Hizi ramani zimechakachuliwa. Nilipokuwa primary school wakati wa enzi za ukoloni, ramani ya kwanza ya Tanganyika tuliyotumia darasani ilionyesha mpaka wa Tanganyika ukipita katikati ya Ziwa Nyasa.
Dah wakisema wilaya ya Kyela nayo ni ya Malawi ina maana Mwakyembe na akina mimi ni raia wa Malawi,mambo mengine ni kutuletea shida tu wakati tulizonazo baado tunatabika nazo
huyu mama atakuwa anatumiwa na nchi za magharibi tuweni makini naye
Achana na mipaka isiyokuwa na kichwa wala miguu. Haiwezekani wananchi wa Kyela wasivue samaki na kutumia maji ya ziwa kwa kuwa eti ni mali ya malawi, kwani Kyela ilianza jana! Kwa hiyo mwananchi wa kyela akitaka kwenda Bambabay aombe visa malawi? Ninavyoongea mpaka sasa maji yale tunatumia kama kawaida na itakuwa hivyo milele. Wakibisha sana wajiandae kwa kichapo... Huu ni uhuni na ukizingatia maji mengi ya kujaza ziwa yanatoka Tanzania. Kama wanabisha tuwafuate lilongwe tukawachakaze. Halafu huyu mama yao(Rais Joyce) anajipendekeza sana kwa wazungu itakuwa vizuri sana kama watachapwa....
Hilo nalo neno!Hii inasikitisha sana kwa upande wetu!!!
Enzi za mwalimu iliwahi kutokea nakumbuka....lakini mwalimu alikuwa anamdhara sana banda!! Kupitia hotuba zake alikuwa
anatoa sababu mbili za kumdharau Kamuzu..
1. Raisi ambae hajui lugha ya wananchi wake!! anaongea kiingereza then anatokea mkalimani anatafiri kwa kichewa!!
2. Banda alishawahi kumdai mwalimu wanyakyusa/na makabila ya watu wote walioko mwambaoni mwa ziwa nyasa!!
alikuwa anadai eti ni wamalawi....nakumbuka mwalimu alikuwa anaipuuza sana kauli hii na kusema itakuwaje kwa wamasai
walioko kenya na yeye awadai!!!
.
Lkn kwa mnaofikiri njia ya vita inaweza kuwa suluhisho, inabidi wafikiri mara mbilimbili kwa serikali hii dhaifu tunaweza
kushinda vita yoyote ya kuihami mipaka yetu??.. JK anaweza kupeleka wanamziki wa TOT vitani tukapigwa nchi ikatekwa
hadi iringa!! Vita si mchezo inataka kiongozi mkuu awe na akili siyo dhaifu!!
Mie naona tuendelee kuwahimiza hawa viazi vyetu kina Membe..kuchukua hatua za ki-diplomasia haraka....
Huku tukisubiri kwa hamu uongozi wamaana utakapokuja mwaka 2015!!
Great Thinkers, You should trust your government, it is very stable and everything concerning the border conflict over lake Nyasa is under control.
Never jump to an issue brother.
Wanasema pia Kyela ni yao...
Suali ni kwamba kama Malawi inakubali mpaka wake na Msumbiji unapita katikati ni kwa nini basi wasikubali mpaka na Tanzania nao upite katikati?Mawazo yangu ni kwanza tutake haki sawa kwenye Ziwa, au tugawe mara 3 nchi 3 zinazopakana kwa usawa, au Tanzania tuchukuwe eneo letu na lile la Malawi pia, au hiyo kazi apewe Dr. Migiro afanye hiyo tu 24HRS akishindwa tuvamie kigeshi na kukalia upande wa Ziwa kati yetu na Malawi
Suali ni kwamba kama Malawi inakubali mpaka wake na Msumbiji unapita katikati ni kwa nini basi wasikubali mpaka na Tanzania nao upite katikati?
jokaKuu,Jasusi,
..kwani mpaka wa "Dosh ist afrika" kwenye ziwa nyasa ulikuwa wapi?
..Muingereza ali-negotiate na Wareno mpaka wa Nyasa Land na Mozambique.
..Je, ni nini kilisababisha wasi-negotiate na Wajerumani???
..hivi hayo maelezo ya Balozi Tsere do they make any sense to u ktk kuielewa position ya Tanzania?