Si kuna tetesi kuwa anaepigwa vita pale ni Mfaransa dhidi ya Mmarekan ili asichimbe gas? Sasa vita tusioijua isije ikaturudishia vijana wetu kwenye majeneza yenye bendera ya Taifa bila sababu za msingi.
Alochukua contract kwa mara kwanza na alofanya savei ni mmarekani tangu 2005 akaingia mkataba ; rasmi 2011 wakaingia Palma kuanza maandalizi ya kazi chini ya Raisi Armando Guebuza!kampuni ilikuwa ikiitwa ANADARKO PROJECT LNG MOZAMBIQUE!!
Kipindi hicho chote ilikuwa ni ujenzi tu ukiendelea huku manyambizi yao yakiwa baharini wakiendelea na utafiti wao!walofanya kazi Mining wataelewa ninaposema ujenzi maana kbla mgodi wwte haujaanza production Duniani kuna construction work nyingi sana zinafanyika Kwanza!!
2015 alipoingia rais Philipe Jacinto Nyusi tatizo likaanzia hapo maana baada Tu ya kuapishwa aka simamisha KAZI sababu eti mkataba waloaingia na president Guebuza wakimagumashi pesa haionekani serikalini kazi ilipigwa bun almost 2years 2015-2017 miezi kama hii ndo kazi ikaanza tena!
Walipoanza Tu Anadarko after 2month Alshababy ndani ya nyumba 2017 hyo wakakinukisha hapo msimboa da praia ni wilaya iliyo karibu na Palma ilipo kazi rasmi, vilipigwa vita kama week hvi Mpka nyusi akaomba Msaada kwa Hayati wakaingia JWTZ huko wakawabonda sana wakakimbia hali ikawa shwari kazi ikaendelea!!
2017 ikaisha 2018 wakaanza tena sasa hvi si kwakupigana na majeshi ila kwa kuingia vijijini usiku na kuchoma nyumba; kuchinja wanaume afu wanasepa asubuhi kazi ni jeshi la msumbiji kuingia kusaidia Raia hali ikawa hvyo ikachanua alshababi wakajizatiti wakaanza kuteka makambi ya jeshi vituo vya polisi na kuwanyang'anya silaha na kuwaua wanazama porini hapo ndo serikali na hao wamarekani wakaanza kuogopa lkn kazi hazikusimama maana kwao hazikuwaathiri chochote wanyonge na masikini ndo walikuwa chambo!!
Nyusi akiulizwa anasema hakuna vita ni vikundi vya wahuni hvyo jeshi lake litapambana navyo kazi ikaendelea huku watu wanaendelea kuchinjwa serikali haitangazi chochote sasa wakahamia kwenye kuteka magari yakatekwa sana, yakapigwa risasi Sana abiria wakachinjwa sana maelfu!!
Sasa kisa cha ANADARKO kumuuzia kazi TOTAL ni hiki hapa 2019 mwezi February,ilikuwa hivi wilaya ya Palma ambayo ndo kutovu cha kazi ilikuwa haina Airport xo ukitaka kufika palma Kwa urahisi inabidi upande ndege mpka Msimboa da praia hii ni wilaya kubwa sana kuliko palma na ilikuwa municipal kabisa yenye kila kitu na uvuvi Sana tu ni kama KM 60 msimboa to Palma baada ya hapo unachukua gari kwenda Palma liwe private au public!!
Sasa huo mwezi wa 2 wazungu na baadhi ya wafanyakazi walikuwa wametoka likizo wakashukia airport msimboa da praia wakachukuliwa na gari za kampuni ya Anadarko kuwapeleka Palma ulikuwa msafara wa magari kama 10 hapo kuna gari 2 za Jeshi I mean escort moja inakaa mbele nyingine nyuma msafara ukaanza vzr Tu wakaiacha msimboa wakaingia palma SASA wao hawakuwa wanaenda palma center wao walikuwa wakienda ilipo Kazi na ma camp ya wafanyakazi kama KM 30 toka palma center hvyo walipofika kijiji cha mwisho ili waingie barabara itakayowapeleka huko kazini kwao wakakuta hiece imewekwa ktkt ya Barabara ina maana kuwa Alshababy waliteka hiece ilokuwa ikitoka palma kwenda msimboa wakachinja Raia wakalaza miili Yao barabani Hilo tukio lilitokea jioni kama saa kumi na moja bado mapema kabisa sema ni nje ya mji kdgo hvyo walipofanya hivyo wakachukua Ile hiece wakaigeuza ikaziba Barabara ina maana tyr walikuwa na taarifa kwamba kuna msafara wa wafanyakazi umetoka msimboa hakikisheni mnamaliza kazi!!
Gari ya Kwanza ilikuwa ya wanajeshi wanakuja kutahamaki jamaa hawa hapa Mita chache Tu kazi ikaanzia hapo risasi zikatembea sana gari zikapigwa rusasi matairi zinapoteza mwelekeo wazungu na wabongo wapo humo ndani ikabidi washuke waanze kukimbilia maporini zile za nyuma zikageuka kurudi msimboa gari zilizobaki zikapigwa moto xo kwenye Hilo tukio ikasemekana hamna kifo zaidi ni majeruhi na vifo ni Kwa wale abiria walotekwa kwenye hiece!!
Basi baada ya hilo tukio kampuni ikatangaza hali ya hatari hvyo kazi ikafungwa kwa mda usiojulikana wafanyakazi maelfu wakarudishwa majumbani mpka watakapoitwa tena;mwezi wa 6/2019wakaanza kuita wafanyakazi kdgo kdgo na hapo ndo taarifa zikaanza kusikika kwamba boss wa SASA ni TOTAL na sio ANADARKO tena na kweli mana uniform zote zikabadilishwa kwa wafanyakazi na kuwa na jina la total na sio anadarko tena mabango na matangazo huo ndo ukawa mwisho wa Mmarekani kuwepo palma akabaki mfaransa Total Mpka Kesho!!
Sasa mfaransa kaenda hali ndo ikazidi kuwa mbaya mpaka 2020 mambo yakawa magumu zaidi corona inapiga alshababy wanapiga sio mchezo kazi ikawa ngumu mara kupunguza wafanyakazi wengine wakawa wanakimbia wenywe coz ya usalama ni mdgo na alshababy wakapiga wilaya zote za pwani wananchi wakakimbia msimboa ikateketezwa kama mlivyoona na mwisho mwaka huu march wakapiga palma kitovu cha kazi na kazi ikaishia hapo mpka Kesho ndo hvyo tunaon a majeshi yetu yanapambana!;
Mwisho tutafute logic ktk Hilo swali lako mkuu je inawezekana wanatuchezea mchezo kutokana na maelezo yangu hapo juu?hicho ndo nnachokifahamu kwa ufupi Tu;mwanzo tulikuwa tunaamini mchezo unachezwa na mmarekani mwenywe ila SASA akaingia total ni yaleyale SASA hii imekaaje?na kama ni wao vipi wanaweza ruhusu mchezo uchezwe mpka kwenye pesa Yao?maana alshababy kuipiga palma mpka kazi imesimama hiyo ni akili kweli?kwamba wamewatuma waingie mpka kwenye himaya Yao!?anyway ya Mungu Mengi tuombe Mungu mission iwe possible Maisha yaendelee Hilo ndo la muhimu!!na log off!!