ni kidogo kuliko kile cha awali ambacho Tanzania kiliamriwa kulipa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID).

Mnamo Julai 14, 2023, Tanzania ilitakiwa kuilipa kampuni ya Indiana Resources Ltd, dola milioni 109 ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 250 baada ya kituo hicho kujiridhisha uwepo wa ukiukwaji wa mkataba wa uwekezaji katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa imeamua kukubali kiwango hicho kupunguza mzigo wa gharama utakaotokana na kuendelea na ubishano katika vyombo mbalimbali vya kisheria. Katika makubaliano hayo Tanzania itatakiwa kumalizia kiwango kilichobaki kwa awamu mbili, ambapo mpaka Oktoba 24 itatakiwa kulipa dola milioni 25 na ifikapo Machi 30,2025, itatakiwa kulipa dola milioni 30.

Changamoto kati ya Indiana Resources na Tanzania ilitokana na mabadiliko ya sheria za madini Tanzania mwaka 2017 na 2018. Mnamo Januari 10, 2018, Serikali ya Tanzania, kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 01 la mwaka 2018, ilitangaza Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018, ambazo zilifuta leseni hodhi zilizokwisha tolewa kisheria.

Pia soma: Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

Aidha, Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018 zilienda mbele zaidi, chini ya kanuni ya 21(2) kwa kueleza kuwa haki zote za madini zilizokuwa zikihodhiwa na wamiliki wa leseni hodhi kwenye maeneo yote yaliyokuwa chini ya leseni hodhi, zitakuwa haki za Serikali ya Tanzania.

Hii iliathiri kampuni ya Indiana Resources iliyokuwa na leseni hodhi katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill ,mradi uliokadiriwa na kampuni hiyo kuwa unaweza kupata madini yenye thamani ya dola milioni 217. Leseni hiyo iliyofutwa ilikuwa inategemewa kuisha muda wake mnamo Aprili 2020.

Leseni hodhi ni zile leseni ambazo zinaruhusu kampuni husika kushikilia maeneo kwa kipindi cha leseni bila kufanya chochote ikiwa wana vikwazo vya kiufundi, au hali ya uchumi kutoruhusu.

Msukumo mkubwa wa Tanzania kufuta leseni hodhi ni kile kilichoonekana kuwa ni mfumo wa kinyonyaji ambapo kampuni huweza kushikilia maeneo bila kuyaendeleza huku wakijinufaisha kwa kuweka kama mali katika vitabu vyao ilhali Tanzania ikiwa hainufaiki chochote.

Hata hivyo, kutokufuata taratibu na sheria ilizoziweka kumeweza kuigharimu Tanzania na kujikuta ikifuguliwa mashauri mbalimbali duniani juu ya maamuzi yake katika miaka hiyo.

Nakala imeambatishwa hapa nchini

Tatizo la Tanzania ni tabia ya kusamehe samehe wezi. Walio ingia mkataba walijua kabisa sio mzuri lakini hawajali leo wapo tu wakati mabilioni yana liwa na kulipwa wakati watu hawana maji🤔
 
Ta
Hao wote ni ccm kwa hiyo solution ni ccm iondoke
Tizo sio CCM tatizo ni hao wezi.

Kaangalie CCM kwenye karatasi u uniambie.

Watu ndio wabaya.

Mimi naamini tukiisimamia CCM ipasavyo tunatoboa.

Sera za CCM ziliikomboa Afrika seuse hapa bongo tu???
 
Amini usiamini! Huo mzigo nusu wanalipwa vigogo wa hapa hapa Tz
Huo ndio ukweli, maana hiyo mikataba wameingia viongozi wetu. Cha ajabu Magufiluli alipora uchaguzi akaweka wabunge wote wa ccm lakini hawawezi kuhoji huu uhuni.
 
Wewe ndio mjinga tena haswa ji bora nusu hasara kuliko hasara kamili..
Sekta ya madini baada ya kufanyiwa marekebisho ya sheria mbalimbali sasa inaingizia nchi trillion sio cuini ya 3 kwa mwaka...bora kulipa hizo fidia maana sasa tunafaidika sana kuliko tulivyokuwa tunanyonywa huko nyuma..
Kumbe maboga mpo wengi ngoja tuyachemshe tuyale.
 
Kuna Kiongozi Kijana wa Burkina Faso, ukisogea mpaka Mali, Niger wao Kwa Sasa wanavunja mikataba ya kinyonyaji ya mabeberu.

Kuanza Upya sio Ujinga... Madini hayaozi, Kulipa Billion hizo, lkn Madini yakabaki salama, na yakachimbwa Kwa Mkataba wenye Masilahi na Nchi, kipi Bora??.

Kama huna GPA ya kuanzia walau 3.5 Chuo Kikuu, huwezi kunielewa.
G.P.A sio hoja.
 
Wanasheria wa serikali kesi wanazoshindaga ni zile za kukamatwa machangudoa na wafuasi wa chadema tu zaidi ya hapo huwa hawatoboi.
 
Ta

Tizo sio CCM tatizo ni hao wezi.

Kaangalie CCM kwenye karatasi u uniambie.

Watu ndio wabaya.

Mimi naamini tukiisimamia CCM ipasavyo tunatoboa.

Sera za CCM ziliikomboa Afrika seuse hapa bongo tu???
Bahati nzuri kwa sasa umeshakiri wanaccm ni wabaya, hatua kwa hatua tu kuna siku utakubali ccm ni janga la taifa.
 
My Take: Kama Nchi ingesubiria na kutangaza kwamba haitaongeza mda wa leseni by 2020 basi mradi hodhi ungerejea Serikalini bila kulipa fidia yeyote.

Akili ni nywele kama huna wenya nazo wataendelea kutunyoa Kwa msumeno.Pia soma Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

---
Tanzania Yakubali Kulipa Bilioni 237 ya Fidia Kwa Kuvunja Mkataba Mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92

Tanzania na kampuni ya uchimbaji madini kutoka Australia, Indiana Resource Limited zimefikia makubaliano ya fidia ambapo Tanzania itailipa kampuni hiyo dola za kimarekani milioni 90 kutokana na kuvunja makubaliano katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill uliopo mkoani Lindi. Tanzania imeshatanguliza malipo ya awamu ya kwanza ya dola milioni 35 sawa na bilioni 92.

Pia soma: Indiana waitaka Tanzania ilipe Tsh. Bilioni 277 kabla ya Agost 17, 2023

Haya yameelezwa leo Julai 29,2024 katika taarifa iliyotolewa na kampuni ya Indiana Resouces ambayo inaeleza kuwa kampuni hiyo imekubali kupokea ofa ya Tanzania ya dola milioni 90 sawa na bilioni 237, kiwango ambacho ni kidogo kuliko kile cha awali ambacho Tanzania kiliamriwa kulipa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID).

Mnamo Julai 14, 2023, Tanzania ilitakiwa kuilipa kampuni ya Indiana Resources Ltd, dola milioni 109 ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 250 baada ya kituo hicho kujiridhisha uwepo wa ukiukwaji wa mkataba wa uwekezaji katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa imeamua kukubali kiwango hicho kupunguza mzigo wa gharama utakaotokana na kuendelea na ubishano katika vyombo mbalimbali vya kisheria. Katika makubaliano hayo Tanzania itatakiwa kumalizia kiwango kilichobaki kwa awamu mbili, ambapo mpaka Oktoba 24 itatakiwa kulipa dola milioni 25 na ifikapo Machi 30,2025, itatakiwa kulipa dola milioni 30.

Changamoto kati ya Indiana Resources na Tanzania ilitokana na mabadiliko ya sheria za madini Tanzania mwaka 2017 na 2018. Mnamo Januari 10, 2018, Serikali ya Tanzania, kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 01 la mwaka 2018, ilitangaza Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018, ambazo zilifuta leseni hodhi zilizokwisha tolewa kisheria.

Pia soma: Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

Aidha, Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018 zilienda mbele zaidi, chini ya kanuni ya 21(2) kwa kueleza kuwa haki zote za madini zilizokuwa zikihodhiwa na wamiliki wa leseni hodhi kwenye maeneo yote yaliyokuwa chini ya leseni hodhi, zitakuwa haki za Serikali ya Tanzania.

Hii iliathiri kampuni ya Indiana Resources iliyokuwa na leseni hodhi katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill ,mradi uliokadiriwa na kampuni hiyo kuwa unaweza kupata madini yenye thamani ya dola milioni 217. Leseni hiyo iliyofutwa ilikuwa inategemewa kuisha muda wake mnamo Aprili 2020.

Leseni hodhi ni zile leseni ambazo zinaruhusu kampuni husika kushikilia maeneo kwa kipindi cha leseni bila kufanya chochote ikiwa wana vikwazo vya kiufundi, au hali ya uchumi kutoruhusu.

Msukumo mkubwa wa Tanzania kufuta leseni hodhi ni kile kilichoonekana kuwa ni mfumo wa kinyonyaji ambapo kampuni huweza kushikilia maeneo bila kuyaendeleza huku wakijinufaisha kwa kuweka kama mali katika vitabu vyao ilhali Tanzania ikiwa hainufaiki chochote.

Hata hivyo, kutokufuata taratibu na sheria ilizoziweka kumeweza kuigharimu Tanzania na kujikuta ikifuguliwa mashauri mbalimbali duniani juu ya maamuzi yake katika miaka hiyo.

Nakala imeambatishwa hapa nchini
Matokeo ya kutokufuata Sheria zilizopo na kutenda kwa mihemko, tocha hiyo
 
Back
Top Bottom