Tanzania magari yaliyotumika nchini yanauzwa bei kubwa kulinganisha na iliyotumika nje

Tanzania magari yaliyotumika nchini yanauzwa bei kubwa kulinganisha na iliyotumika nje

Mleta mada Hebu tueleze kwanza wewe ungenunua IST toka nje ikakucost max 11.5mil
ukaitumia let's say miaka mitatu,
ukitaka kuiuza utafanya bei gani.
Ili tuone kama na wewe huna double standard
Au umenunua Landcruiser V8 2020 total
coast 179 mil
ushuru ikafika 106 mil
Jumla 281mil

Ukitaka kuiuza baada ya miaka 5 utauzaje?
By the way ushuru wa magari kwa Tz ni mkubwa sana unaumiza, yani gari mamlaka zetu zinasoma kama anasa au ndio ile sera ushuru uwe mkubwa kupunguza importation wakati sisi humu ndani hatutengenezi magari.

Lakini sio makosa ya muuzaji. Shida iko hapa

Kuna watu kufikiri kwao kuko chini sana wanaangalia kupiga pesa leo tu.

Ukiweka ushuru chini importation ya magari itakua kubwa
THUS
1. Clearing agent watapata pesa

2. Wauzaji wa petrol watauza zaidi, (utapata Kodi itakayozalishwa na kuuza petrol ndani na kodi ya kuingiza petrol toka nje), Ajira za wauza petrol station

3. Wauza matairi, vipuri, waosha magari,

Hivi ni baadhi ya vitu tu ambavyo vita-inject income kwa Central government.

Na ushuru huu kama ukipunguza wa uingizaji bidhaa nyingine tena kama nguo, viatu, (bidhaa zote zinazoagizwa nje) utaongeza wigo wa wafanyabiashara kupunguza bei na kuwauzia nchi jirani yani badala ya sisi kwenda Uganda kununua chupi na sidiria, Waganda ndio waje kwetu kununua

But kwa sasa hivi sisi tunakwenda kununua Uganda baada ya wao kupitisha mizigo yao hapa bandarini kwetu. Silly

Amin nakwambia bandari yetu ina uwezo wa kuilisha nchi bila kutegemea hata ndege.

Kwa waliosomea biashara

Law of maximizing sales
Sales maximisation is a theoretical objective of a firm which involves selling as many units of a good or service as possible, without making a loss. This means sacrificing some short-term profit with a view to achieving a longer term gain.

You reduce price--You raise sales---Higher profit at a short period of time

Higher price--lower sales--higher profit after a long period.

Nilikimbia IFM kwa sup lakini nilitoka na kitu
Huo ndio ukweli, lakini bahati mbaya wahusika na maswala ya uchumi kitaifa bado wanatunga sera. TRA wenye dhamana ya kukusanya kodi ni vihiyo katika taaluma hiyo. Wapo tu kwa sababu wapo.
 
Huo ndio ukweli, lakini bahati mbaya wahusika na maswala ya uchumi kitaifa bado wanatunga sera. TRA wenye dhamana ya kukusanya kodi ni vihiyo katika taaluma hiyo. Wapo tu kwa sababu wapo.
Wanasubiri mwanasiasa awaambie. Yani shida sana,
Wenye akili hawana mamlaka na wenye mamlaka .......
 
Nilikuwa namsaidia mtu kutafuta ist au raum au run x iliyotumika nchini, bajeti ilikuwa 6.5 to 7m. Nikajisemea kwa bei hii atapata gari ambayo itakuwa imetumika mwaka au miaka miwili nchini na itakuwa nzuri tu.

Matokeo yalinishangaza kidogo. Ukitaka kununua Gari iliyotumika hata 5 years nchini mfano ist, raum n.k inauzwa mil 8 mpaka hata 10. Gari hiyo hiyo bila ushuru iliyotumika nje ni m3 hadi 4, ukiweka na ushuru utalipa 10 mpaka 11.

Ukizingatia suala la uchakavu na kulinganisha na bei, gari lililotumika hapa litakuwa na bei juu sana.

Swali ni inamaana demand ya magari yaliyotumika nchini ipo juu sana au ni kitu gani kinasababisha bei kuwa juu?

Na wauzaji wa magari mapya yaliyotumika nje, si wanapata changamoto sana kushindana na bei hizi za magari yaliyotumika hapa?
...ukitaka kununua ndege tafuta na uwanja wako hahaaaaa
 
hao SBT na BEFORWARD ofisi zao ziko wapi?
Be forward wapo mtaa wa lumumba pale jengo la New ushirika tower floor ya 12,

Pia wapo jengo la apex towers, floor ya 5, Area 11,pale Gerezani.

Lakini pia wapo hapo mtaa wa msimbazi ukishaipita sheri ya big bone ukiwa unaelekea mataa ya fire kule direction ya upanga.
 
Be forward wapo mtaa wa lumumba pale jengo la New ushirika tower floor ya 12,

Pia wapo jengo la apex towers, floor ya 5, Area 11,pale Gerezani.

Lakini pia wapo hapo mtaa wa msimbazi ukishaipita sheri ya big bone ukiwa unaelekea mataa ya fire kule direction ya upanga.
na SBT wako wapi?na ukilinganisha kati ya Beforward na SBT kampuni ipi wako smart kwenye kuwahi kufikisha gari kwa haraka bila mambo ya kusumbuana kuacha kazi zako na kwenda kucomplain kila siku?si unajua waswahili walivyo
 
Lazma iwe hivyo maana kinachopendwa sokoni ndo chenye thamani siku zote iko hivyo.

Na ndio maana ni rahisi mtu kulanguliwa kwenye uuzaji wa toyota IST kuliko kwenye gari kama Crown,Brevis au Mark X. Dalali anatoa bei ya kuropoka gari ikiwa IST number D hata kama ni gari ya 2015 utalabuliwa 8.5M wakati thamani ya gari hio hio kwa kuagiza ni 10.5M! Kimsingi kwa miaka iliotumika hio gari ilipaswa iuzwe hata 4.5M ila tatizo ni nguvu ya soko.
Mkuu toyota wish 2007 kwa bei ya kuagiza mpaka kulipia ni shs ngapi? je ina ubora gani?.
 
GARI YA KUNUNUA KWA MTU KWA HAPA KWETU TANZANIA NI MAJANGA TU JAMAA YANGU KWANZA UTAPIGWA BEI, PILI UIMARA WA HICHO CHOMBO BADO HUKO MASHAKANI, SIWEZI MSHAURI MTU ANUNUE GARI KWA MTU LABDA KAMA UNAUZIWA NA NDUGU AU JAMAA WA KARIBU, LKN WALIOBAKI HAWEZI KUKWAMBIA UKWELI KWANINI ANAUZA HIYO GARI.
mkuu kwa daslam hii hadi ndugu wapigaji
 
mkuu kwa daslam hii hadi ndugu wapigaji
Hatari utasikia dalali anatamba gari haina kipengele....
2017 ndugu yangu mmoja alichukuaga gari kimeo asee tulikua mafundi mbona hadi leo tukiitwa kucheki gari tunakagua wenyewe tu mana tulipata uzoefu wa kutosha...

Gari ikiwa kimeo hadi uzito unapungua
 
Kununua gari kwa mtu ni changamoto.
Magari mengi yanauzwa na madalali ndio maana bei ziko juu kupita uhalisia, na mengi yana matatizo ambayo dalali hatayasema.

Jipe muda agiza gari kwa ma agent wa kuagiza magari.
 
Back
Top Bottom