Kitu ambacho hamuelewi ni kwamba hatuwategemei nyinyi kwa chakula. Chakula tunacho chukua kutoka kwenu tunakinunua kwa cash, tena bei ya juu kuliko kama mkulima angeuza chakula hicho hapo Tanzania. Si msaada mnatufanyia, ni biashara kaka, na kama ilivyo kwa biashara its all about supply and demand.... Wakati ule JPM alileta kichwa kichwa biashara kati ya Kenya na TZ ilishuka hadi $180m (Sahii iko $1 Billion chini ya Mama), lakini si unga bado ulikua unapatikana Kenya? Uganda ndo walifaidi kwani tulikua tunanunua kutoka kwa, na Uganda walipopungukiwa tulinunua ziada kutoka Mexico na Brasil....
So hamuezi kutubabaisha na mahindi yenu, hata leo leo mkafunga mipaka, Kesho malori ya Uganda yatakua yamepiga foleni pale mpaka wa Uganda/Kenya yakingoja kuruhusiwa kuingia..... So nyinyi mshukuruni mama Samia kwa kua na akili timamu ya kugundua kwamba tit for tat nyingi zinaumiza wakulima na wanabiashara wa nchi zote mbili, mambo ya kujigamba kwa vitu vya upuzi na kuchoma vifaranga haisaidi mtu wa kawaida, ni sifa na kiki tu.... Biashara ni utulie nyamaze na uwache wananchi wachape kazi!