Tanzania kupeleka magari yanayotembea juu ya waya arusha (ngorongoro)

Tanzania kupeleka magari yanayotembea juu ya waya arusha (ngorongoro)

Calyx24

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2018
Posts
213
Reaction score
292
[http://www]

Arusha. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imepokea ujumbe wa wawekezaji zaidi ya 50 ili kuona maeneo ya kuwekeza katika eneo hilo ambapo utajengwa uwanja wa ndege eneo la Olduvai Gorge na kuanzishwa aina mpya ya utalii wa magari yanayotembea juu ya waya.

Mipango hiyo inatarajia kuongeza idadi ya watalii na mapato ya NCAA ambayo mwaka wa fedha 2017/18 yamevuka lengo baada ya kukusanywa Sh124 bilioni na lengo lilikuwa Sh121 bilioni.

Akizungumza kwenye ziara ya wawekezaji hao, Naibu Mhifadhi wa NCAA, Asangye Bangu alisema, ujenzi wa uwanja huo na kuanzishwa vivutio vipya vya utalii katika maeneo yaliyotengwa itakuwa fursa nyingine ya kuongeza watalii.

Alisema NCAA inahitaji wawekezaji wa ujenzi wa mahoteli, kambi za utalii, kuendesha utalii wa farasi, utalii na balloon na baiskeli.

Akizungumzia wawekezaji hao, Bangu alisema kwa muda mrefu wawekezaji wamekuwa wakiona maeneo lakini kumekuwa hakuna utaratibu wa kuyatangaza ili wakawekeze kwa lengo la kuongeza idadi ya wageni na muda wa kukaa.

“Kuna uwekezano mgeni kukaa mpaka siku saba hapa NCAA tofauti na sasa siku moja au mbili. Tumeona ni vyema tuweke mkakati mpya unaolenga kuongeza mapato kutoka kwenye utalii na tutakutana tena Julai 16, mwaka huu kwenye Jukwaa la wawekezaji eneo la NCAA," alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii nchini (Tato), Wilbard Chambulo aliomba kuwapo kwa uwazi katika maeneo ya uwekezaji ili kila mtu aweze kushiriki kushindana.

“Tunataka kuwe na uwazi awe Mtanzania au raia kutoka nje wote tukae mezani tushindane, mchezo wa kufichaficha uishe tunataka kushirikishwa kuijenga nchi yetu tunaweza na tunafaa,” alisema Chambulo.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya Miracle Experience, Hasnai Sajan alionyesha kuvutiwa na kuwekeza kwenye magari ya kuvutwa hewani na waya pamoja na balloon eneo la Ngorongoro.

“Ushirikishwaji huu ni mzuri, tukipata fursa ya kuwekeza tunaweza kuongeza zaidi wageni, maeneo ya Ndutu, Bonde la Ngorongoro na Embakai yanafaa kuweka magari ya waya yanayopita hewani,” alisema Sajan.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Tato, Henry Kimambo alisema uamuzi wa kuwashirikisha kwenye maandalizi ya GMP ni jambo muhimu kwani wao ndio wanaotumia bidhaa zitokanazo na uhifadhi.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ilianzishwa mwaka 1959 na ina ukubwa wa kilometa za mraba 8300.
 
Mliiponda sana Kenya kwasababu ya zile cable cars Mombasa. Eti project zingine hazifai Africa. Sasa mnasifia sana hii ya Tz. Huwa siwaelewagi hata kidogo.
Wewe ni moja ya wakenya wanaojua kiswahili sanifu na safii

Hongera kwa hilo ,kujifunza kiswahili toka Tanzania
 
Mliiponda sana Kenya kwasababu ya zile cable cars Mombasa. Eti project zingine hazifai Africa. Sasa mnasifia sana hii ya Tz. Huwa siwaelewagi hata kidogo.
Kuna tofauti hapo
Hii ni Ngorongoro
 
Nyie mmeweka Kama kivuko cha watu kitu ambacho hakifai, Sisi tumeweka Kama luxury na utalii zaidi
Ety hakifai, nyinyi hua wapuzi sana. Nadhani ni kwa kua akili zenu hua local tu. Hamna uzoefu kwa international affairs. Cable cars zimejaa duniani as a mode of transport, Wewe unatuambia mambo ya luxury hapa. Ushamba yenu itachukua muda kumaliza.
 
Kama hujui maana ya luxury ni heri unyamaze kuliko kujiaibisha.
 
Ety hakifai, nyinyi hua wapuzi sana. Nadhani ni kwa kua akili zenu hua local tu. Hamna uzoefu kwa international affairs. Cable cars zimejaa duniani as a mode of transport, Wewe unatuambia mambo ya luxury hapa. Ushamba yenu itachukua muda kumaliza.
Offcourse cable cars ni mode of transport kila mtu analijua hilo. Ila sio kila sehemu inafaa kuwekwa.
 
Ety hakifai, nyinyi hua wapuzi sana. Nadhani ni kwa kua akili zenu hua local tu. Hamna uzoefu kwa international affairs. Cable cars zimejaa duniani as a mode of transport, Wewe unatuambia mambo ya luxury hapa. Ushamba yenu itachukua muda kumaliza.
Akili zako sio nzuri Angalia over 80 percent of cable cars project kwenye nchi zilizoebdelea wameweka sehem gani, halafu nchi za ulaya au zilizoendelea kuna options nyingi watu wanaweza kutumia barabara, rail, au cable but you guys have no option wote mtakua mnasubiria usafiri mmoja kitu ambacho kitakua ni usumbufu na population ikiwa inazidi kukua day by day
 
Mbuga ya Manyara ndiyo ingefaa zaidi kwa Matumizi ya Cable Cars.
 
Akili zako sio nzuri Angalia over 80 percent of cable cars project kwenye nchi zilizoebdelea wameweka sehem gani, halafu nchi za ulaya au zilizoendelea kuna options nyingi watu wanaweza kutumia barabara, rail, au cable but you guys have no option wote mtakua mnasubiria usafiri mmoja kitu ambacho kitakua ni usumbufu na population ikiwa inazidi kukua day by day
Learn to think before you write. Kwanza it's not the main mode of transport, get the word MAIN deep into your head. Sasa ukisema hakuna other options of transport hio ni uongo pengine kama huelewi ambacho unasema. Pili it's about difficult landscape terrain, that's why cable cars are preferred na ya tatu ni Reliability kwasababu ziko fast na accessibility haina challenges mingi. Kabla mtu awekeze kwa biashara llote hua amefanya research na akajua challenges.
 
Back
Top Bottom