Tanzania Military Intelligence vs TISS

Tanzania Military Intelligence vs TISS

Status
Not open for further replies.
Wadau nadhani kwakuwa wote tumeshapata picha kuhusu hizi idara mbili. Sasa hebu tuangalie wamefaulu vipi ktk kazi zao. Nitoe mfano tu wa Marekani ambapo CIA na intelligence organisations zingine zimefanikiwa kuifikisha Marekani hapo ilipo na kuwa Taifa lenye nguvu na sauti zaidi hapa duniani.wamefanikiwa hata kuiangusha dola kubwa iliyokuwa Hasimu wake mkuu yaani USSR. Hata hivyo kuna sehemu idara hizo za kijasusi za USA zilifanya makosa hata kugharimu maisha ya watu. Mfano tukio la Sep 11.

Sasa kwa hapa kwetu, mtizamo wangu ni kwamba Hizi idara zetu zimefanya mengi makubwa sana hasa hali ya usalama na Amani iliyopo kwa miaka mingi sasa, umoja wa kitaifa na Jeshi lenye Nidhamu kubwa sana ambapo hata baadhi ya nchi zilishasikika zikitamani kuwa na Jeshi lenye nidhamu kama Tz. Kwasababu inaaminika kuwa ni mara chache sana kukuta nchi masikini ikawa na jeshi lenye nidhamu. Mifano ipo mingi sana. Sasa yote hii ni kazi ya idara zetu hizi.

Success ingine ya idara zetu hizi ni ushindi ktk vita ya kagera. Kuna msemo kuwa ukiwa na MI imara basi ni rahisi kushinda vita hata kama adui ana silaha kuliko zako. Hata hivyo pamoja na success ya zaidi ya 90% lakini pia kuna sehemu kulifanyika mistakes. Mfano:-

1. Kushindwa kuzuia mashambulizi kwenye ubalozi wa Marekani. Jukumu la Tiss

2. Mabomu ya gongo la mboto na mbagala. Jukumu la MI. Walipaswa ku fore see.

3. Kutoroka kwa kanali Seromba. Kinachodaiwa kuwa sio raia wa Tz na ni Mrwanda. Kama ni kweli basi Vetting ya kujiunga na Jeshi is questionable kwani hadi kufikia cheo hicho ni kwanini hakubainika. Yamkini kuna wengine wengi wamebaki bado. Na kama ni kweli alikuwa ni raia wa nchi jirani basi ujasusi wao ni wa hali ya juu kuzidi wa kwetu kwani wameweza kumuingiza mtu akiwa na umri mdogo hadi anapata vyeo vi kubwa karibia na retirement age.

INGAWA MENGI YALIYOFANYWA NA IDARA ZETU NI MAZURI NA YALIYOTUKUKA LAKINI WANATAKIWA KUWA MACHO ZAIDI

mkuu, japo natoka nje ya mada lakini naomba unijuze kidogo apo kivip idara za USA walifanya mistake kwny sep 11.
 
Mbona USA na huko UK wanachukua watu ambao hawakuzaliwa nchi hizo kujiunga na Intelligence services za huko?
 
Sidhani kama kuna mtu anayejua mafunzo ya TISS yakoje isipokuwa wao TISS wenyewe! Wengi wenu humu mnatumia zaidi hisia kujenga hoja!!
 
Habari nyingi zinapatikana humo. Ukitaka kujua intelligence organisation za nchi mbalimbali utazipata tu na hata majukumu yao. Hata hizo za kijeshi yaani MI zipo humo na karibia kila Jeshi lina kitengo hicho na hizi idara kazi na majukumu yao ya msingi ni yaleyale sema namna zinavyo operate inaweza kuwa tofauti kulingana na mazingira ya kila nchi. Mfano ushushushu unavyofanyika kwa Taifa kama la Israel ni tofauti na sehemu zingine kama Tz kwa kuwa kule Tishio kubwa ni adui wa nje kuishambulia israel na hapa kwetu kwasasa Tishio linaweza kuwa ni Harakati za kisiasa zinavyokwenda na Suala la muungano ambapo lina maslahi ya kiusalama zaidi. Hivyo uki Google utapata mengi halafu una Digest na ya kwako. Ndivyo tunavyofanya humu kwenye Jamvi halafu tunapata maujiko utadhani Kweli tupo au tuna access na information za hizo ofisi. Labda tu kwa faida ya wengi ni kwamba msingi wa intelligence organisation hapa duniani umetokana na Jeshi ambapo kitengo hicho cha ushushushu kinajulikana kama MI ambapo ulihusu zaidi mambo ya kijeshi ndani na nje ya nchi hasa ktk kujua tishio na uwezo wa adui. Kwa wale wasomaji wa Bible kama utakumbuka wakati musa anawaongoza wenzake kutoka misri kwenda huko kunakosemwa nchi ya ahadi basi katika safari yao hiyo walikuwa wanatuma wapelelezi ili kujua uwezo wa adui au jeshi la nchi watakazopita na mashushushu wake ndio waliomsaidia kuwashinda maadui zake kila alipopita kwani aliwajua vizuri sana.Hivyo baada ya mabadiliko mbali mbali na maendeleo ya mataifa hasa baada ya vita kuu ya Dunia ndipo mataifa mengi hasa makubwa yakaanzisha intelligence organisation zitakazofanya kazi kwa mapana zaidi. Yaani zaidi ya mambo ya kijeshi. Ingawa MI bado ipo palepale. Ndio maana ukienda nchi kama uingereza utakuta wana Defence Intelligence au DI ambayo ipo chini ya wizara ya Ulinzi na wakati huohuo idara yao kama Tiss inaitwa Military Intelligence Section 6 na Military Intelligence Section 5, kwakifupi ni MI 6 na MI 5.Hizi idara zilianzisha na Jeshi kipindi cha vita kuu ya Dunia lakini baadae zikapewa majukumu mengine zaidi na mambo ya kijeshi na hazipo chini ya Jeshi au Wizara ya ulinzi, japo hata baada yakubadilishwa zimeendelea kutumia Jina lake hilohilo tofauti na CIA ilivyobadili japo nayo ukiangalia history background yake ilianzia Jeshini . Hizi facts zote nimepata kwenye Google

Ndio raha ya jamvi hili sasa, ndio maana nilistuka ulipoanza kuwakashifu "waalimu" wanaojitolea kutoa wanachokijua regardless of their "status" sababu kinachotakiwa ni hizo ABC's tu na sio "cores" mkuu au kwa bandiko hili nawe unakuwa "agent mbao"???!!!!
 
Mbona USA na huko UK wanachukua watu ambao hawakuzaliwa nchi hizo kujiunga na Intelligence services za huko?

Mtu kuzaliwa au kutozaliwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja na "uwezo au kuweza kumudu" yale anayotakiwa kuyafanya iwapo atapewa jukumu fulani nadhani!!!

Lakini wenzetu wako mbali sana kuweza kumchuja mtu na kujua kama anaviashiria hatarishi bila kujali kazaliwa wapi!!

Lakini pamoja na yote bado hawana uwezo wa kuishikilia dhamira ya mtu ndio maana wengine hugeuka hizo agency na kuwa "doubles" !!!

Hivi Snowden ni mzaliwa wa wapi huyu mtu!!!???
 
Mbona USA na huko UK wanachukua watu ambao hawakuzaliwa nchi hizo kujiunga na Intelligence services za huko?
Una maana hawana nasaba za huko? pia ujue kuna watu wanaopandikizwa kwa uraia feki. Yaani Mtanzania napandikizwa kenya kwa Uraia wa Kongo
 
Snowden ni aidha self deluded na hana threat kwa America au ana "kazi maalum". Vinginevyo tungekuwa tunaongelea habari tofauti

Kwenye hiyo michezo kujua nini ni nini na nani ni nani yaweza kuja mtu akisha expire au yuko kwa death bed ndio atapike!!!!
 
Unaweza kukuta sio mbumbumbu kama unavyosema. Wengine wanaamua kuwatega ili wahusika wazidi kutiririka tu. Thread kama hizi unaweza kukuta 70% wanaochomekea humu ndio wahusika. Halafu hao wenye majina makubwa mnaowaamini wanaotiririka karibia wote si ajabu ni makanjanja tu na hawajui lolote japo wanajitahidi kutafuta datas hasa kwa Google zinazohusu intelligence carriers halafu wakisha Digest vya kutosha huchanganya na thoughts zao . Sasa wengi humu wanajipatia umaarufu kwa taarifa za kubumba tu. Ninaamini mambo mengi ya intelligence ni Classified na intelligence officer wa kweli hawezi kuwaandikia humu sanasana atakuwa anaandika kama vile hajui. Disguise. Na sisi ma intelligence wa Mbao ndio tunajidai kutiririka na kujibu

Hahahaha.
 
Idara ya usalama wa taifa....idara ya usalama jeshini.....jeshi ni sehemu ndogo ya taifa na idara ya usalama wa taifa inawakilishwa na ina classified agents wake (undrcover) ndani ya jeshi na idara zake zote kwa ujumla....
 
Kwa nn jengo jipya la usalama lijengwe na contractor wachina na sio kamouninya kizalendo?
 
kuna jambo moja,,,askari wa jwtz kama kafanya kosa tu la jinai atakamatwa na askari polisi na kufunguliwa mashtaka regardless of his/her rank, halikadhalika afisa usalama (tiss). Akitenda kosa la kinidhamu atasokotwa na mp's humo humo ndani kwa ndani. Kuhusu uzalendo si kweli eti wanafundishwa uzalendo uliopindukia wengine bali wanalipwa vizuri. serikali inawajali zaidi benefits and other fringes ndiyo maana ni ngumu kufikiria lolote negative against government of the day@ccm
 
vp kuhusu hawa takukuru wao nao ni mashushushu? je wao wapo chini ya tiss au wanajitegemea kukusanya taarifa zao?
 
Huwa nawaonea huruma watz na fikra zao,intellgnc tanzania ni totl failure,kuna vitu kuviweka hapa ni kuhatarisha usalama lakin we fall behind,jwtz kuwa waburund,rwanda,kenya na wengne,upumbav wa mwsho kabsa ni kuwa hata mi6 wana watu gvt,na c.i.a siku wana recruit directl,wtf,kulikuwa na deadl mistake kule congo,mengne tuyaache hapa
 
Huwa nawaonea huruma watz na fikra zao,intellgnc tanzania ni totl failure,kuna vitu kuviweka hapa ni kuhatarisha usalama lakin we fall behind,jwtz kuwa waburund,rwanda,kenya na wengne,upumbav wa mwsho kabsa ni kuwa hata mi6 wana watu gvt,na c.i.a siku wana recruit directl,wtf,kulikuwa na deadl mistake kule congo,mengne tuyaache hapa

Funguka zaidi mkuu,,!
 
Una maana hawana nasaba za huko? pia ujue kuna watu wanaopandikizwa kwa uraia feki. Yaani Mtanzania napandikizwa kenya kwa Uraia wa Kongo

Enzi za uraia zimepitwa na wakati sana. Ingekuwa hivyo CIA FBI etc wasingekuwa that powerful. Hawa jamaaa waliamua kuchukua talents na wanazo vichujio kujua vipandikizi ni akina nani. Infact katoka historia yao mara nyingi moles ni raia waliozaliwa hapa hapa USA badala ya wale waliokuwa raia kwa kupewa.

Why do u think USA is so powerful? Simple kwa sababh walichukua na wanaendelea kuchukua vichwa vyote vyenye talent na akili duniani. Nyinyi bado mnapigana vita vya kiukooo na kikabila
 
Mkuu labda unajua zaid ya hawa tunaowaona wanajua na kukubali kujifunza kutoka kwao lakini kama usemavyo kama wanatumia google na kuweza kutuletea mambo tusiyoyajua nini mbaya wa hilo??!!!

Hivi google kwa nyie mnaoijua vizuri kuna hizi mambo zinazohusu hii comparison specifically kwa vyombo tajwa??!!!

Halfu na nyie mnaojua mambo msikae mbali mpaka tunaojifunza tupotezwe njia jamani. Hayo ma classified kaeni nayo ila japo msituache tukapotezwa!!


Jaribuni kutuweka sawa basi mana naona watu wanakanyagana tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom