Tanzania kusoma imekuwa nongwa sana sijui tufanyeje

Tanzania kusoma imekuwa nongwa sana sijui tufanyeje

Elimu haijatusaidia.Kwenye swala la fikra,kutenda na maamuzi kuna tofauti ndogo sana kati ya aliyesoma na ambaye hajasoma.Ndo maana tumeweka ushabiki wa kisiasa na burudani mbele zaidi kuliko elimu na maendeleo.Elimu kubwa imebaki kujitambia tu ila haina kikubwa chakufanya kwenye jamii.
 
Elimu Tanzania imegeuka kichekesho maana hakuna anae jali sana kuhusu umuhimu wa elimu. Watu hawataki tena kujifunza na kutatua changomoto za jamii ila wanatafuta vitu ili kujitoa kwenye midomo ya wacheshi.

Ajabu hii wasomi wanadharauliana wao kwa wao kila mmoja anamuona mwenzie kilaza. Kumeibuka kundi la darasa la Saba B hawa ni wale waliobahatika kupata pesa pasipo kuwa na elimu kubwa hawa wanawaona wasomi kuwa ni vilaza tu. Elimu, Elimu, Elimu iko taabani Nani wa kutunusuru?.

Wasome wamegeuka kechekesho( laughing stock ) wao wao kwa wao wanaparuana na kulaumiana sijui tatizo nini? Anaemlaumu mwenzie ana wajibu wa kufanya anachokataka mwenzie afanye.
Afadhali umeliona hili. Sasa nawe kuwa mfano mwema. Tulijidanganya na kuamini kwamba ukeshasoma unakuwa umepata kibali cha kudharau wengine. Sasa naomba kila mmoja awe mfano kwa wengine na isiishie kulalamika tu.
 
Back
Top Bottom