Halafu kuna mshikaji wangu alikua anafuata mbao na magogo Tanzania kitambo, alipiga hela sana jamaa enzi zile, sijamuona siku nyingi, itabidi Wakenya tuchangamkie hizi fursa, hawa watu wana ardhi kubwa ambapo kuna kila aina ya malighafi.
Vitalu vya madini ndio najua hatutapata maana tulichelewa, makaburu wa Afrika Kusini na Waarabu walishayahodhi na kujichukulia.
Tuanze kuamsha viwanda vyetu sasa malighafi ipo, ukizingatia hata DRC wanaingia kwenye jumuia ya EAC na liinchi lao lile, aisei mwendo wa kula kwa urefu wa kamba, au tukate kamba kabisa na kula kote.