Kuhusu Tanzania Kuingia Uchumi wa Kati, Prof Ngowi Mchumi amefafanua vizuri Sana hata mm layman wa Uchumi nimeweza kuelewa. Mambo ya Msingi hapa Ni kwamba
1. Tunaposema tumeingia Uchumi wa Kati tunachukua Pato la WATANZANIA wote tunatafuta wastani. Maana yake Pato langu linajumlishwa na la kina Mo au Pato la msukuma toroli pale soko la Tandale linajumlishwa na Pato la kina Bakharesa halafu wanatafuta wastani. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo wastani wa Pato la kila mtanzania kwa Sasa linaanzia milioni mbili Hadi milioni nne.
2. Ukiingia Uchumi wa Kati maana yake unaanza kuachana na Misaada mfano tuna miradi mingi Sana tunayofadhiliwa Kama nchi kwenye Afya, Elimu nk hii tuanze kufikiria muda si mrefu haitafadhikiwa tena, Bajeti yako ya ndani kwa asilimia kubwa inatakiwa ibebwe na Pato la ndani, Mahali ambapo ulikuwa ukikopa wanakupa kwa riba ndogo Sasa riba itakuwa kubwa nk. Kwa maana ya Prof Ngowi ni kuwa mtoto kakua anapaswa kujitegemea Mwenyewe.
3. Wananchi waelimishwe wajiandae na mazingira ya Kuingia Uchumi wa Kati kuwa Ni kuzidisha kufanya kazi kwa bidii sio kupumzika, wengi wanaoshangilia wanadhani Ni muda wa kula Bata kumbe Ni kinyume chake kuwa ni wakati wa kupambana haswa kuelekea kujitegemea.
4. Kuna wanaosema World Bank imetutega kutuongoza Uchumi wa Kati ili wapate kutubagaza kwa kutunyima mikopo ya masharti nafuu na kukosa misaada kwa maana ya kutakiwa kujitegemea. Wenye nadharia hii wanadai kuwa nchi kama nchi ilikuwa haijafikia kuingia kwenye Uchumi wa Kati Bali ni Janja ya Mabeberu kutubagaza. Hili wewe unalionaje?
5. Kuna ambao wanafurahia kuwa nchi Sasa imepiga hatua kwa maana ya kuelekea kujitegemea. Hili wewe unalionaje? ....
Msikilize Prof Ngowi