Wanabodi,
Uchumi unapimwa kwa vigezo vingi sana lakini vikubwa ni viwili ambayo Benki ya Dunia na IMF wanatumia navyo ni:
GNI(Gross national income) pamoja na GDP(Gross domestic product)
Kwa mujibu wa Taarifa ni kwamba GNI ya Tanzania imeongezeka na kufikia kwenye midhania ya viwango vya Benki ya Dunia ya uchumi wa kati.
GNI ni kitu endelevu
GNI au Gross national Income ni jumla ya mapato yote yanayoingia nchini au yaliyotengenezwa nchini na watu ambao ni Raia wa Tanzania au ambao sio Raia wa Tanzania
Mapato yanayoongelewa kwenye GNI ni kama ifuatavyo:
Haya mapato yanaongeza GNI na kuifanya kuwa kubwa hivyo kufanya Taifa la Tanzania kufikia uchumi wa kati
Foreign Aid au Misaada yote tunayopokea toka kwa wahisani toka nje. Hii misaada inaongezwa kwenye GNI na kuifanya ionekane GNI imeongezeka.
FD's (Foreign direct investment) huu ni uwekezaji wa moja kwa moja toka nje ,Thamani ya uwekazaji huu nayo inaongezwa kufanya GNI iwe kubwa
Pesa za Watanzania waishio nje au Makampuni ya Kitanzania yaliyo nje ya nchi ambazo pesa wanazituma moja kwa moja Tanzania. Hizi pesa nazo zinaongezwa kwenye GNI na kuifanya iwe kubwa.
Riba(Interest) pamoja na hisa ambazo nchi inapokea kwenye uwekezaji mbalimbali kwenye hati fungani za muda mfupi(bills) au hati za muda mrefu(Bonds). Hizi riba na hiza zinaongeza GNI na kuifanya iwe kubwa.
Mapato yafuatayo yanapunguzwa kwenye mahesabu ya GNI na kuifanya GNI kuwa ndogo au Yanaondolewa wakati wa mahesabu ya GNI.
Mapato yote ambayo wawekezaji wa kigeni waliopo Tanzania au Raia wa kigeni kipato wanachokipata Tanzania yanaondolewa kwenye kufanya mahesabu ya GNI.
GDP au Gross domestic product ni thamani ya bidhaa au huduma kwa bei ya soko kwa wakati huo. Hapa zinaongelewa thamani ya bidhaa au huduma zilizozalishwa kwa muda fulani mfano mwaka mmoja,Hizi ni bidhaa za ndani.
Kuna utofauti mwembamba sana kati ya GDP na GNI, GNI inachukua thamani na zile za nje
Benki ya dunia wanachofanya kupima uchumi ni kama ifuatavyo
GNI=GDP+ (Foreign aid,Foreign investment+interest+..............)
Je, GNI ya Tanzania imekua na kutufikisha uchumi wa kati?
Maswali yafuatayo ni muhimu kujua kama kweli tumefika uchumi wa kati
Je, uwekezaji toka nje umeongezeka Tanzania?
Je, mikopo na misaada imeongezeka Tanzania?
Je, uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani umeongezeka Tanzania?
Je, diaspora au watanzania toka nje wanaleta vipato nyumbani?
Katika awamu ya Tano ya JPM ni kweli kuna uwekazaji mkubwa sana kwenye SGR, barabara na sehemu kadhaa. Yote hayo yanaongeza GNI.
Kama Jibu ni ndiyo basi mambo mazuri.
Benki ya dunia wamegawa hivi vipato kwa madaraja matatu.
Low, Middle na High
Kuongezeka kwa GNI au kufika uchumi wa kati siyo kigezo kuwa maisha ya mtu mmoja mmoja yamekuwa mazuri au Nchi yetu siyo maskini.
Qatar ni moja ya nchi yenye GNI kubwa kutokana na visima vya mafuta au oil reserves.
Qatar kidogo GNI yao inafanana na Maisha ya Raia wake
Nchi kama kenya wao wapo uchumi wa kati siku nyingi lakini ni maskini wa kutupwa sana
Naomba tuendelee kujadili kwa lugha rahisi ili kuelimisha wengi juu na maana ya uchumi wa kati.
Nadharia za uchumi hasa GNI na GDP zina mapungufu yake mengi Sana. Mara nyingi nadharia hizi zinashindwa kuhusianisha ukuaji wa uchumi na Maisha ya mtu mmoja mmoja.
Wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia zaidi,Sisi wengine hatujasoma uchumi bali tunaelezea jinsi mambo yalivyo na yanavyofanyika World Benki na IMF
Watanzania wengi wanashangilia hasa wanasiasa sidhani kama wanaelewa maana halisi ya uchumi wa kati kwa hivi vipimo vya GNI vya Benki ya Dunia na IMF
Huu ni ushauri pia umetolewa na Mwana JF ambao nchi zao ziliingia matatizo kwa kufikia uchumi wa kati soma
Tanzania Chungeni mambo ya Eurobond