Chief Sanze
JF-Expert Member
- Jun 13, 2014
- 1,668
- 3,736
Kwani serikali ingekosa chochote sema mungu wenu alikuwa bwege tu na roho mbaya.Hujui kitu wewe. Kwahiyo unataka kusema wangechimba nickel wangepata kama hiyo? Ten million us dollars?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani serikali ingekosa chochote sema mungu wenu alikuwa bwege tu na roho mbaya.Hujui kitu wewe. Kwahiyo unataka kusema wangechimba nickel wangepata kama hiyo? Ten million us dollars?
Hivi bado upo kwenye D tu?B na A amechukua nani?Bogus. ni wewe ambaye unakubali kupelekeshwa hata nyumbani kwako. Maamuzi ya Serikali ya Mwamba Magufuli yalikuwa sahihi kabisa. Sasa hivi hakuna kampuni ina kuja na kuingia mikataba ya ovyo ovyo. Wao wamepata kidogo na hasara kidogo na Tanzania imepata hasara kidogo na faida kwa maana bado madini tunayo!
Hayo ndio maamuzi ya wenye akili! Wenye D moja mtaelewa wapi!!
Let us stick to a scholarly argument ingawa najua huwezi kitu kama hicho!Kwani serikali ingekosa chochote sema mungu wenu alikuwa bwege tu na roho mbaya.
Kuna mtu alikuwa bogus sana lakini kuna mazezeta eti ndiyo wanamsifia!
Huyo mnayemsifia alikuwa akiona kutumia miguvu ndiyo kila kitu.Let us stick to a scholarly argument ingawa najua huwezi kitu kama hicho!
Bogus. ni wewe ambaye unakubali kupelekeshwa hata nyumbani kwako. Maamuzi ya Serikali ya Mwamba Magufuli yalikuwa sahihi kabisa. Sasa hivi hakuna kampuni ina kuja na kuingia mikataba ya ovyo ovyo. Wao wamepata kidogo na hasara kidogo na Tanzania imepata hasara kidogo na faida kwa maana bado madini tunayo!
Hayo ndio maamuzi ya wenye akili! Wenye D moja mtaelewa wapi!!
Wala hakuwa hivyo bali alikuwa zigo la mavi.Jiwe alikuwa mzigo wa chuma na miba kwa watanzania.
Nchi zote duniani zilipata Maendeleo kwakiwa na viongozi "shrewd" kama Mwamba Magufuli! Soma historia ya Rais Lee Kuan Yew wa Singapore kwenye kitabu chake cha "One Man Army" utaelewa Mwamba Magufuli alimaanisha nini...hasara hii ilikuwa inaepukika.
..Magufuli alipaswa kusubiri leseni ya hiyo kampuni iishe halafu asikubali ku-renew.
..pia kulikuwa na option ya kuwashitaki ktk ICSD kama alikuwa na ushahidi kuwa wamekiuka mkataba.
..tatizo la Magufuli ni kushughulika na makampuni ya kimataifa kana kwamba anashughulikia wapinzani wake hapa nchini. Matokeo yake ndiyo haya mabilioni ya hasara tunayolazimika kuyalipa.
Kiongozi gani duniani hatumii nguvu? Au utofauti wao wa namna Gani ya kuzitumia hizo nguvu ndio kunakuchanganya!?Huyo mnayemsifia alikuwa akiona kutumia miguvu ndiyo kila kitu.
😂😂😂Mungu wenu kila kitu alimkabidhi Mr.Slim,kuanzia bandari,mirerani yote alimkabidhi na ndiyo alikuwa mwalimu wake jinsi ya kupoteza watu wanaopingana naye,unajifanya hujui!
Huyu wa sasa hakuna kilichobakia.Mtu mmoja kaliacha taifa na hasara ya mamia ya matrilioni, ni hasara ambayo hailingani hata na gharama ambazo Tanzania ilitumia kwa vita vya Kagera.
Nchi inaendelea kuomboleza maamuzi yaliyokuwa yanafanywa na awamu ya tano kwa kivuli cha uzalendo. Waliokuwa wanaonya maamuzi ya hovyo hovyo walishambuliwa. Sasa tuko hapa.
View attachment 3056168
Nchi zote duniani zilipata Maendeleo kwakiwa na viongozi "shrewd" kama Mwamba Magufuli! Soma historia ya Rais Lee Kuan Yew wa Singapore kwenye kitabu chake cha "One Man Army" utaelewa Mwamba Magufuli alimaanisha nini.
Hatari sana 🙌Ila hii nchi watu wanajipigia tu🙆
Nyie UWT ndiyo mnaongoza nchi tangu 1960, huwa mnamlaumu nani?Thibitisha kama hizo ni kampuni za watu wa ndani.
Pili kwani kampuni za ndani ndio zinatakiwa zipate hasara Kwa sababu ya maamuzi yenu mabovu?
CCM ni zaidi ya shetani kabisaHivyo hivyo kama ile Richmond tuliambiwa kampuni ya Marekani kumbe ni kijana wa kiasia aliyekuwa na kiofisi cha kupigia simu za kimataifa kupitia Internet pale nyuma ya Key’s Hotel mnazi mmoja.
Jamaa alikuwa anakusanya mia tano tano kwa ajili ya simu na pia wanaojifunza kompyuta 😂🙄😳
Ghafla eti akawa ni mmarekani mwenye Richmond LLC 🤣😱
Bunge lote liliwekwa na Magufuli akisema ni wazalendo. Wahoji tuone uzalendo wao.I smell something....huu ni upigaji..anyway...wacha tuwalipe..fedha zitaisha na madini yatabaki..
Tundu Lissu aliwaambia mkambeza sasa kiko wapi?My Take: Kama Nchi ingesubiria na kutangaza kwamba haitaongeza mda wa leseni by 2020 basi mradi hodhi ungerejea Serikalini bila kulipa fidia yeyote.
Akili ni nywele kama huna wenya nazo wataendelea kutunyoa Kwa msumeno👇👇
---
Tanzania Yakubali Kulipa Bilioni 237 ya Fidia Kwa Kuvunja Mkataba Mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92
Tanzania na kampuni ya uchimbaji madini kutoka Australia, Indiana Resource Limited zimefikia makubaliano ya fidia ambapo Tanzania itailipa kampuni hiyo dola za kimarekani milioni 90 kutokana na kuvunja makubaliano katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill uliopo mkoani Lindi. Tanzania imeshatanguliza malipo ya awamu ya kwanza ya dola milioni 35 sawa na bilioni 92.
Pia soma: Indiana waitaka Tanzania ilipe Tsh. Bilioni 277 kabla ya Agost 17, 2023
Haya yameelezwa leo Julai 29,2024 katika taarifa iliyotolewa na kampuni ya Indiana Resouces ambayo inaeleza kuwa kampuni hiyo imekubali kupokea ofa ya Tanzania ya dola milioni 90 sawa na bilioni 237, kiwango ambacho ni kidogo kuliko kile cha awali ambacho Tanzania kiliamriwa kulipa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID).
Mnamo Julai 14, 2023, Tanzania ilitakiwa kuilipa kampuni ya Indiana Resources Ltd, dola milioni 109 ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 250 baada ya kituo hicho kujiridhisha uwepo wa ukiukwaji wa mkataba wa uwekezaji katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa imeamua kukubali kiwango hicho kupunguza mzigo wa gharama utakaotokana na kuendelea na ubishano katika vyombo mbalimbali vya kisheria. Katika makubaliano hayo Tanzania itatakiwa kumalizia kiwango kilichobaki kwa awamu mbili, ambapo mpaka Oktoba 24 itatakiwa kulipa dola milioni 25 na ifikapo Machi 30,2025, itatakiwa kulipa dola milioni 30.
Changamoto kati ya Indiana Resources na Tanzania ilitokana na mabadiliko ya sheria za madini Tanzania mwaka 2017 na 2018. Mnamo Januari 10, 2018, Serikali ya Tanzania, kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 01 la mwaka 2018, ilitangaza Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018, ambazo zilifuta leseni hodhi zilizokwisha tolewa kisheria.
Pia soma: Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba
Aidha, Kanuni za Haki za Madini za Mwaka 2018 zilienda mbele zaidi, chini ya kanuni ya 21(2) kwa kueleza kuwa haki zote za madini zilizokuwa zikihodhiwa na wamiliki wa leseni hodhi kwenye maeneo yote yaliyokuwa chini ya leseni hodhi, zitakuwa haki za Serikali ya Tanzania.
Hii iliathiri kampuni ya Indiana Resources iliyokuwa na leseni hodhi katika Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill ,mradi uliokadiriwa na kampuni hiyo kuwa unaweza kupata madini yenye thamani ya dola milioni 217. Leseni hiyo iliyofutwa ilikuwa inategemewa kuisha muda wake mnamo Aprili 2020.
Leseni hodhi ni zile leseni ambazo zinaruhusu kampuni husika kushikilia maeneo kwa kipindi cha leseni bila kufanya chochote ikiwa wana vikwazo vya kiufundi, au hali ya uchumi kutoruhusu.
Msukumo mkubwa wa Tanzania kufuta leseni hodhi ni kile kilichoonekana kuwa ni mfumo wa kinyonyaji ambapo kampuni huweza kushikilia maeneo bila kuyaendeleza huku wakijinufaisha kwa kuweka kama mali katika vitabu vyao ilhali Tanzania ikiwa hainufaiki chochote.
Hata hivyo, kutokufuata taratibu na sheria ilizoziweka kumeweza kuigharimu Tanzania na kujikuta ikifuguliwa mashauri mbalimbali duniani juu ya maamuzi yake katika miaka hiyo.
Nakala imeambatishwa hapa nchini