Tanzania kuna kabila linaitwa Waarusha au ni Wamasai mmeamua kujiita hivyo?

Tanzania kuna kabila linaitwa Waarusha au ni Wamasai mmeamua kujiita hivyo?

Kimasai ni wame adopt tu ila ni makabila mawili tofauti kabisa ka ilivo wameru wanaongea kimachame ila si wachagga
ukiacha lugha, je unaweza kuwatofautisha vipi Waarusha na Wamaasai?
 
Waarusha,ni sub tribe ya Maasai ambapo kihistoria kabila lao lilitokana na wamasai walioasi mila na desturi za kimasai kwa kufanya baadhi ya mambo ambayo sio mafundisho wala mapokeo ya kimasai,na neno 'waarusa'kwa kimasai ni waliokengeuka kwa tafsri rahisi,...moja ya makengeuko ya enzi hizo ni kuooana na wanawake wa kibantu,......wanaishi pembezoni mwa jiji la Arusha ni viunga vyake..koo maarufu ni Laizer,mollel,na lukumay..
N:B..wana tabia za wivu,husda,ubinafi,kupenda kesi na kujiona wajanja pindi ukiingia kwenye kona zao.
 
Kimasai ni wame adopt tu ila ni makabila mawili tofauti kabisa ka ilivo wameru wanaongea kimachame ila si wachagga

Enhee tulia hapo hapo, hivi hawa wachagga linipokuja suala la kabila huwa wanajiandikisha kama wachagga…. au kila wao kivyao?

Yaani Mmarangu, Mmachame, Mrombo, Mkibosho etc…. kwa maana inasemekana kila wao na lugha yao!
 
Mbona katika list ya makabila 121 yanayo patikana Tanzania hili kabila halipo wakuu?

Na mbona wanaongea kimasai tu au na wenyewe wana lugha yao ya kiarusha?

Hao waarusha ni photocopy ya wamasaai. Kiarusha kinashabihiana sana na kimaasai, lakini ni lugha mbili tofauti.
 
Waarusha na Masai ni makabila mawili tofauti, waarusha ni wenyeji wa Arusha mjini, wao ndio wameuza maeneo yao ya maboma kwa wengine (wahamiaji) waliopo Arusha, ila nao wakati mwingine hujifunika mashuka kama wamasai.
Waarusha ni Wamasai wanaovaa Nguo, kujenga permanent houses, Kulala na wake zao chumba kimoja Hadi Asubuhi, kuzika Wafu wao na kwenda Shule. Wamasai ni wale wanaohama na Mifugo, hawana Makazi ya kudumu, wavaa Rubega na wanaume kuachia paja nje, Shule hawapendi, kuoga no, Kula na wake zao hadi Asubuhi no, wanakimbia Maiti n.k
 
Waarusha,ni sub tribe ya Maasai ambapo kihistoria kabila lao lilitokana na wamasai walioasi mila na desturi za kimasai kwa kufanya baadhi ya mambo ambayo sio mafundisho wala mapokeo ya kimasai,na neno 'waarusa'kwa kimasai ni waliokengeuka kwa tafsri rahisi,...moja ya makengeuko ya enzi hizo ni kuooana na wanawake wa kibantu,......wanaishi pembezoni mwa jiji la Arusha ni viunga vyake..koo maarufu ni Laizer,mollel,na lukumay..
N:B..wana tabia za wivu,husda,ubinafi,kupenda kesi na kujiona wajanja pindi ukiingia kwenye kona zao.
Hapo kwenye tabia zao hujakosea
 
Hakuna kabila la waarusha, Hawa ni wamasai walioasi kwa kuona aibu ya kuitwa Masai. Waliona aibu kutoboa masikio na Mila zingine za kimasai wakajiita Masai wa Arusha baaadae wajiita waarusha.

Wanaugomvi mkubwa Sana na wamasai kwa sababu wao wanafanya kila kitu sawa na wamasai isipokuwa kutoboa masikio.

Mwingiliano mkubwa na wameru imefanya lafudhi zao kubadilika kidogo
 
Naona watu mnabwabwaja tuu vitu msivyojua. Waarusha ni kabila na Arusha limetokana na jina la kabila na sio kabila kutokana na jina la Mkoa. Wamasai na waarusha wanasikilizana lugha kwa kiasi kikubwa na baadhi ya tamaduni zinaingiliana
 
Hakuna kabila la waarusha.arusha ni eneo.kabila ni masai.hao wanaojiita waarusha ni wamasai waliotoka kuchunga ng"ombe wakakimbilia arusha kulima.baada ya kumiliki maeneo mengi ya kilimo ndo wakaanza kujitofautisha na wale wa kijijini wanaofuga mifugo na ndipo hapo wakaanza kujiita waarusha.Ila lugha na tamaduni ni zile zile japo kwa miaka ya karibu vitu hivyo vimeanza kuathirika kwasababu yakimazingira.
 
Waarusha na Masai ni makabila mawili tofauti, waarusha ni wenyeji wa Arusha mjini, wao ndio wameuza maeneo yao ya maboma kwa wengine (wahamiaji) waliopo Arusha, ila nao wakati mwingine hujifunika mashuka kama wamasai.
ungejaribu kuuliz hata wazee, maana hapa haujaongea chochotee
 
Nimeona niingilie kati kusaidia karibia wote humu kasoro wawili wamejaribu kuelezea.Mimi Arusha naijua na nilikuwepo toka miaka ya 1968.Ni hivi zamani mji wa Arusha ulikuwa hauna maingiliano ya makabila sana wamamasai walikuwa hadi Ngarenaro,Moshono nk ukifika unawakuta wanafuata mila zao za kuvaa lubega.Kama ilivyo kawaida wamasai ni kabila ambalo ni wagumu sana kuacha mila zao za asili.Sasa maendeleo yalivyokuwa yanajongea taratibu waliokuwa wanakuwa rigid wakawa wakiona nyumba nzuri zinajengwa wakawa pia wanaona mifugo yao maeneo kufuga ni finyu wakawa wanaamua
kuuza maeneo yao na kusogea maporini.Wengine walioamua kukomaa kubaki ikabidi wabadilike wajenge nyumba za kisasa na kuvaa suruali kuachana na kuvaa lubega.Hawa sasa ndo likatengenezwa jina wakaitwa Waarusha.
Kiuhalisia kwa lugha nyepesi na rahisi Waarusha ni wamasai wa mjini na wamasai original ni wale wa porini walioko maeneo ya Ngorongoro na Kenya kwa Kenya mji wa Nairobi wakazi wake walikuwa wamasai..Hata hivyo mmasai ni normadic wakati mwingine anahama kulingana na malisho ya mifugo yake ndio maana wako Kilosa Morogoro,Mbeya,Iringa in principle Wamasai hawana kitu kinaitwa ukabila kabisa wana cope mahali popote pale hata Zanzibar wapo
Ila wako wanajisikia sana fahari kuitwa wamasai mfano Mhe Mzee Edward Lowasa na Marehemu Sokoine.
Lugha wanayotumia ni moja hiyo hiyo mtu asikudanganye kuwa hawaelewani.
 
Kwa uelewa wangu, waarusha ni wamasai wa mjini (civilised). Ila hawapendani kabisa. Wamasai wanakeketa, waarusha hawakeketi. Wote ni wafugaji, ila waarusha ni wafugaji wa kisasa. Wote hawatahiri hospitali.

Kina Seuri, Kibona, Babuu, na wengine tulikuwa nao fresh tu kitaa, ila walivyotoka Kibongoo (jando) wakajikuta superiors kisa tu chululu zetu zilikatwa hospitali. So yeah, wana ubaguzi flani hawa wote, au unaweza kuita pride kwa mtazamo mwingine.
 
Back
Top Bottom