TANZANIA KUA KITOVU CHA BIASHARA AFRIKA NDANI YA MIAKA 25 KWA LENGO LA KUKUZA UCHUMI.
UTANGULIZI
Tanzania ni nchi ambayo imepakana na Bahari ya Hindi upande wa mashariki mwa Afrika na kuzungukwa na Nchi nyingine nyingi upande wa Kaskazini, Magharibi na Kusini ambazo kwa miaka mingi zimekua zikiitegemea Bandari ya Dar es salaaam kama mlango mkuu wa Kupitishia mizigo yao kutoka ughaibuni hususani China. Hivyo kijografia Tanzania tuna fursa kubwa ya kua kitovu cha biashara kwa baadhi ya nchi nyingi za Afrika hususani nchi zilizoko Mashariki mwa Afrika, Magharibi, Kusini na Katikati ya Afrika.
Ndani ya miaka 25 ijayo kuanzia sasa yapo mambo mbalimbali ya kufanya/kuendelea kufanyika ili kuweza kufikia malengo ya kua kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika ambapo wengi tungependa kuiona Tanzania ya aina hii kwa miaka ijayo.
Kuboresha bandari zetu, ili ziweze kutoa huduma bora na kwa gharama nafuu ili kuleta ushindani kwa Nchi jirani, na kushawishi mataifa mengine kutumia Bandari hizi. Mfano Bandari ya Dar es salaam kwa mizigo itokayo ughaibuni na Bandari ya Kasanga na Karema kwa mizigo iendayo na itokayo Congo DRC.
Kuboresha vyanzo vyetu vya uzalishaji wa umeme ili kujihakikishia nishati ya uhakika kwa kipindi chote cha Mwaka. Hii itasaidia kuvutia uwekezaji katika sekta mbalimbali kama vile uzalishaji na usafirishaji lakini pia kuleta unafuu wa gharama za umeme kwa watumiaji wa ndani.
Endapo tutakua na nishati ya kutosha inayokidhi mahitaji ya ndani, ni vyema Serikali kupitia shirika lake TANESCO ilazimike kupunguza gharama za umeme kwa watumiaji wa ndani, Ili pia kuachana na matumizi ya nishati mbadala kama vile Mkaa, Kuni na Gesi ambazo zinaongeza ukali wa gharama za maisha kwa Watanzania. Ni vyema umeme wa ziada utakaozalishwa kuuzwa kwa Nchi jirani ili kuliongezea shirika la TANESCO kipato, na Kufidia gharama nyingine ambazo shirika hilo litakua likiwapatia wananchi kwa gharama nafuu ikiwemo maunganisho ya umeme.
Kuimarisha miundombinu ikiwemo kukamilisha na kuanza ujenzi wa reli ya treni iendayo kasi kwa mikoa ya Kagera, Mwanza, Rukwa (Kasanga), Mbeya (Kyela), Songwe (Tunduma). Hii itasaidia swala la usafirishaji wa mizigo mingi na mizito kwa wakati mmoja kwa njia ambayo ni salama na ambayo haitakua kero kwa watumiajia wa barabara kama ilivyo kwa sasa. Usafirishaji wa mizigo mizito kwa njia ya barabara sio rafiki kwani hupelekea matengenezo ya mara kwa mara ambayo huingizia serikali gharama zisizo za lazima.
mfano wa barabara iliyoharibiwa na magari ya mizigo mizito na kuitia serikali hasara (Picha kutoka Mtandaoni)
Kuingia mikataba chanya na rafiki na Nchi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa bidhaa duniani kama China, Na kuwapa fursa ya kuwekeza Tanzania kwa kuzalisha bidhaa ambazo kwa asilimia kubwa zinasafirishwa kutoka China kwenda nchi mbalimbali za Afrika. Pia kuingia mikataba na nchi mbalimbali za Afrika na kununua malighafi ambazo zitakua na manufaa katika uzalishaji, Lakini kwa bidhaa ambazo haziwezi kuzalishwa Tanzania kutokana na ukosefu wa malighafi Makapuni yapewe fursa ya kufungua ofisi za uwakala Tanzania ili kushawishi wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuja Tanzania badala ya kwenda China.
Ili kuweza kufikia malengo ya kua kitovu cha biashara ndani ya miaka 25, ni vyema pia serikali iboreshe mfumo wetu wa Elimu, uwe ni mfumo ambao unajikita zaidi katika kuzalisha watu wenye ujuzi katika sekta mbalimbali za uzalishaji kama vile ufundi wa samani, ufundi wa nguo, ufundi wa viatu, utengenezaji wa vifaa vya magari kama vile taa, makava ya viti vya magari (seat cover), Vifungashio vya karatasi, Mishumaa, Sabuni, Chaki n.k ili kuweza kutoa fursa ya kujiajiri na hata kufungua viwanda vidogo vidogo ambavyo vitakua vikizalisha bidhaa ambazo zitauzika nje ya nchi.
Kwa kua Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kua na vivutio vingi vya utalii, kama vile Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama, Mabonde na Visiwa, ndani ya Miaka 25 ni vyema kuimarisha shirika letu la ndege ATCL kwa kuongeza idadi za ndege na idadi ya safari za nje na kulitumia vizuri shirika hili kutangaza utajiri wa mali asili tulizo nazo ilikushawishi mzunguko mkubwa wa watu kuja zaidi Tanzania.
HITIMISHO
Endapo Tanzania itakua kitovu cha biashara kwa Nchi za Afrika, itasaidia kusukuma maendeleo Miji na vijiji mbalimbali na kuvutia uwekezaji zaidi kama vile ujenzi wa Hotel za Kisasa, Kukuza biashara katika miji mbalimbali, Pamoja na kutoa fursa kwa wazalishaji wengine wa ndani kama wakulima kwa kuuza mazao yao nje ya nchi na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Ongezeko la pato la Taifa litasaidia serikali kuweza kumudu gharama za kuihudumia jamii na kuboresha huduma mbalimbali kama vile Afya, Huduma bora za maji na Elimu, Na kuacha kuweka Tozo mbalimbali kwa ajili ya kuongeza pato la Taifa ambazo zimekua zikidumisha uchumi wa Watanzania siku hadi.
Ongezeko la fursa mbalimbali za kujiajiri kama vile biashara na usafirishaji.

Upvote
6