Ukifuatilia kwa karibu namna gani viongozi wetu wanaendesha nchi hii kwa vyo vyote vile lazima utapata msongo wa mawazo. Kwamba hakuna kitu ambacho sisi Watanzania na hasa Watanganyika tunachoweza kukifanya bila msaada kutoka nje.
Ni kweli hatuna tekinolojia kubwa kufanya mambo makubwa kama kutengeneza ndege, injini za mitambo na magari, programu za computa nk na hivyo tunalazimika kununua au kukodisha. Lakini hili la kukodisha watu kutoka nje kutunza misitu yetu limenishangaza!
Misitu yote ya asili imejiotea yenyewe na haihitaji kumwagiliwa wala kupaliliwa, yenyewe inasubiri mvua na kuendelea kukua. Wananchi wanaozunguka misitu hiyo wamekuwa wakiitunza chini ya uangalizi wa serikali kwa gharama ndogo sana.
Sasa je ni shetani gani amewaingilia viongozi wetu kuwakabidhi hekta milioni nane za misitu Waarabu wa Dubai waitunze. Ni zimwi gani hilo lisilo na jina limewaingia vichwani viongozi wetu kumkabidhi Mmarekani mmoja hekta milioni sita za misitu amiliki na kufanya biashara.
Kweli wananchi wanaozunguka misitu hiyo wameshindwa kuitunza na kufanya biashara? Maeneo mengi yanayozunguka misitu hiyo hawana madawati katika shule zao! Nyumba za wananchi ni mbavu za mbwa na bahati mbaya wakikutwa na mazao ya mbao adhabu wanazopewa hazielezeki!
Enyi viongozi wetu kuanzia Rais Samia oneni aibu! CCM oneni aibu! Wabunge mchongo nyie oneni aibu!