Pale nyumbu kwanini wasitengeneze mabus kama haya Kwa ajali ya Askari wetu baadala ya kununua?
Hizi bus za kisasa hatari kwa vyombo vya usalama, ni rahisi kuwa chipped na kutumika kwa ajili ya spying.
Tungeanza kupunguza utegemezi wa baadhi ya military facilities na hardware na baadala yake tungeanza kuwa tunatengeneza wenyewe.
Kuunda bodi na chasis sio kazi, sidhani kama nyumbu wangeshindwa, tungeagiza engine kutoka weichai au hata man etc pure mechanical, mechanical gearboxes, na differentials halafu tunaagiza nyingine as spares lakini ni kwa ajili ya kustudy (copy and paste) na kuanzia hapo watalaam wetu wanaanza kufyatua zakwetu wenyewe.
Pale liganga Kwa kuanzia tungeanza kuchimba kile chuma Kwa ajili ya malitary hardware tu, na kila kwenye copper tungefanya hivyo na wahusika ni hao hao wanajeshi, hiko chuma kingetumika kutengeneza vifaa vya kijeshi tu.