Tanzania kuna uhaba mkubwa wa wachambuzi wa hotuba, watu wanategemea wanasiasa

Tanzania kuna uhaba mkubwa wa wachambuzi wa hotuba, watu wanategemea wanasiasa

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Ombwe kubwa la wachambuzi na wabobezi wa hotuba linapelekea kila mmoja kutoa tafsiri kwa utashi wake na mrengo wa aliko egemea maana wanao jikita kutaka kuchambua wengi wana mirengo ya kisiasa lazima avutie kwake.

Tumesikia hotuba bora ya kufunga mwaka ilivyojadiliwa kutafsiriwa kiupande mmoja bila kuichambua neno baada ya neno.

wengi wamejihisi wamelengwa wao wengine wamejigeuza ndio mabalozi wanawakilisha nchi zao ili hali ni watanzania.

Nchi inakoelekea ni kubaya kukosa watu wenye weledi kuufamisha umma.

Tunawaachia wanasiasa watuendeshe na mihemko yao!

Nchi yetu moja.

Lema alisema wapo tayari kuhesabiwa ikifika siku ya hesabu mbona anatoka nduki!
 
IMG_5563.jpeg
 
Kunanchi zinaongozwa na watu wenye maarifa duni mmmno na roho mbaya saana... Bila kuelewa kunamajinga yanafuata mkumbo kutetea vitu vya hovyo.
Kila kijana anajidai hodari kuchambua mpira kuchambua siasa waogaaaa
 
Tunaelekea katika Uchaguzi.

Porojo nazo zinakuwa nyingi, disinformation, misinformation nazo, spinners ndani, yaani kwa sasa ni mtaji kwa CHADEMA, Rais akiongea na wao wanataka kuongea na kushika headlines.

Wamekoroga kila kilichosemwa.

Nimekumbuka nyuma huko wanachadema walidai kuwa kuna "alternative truth"😊 labda safari hii nayo wanaona hotuba nayo ina alternative motives?....wakati kila mtu amesikia ama kuiona u tub hotuba. Wengine live hapa.🤔

Anyways Tanzania hakuna mazuzu🧐
 
Ombwe kubwa la wachambuzi na wabobezi wa hotuba linapelekea kila mmoja kutoa tafsiri kwa utashi wake na mrengo wa aliko egemea maana wanao jikita kutaka kuchambua wengi wana mirengo ya kisiasa lazima avutie kwake.

Tumesikia hotuba bora ya kufunga mwaka ilivyojadiliwa kutafsiriwa kiupande mmoja bila kuichambua neno baada ya neno.

wengi wamejihisi wamelengwa wao wengine wamejigeuza ndio mabalozi wanawakilisha nchi zao ili hali ni watanzania.

Nchi inakoelekea ni kubaya kukosa watu wenye weledi kuufamisha umma.

Tunawaachia wanasiasa watuendeshe na mihemko yao!

Nchi yetu moja.

Lema alisema wapo tayari kuhesabiwa ikifika siku ya hesabu mbona anatoka nduki!
Hili ni Janga jingine la Kitaifa. Hata the so called Intellectuals kwenye Vyuo vyetu nao siku hizi wako busy na kushughulikia matumbo yao kuwa chawa wa wanasiasa hao hao, so uchambuzi huru na wa kina haupo tena. Heri ya akina Dr.Bashiru na wenzake akina Dr Benson (kabla hawakenguka na kupotea njia) walikuwa wanajitahidi kuchambua na kushiriki mijadala kwa ustadi. The rest hata hao Intellectuals wamebakia kuwa sawa na wakulima wa kule Kasulu na Namtumbo, nao ni walalamishi tu na hawataki kutumia uwezo wao wa kitaaluma kuchangia hoja na kutoa maoni kwenye mambo makubwa ya Kitaifa. Tunaelekea wapi kama Taifa?
 
Back
Top Bottom