Tanzania kwanini isitangaze rasmi lugha ya 3 ya taifa?

Lugha yetu ya Taifa ni moja tu,hizi nyingine ruksa kuzungumza nyumbani
 
Hauna akili wewe Kisukuma cha wasukuma. Lugha ya taifa ziendelee kuwa mbili English + Kiswahili. Wewe unataka kuleta ukabila . Na ukiona nchi ina malugha Mengi ya taifa kama Kongo na South kuunite watu ni ngumu Sana. Nchi zilizoendelea zina lugha moja ya taifa mfano USA, China , Germany, N.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wenzako tunahangaika kuondoa language barrier (and all other barriers of communication) we mwenzetu unataka kuturudisha nyuma kama enzi za kuanguka kwa mnara wa Babel!
 
Hicho kiingereza tu mtihani wangeanza kuboresha hicho kwanza lakini pia tuna kiswahili kama lugha mama kwanini tuingize lugha ya kikabila?? popote uendapo ukizungumza kiswahili watu wataelewa sasa kisukuma wakati Tz kuna makabila sijui 200, lol.

Nakataa hoja yako.
 
Bado kidogo tu utapendekeza kisukuma kitumike mashuleni kama lugha ya kifundishia kwa vile kinaeleweka na watu wengi!!!

kutoka: 22D Arnold st.
 
Sisi wataalamu wa lugha, tunasemaga "Hakuna lugha iliyobora kuliko nyingine" ila yofauti iliyopo ni jinsi lugha hiyo inaeleweka kiasi gani na kiasi gani cha jamii kinaitumia hiyo lugha. Watu wengi wanakielewa kisukuma na pia kinazungumzwa na watu wengi pia. Tukizungumzia habari ya kujirosheleza kimsamiati ni...Kinaweza kutohoa majina au maneno hayo kutoka lugha zingine na kuyafanya kuwa misamiati ya lugha ya kisukuma. Mfano kiswahili kimetohoa misamiati mingi sana si ya kwetu tumeiba kutoka lugha za wenzetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda ungesema kinyakyusa.. Maana ndo angalau lugha ambayo ina misamiati inayojulikana nchi nzima.. Na watu wanajisikia proud kutamka maneno ya kinyakyusa!
 
The Applicant must be fluent in English, Kiswahili and Kisukuma!!!
 
Ukiondoa kiingereza na kiswahili lugha inayoongeleka zaidi jf ni kinyakyusa
 
... Kichagga kipi bro? Cha Machame? Uru? Kibosho? Old Moshi? Marangu? Mwika? Mamsera? Mkuu? Mashati? au Tarakea? Maana kila baada ya hatua chache ni lugha mbili tofauti! Kama taifa tulishaachana na ukabila lakini!


Kisukuma nacho hakina tofauti kama hizo?
 
Kisukuma nacho hakina tofauti kama hizo?
... sina hakika japo uwezekano huo upo ila haiwezekani ikawa kwa kiwango cha kutisha kama Kichaga! Kwa mfano Kimasai; Kimasai ni Kimasai - no matter ni mmasai wa Tanzania au Kenya; Kiteto au Mkuranga; Kilosa au Katavi!
 
... isipokuwa India - 12 official languages.
 
Wagonjwa wa akili tunao mitaani then milembe tumepeleka wenye afadhali duh! Knifeclit my foot! [emoji848][emoji848][emoji848]

ᴾᵘⁿⁱˢʰ ᵒⁿˡʸ ʰᵉ ʷʰᵒ ᶜᵒᵐᵐⁱᵗᵗᵉᵈ ᵗʰᵉ ᶜʳⁱᵐᵉ✓
 
... sina hakika japo uwezekano huo upo ila haiwezekani ikawa kwa kiwango cha kutisha kama Kichaga! Kwa mfano Kimasai; Kimasai ni Kimasai - no matter ni mmasai wa Tanzania au Kenya; Kiteto au Mkuranga; Kilosa au Katavi!


Safi sana . Pendekeza na Kimasai nacho kiwe lugha ya Taifa. Kama ulivyosema kinavuka hata mipaka.
 
Safi sana . Pendekeza na Kimasai nacho kiwe lugha ya Taifa. Kama ulivyosema kinavuka hata mipaka.
... post yangu ya kwanza uliniyo-quote awali niko against na ukabila. Siwezi kupendekeza kitu cha aina hiyo!
 
Tupo karibia robo tatu ya watanzania, kwenye kupiga kura sisi ndio tunaamua nani atuongoze. Kuna siku tutaizunguka bongo yote tutaiweka mtu kati yani tutakua remote ya Tanzania yetu, I'm lake zonian.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…